in , , ,

TETESI ZA USAJILI LEO LEO

*Falcao atua Old Trafford, Chicharito Real Madrid
*Defoe kurudi EPL, Van Gaal atafutia sita pa kwenda
*Daley blind naye atua Old Trafford
*Danny Welbeck, aonekana Arsenal

 
Manchester United wamemsajili kwa mkopo mpachika mabao wa FC Monaco, Radamel Falcao wakati dirisha la usajili likielekea kufungwa usiku wa Jumatatu hii.

Kocha Louis van Gaal ameamua kuongeza mshambuliaji, japokuwa wapo vizuri mbele, ambapo tayari kuna ushindani baina ya nahodha Wayne Rooney na Nahodha wa Uholanzi, Robin van Persie.

Falcao ameingia Old Trafford kwa dili la pauni milioni sita na anaweza kusajiliwa na United moja kwa moja baada ya kipindi hicho. Alijiunga na klabu hiyo ya Ufaransa Mei mwaka jana kwa dili la pauni milioni 50.

Katika mechi zake 20 alizochezea Monaco msimu uliopita alifunga mabao 11 na katika msimu huu amefunga mawili kwenye mechi mbili. Ikiwa Man U watataka kumsajili akimaliza mkopo wake, watalazimika kulipa pauni milioni 43.5 kwa Monaco.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji wa Man U, Javier Hernandez ‘Chicharito’ amepelekwa Real Madrid kwa mkopo wa msimu mmoja.  Real wanajiimarisha baada ya kumuuza mshambuliaji wao, Alvaro Morata kwa Juventus.

Arsenal walikuwa wakijaribu kupata saini ya mshambuliaji wa Sevilla, Carlos Bacca na kiungo wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot wakati mshambuliaji wao, Joel Campbell ameomba kuondoka kwenda Benfica huku Man United wakitafuta timu ya kumchukua Danny Welbeck kwa mkopo wa pauni milioni tano.

Tom Cleverley alitarajiwa kuuzwa na Man U kwenda Aston Villa kwa pauni milioni nane, lakini tatizo alikuwa aking’ang’ania kiasi kikubwa cha mshahara. Sunderland walikuwa wakikaribia kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan, Ricky Alvarez.

Tottenham bado hawajakata tamaa na walikuwa wakiitafuta saini ya mshambuliaji wa   Southampton, Jay Rodriguez nao wawape winga wao, Andros Townsend katika sehemu ya dili la pauni milioni 14 kutolewa kwa Saints.

Kocha wa Southampton, Ronald Koeman alikuwa katika mpango wa kumsajili winga kutoka Norway, Nathan Redmond na mlinzi wa Celtic, Virgil van Dijk.

Kocha wa Sunderland, Gus Poyet alikuwa akipigania kumsajili moja kwa moja mchezaji wa Liverpool aliyekuwa kwao kwa mkopo, Fabio Borini wakati maofisa wa Valencia walikutana na mwakilishi wa mshambuliaji wa Manchester City, Alvaro Negredo aliyedaiwa pia kwamba Arsenal wanamuwania.

Mshambuliaji wa zamani wa Spurs, Jermain Defoe anatakiwa kwenda kucheza Queens Park Rangers (QPR). Kwa sasa anachezea Toronto na anataka kuondoka kwani kocha aliyemsajili, Ryan Nelsen amefukuzwa kazi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal sare tena

FUNGA KAZI YA USAJILI