in , , ,

TETESI ZA USAJILI HII LEO

*Manchester United wamepata matumaini makubwa kutokana na habari kwamba mshambuliaji wa Uholanzi wanayemhitaji, Memphis Depay (21) atakuwa sokoni.

Mkurugenzi wa PSV Eindhoven anakochezea, Marcel Brands ameliambia Shirika la Habari la Uholanzi ANP kwamba mchezaji huyo ataondoka kiangazi hiki.

Everton wanataka kumfanya kiungo wa Man United, Tom Cleverley kipaumbele chao kwenye usajili ujao.

Kwa sasa Cleverly (25) yupo kwa mkopo Aston Villa, baada ya Kocha Louis van Gaal kumweka kwenye kundi la wachezaji wasio na kiwango kinachotakiwa.

Tottenham Hotspur kwa upande mwingine, wapo kwenye mkakati wa kumsajili beki wa Schalke ya Ujerumani, Benedict Howedes (37) kwa pauni milioni 13. Huyu hucheza ama kama beki wa kati au wa kulia.

Kipa wa Chelsea, Petr Cech (32) aliyepoteza nafasi yake ya kwanza kwa Thibaut Courtois (22) anatakiwa na klabu ya Italia ya Inter Milan kuchukua nafasi ya Samir Handanovic anayekataa kusaini mkataba mpya.

Beki wa kulia wa Barcelona kutoka Brazil, Dani Alves (32) amekataa mkataba mpya wa miaka mitatu Nou Camp. Anatakiwa na Manchester United na Paris St-Germain.

Kkungo wa Chelsea, Marko Marin (26) huenda akapelekwa tena kwa mkopo, safari hii kwa Malaga ya Hispania.

Mchezaji huyu aliyezaliwa Bosnia lakini mwenye uraia wa Ujerumani kwa sasa yupo kwa mkopo Anderlecht.  Alicheza mechi 15 tu kwa Chelsea.

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amewatishia wachezaji wake kufanya mazoezi kwa muda mrefu usio na kikomo iwapo hawataongezeka kiwango.

Ametoa onyo hilo baada ya Napoli wanaofundishwa na Rafa Benitez kutolewa kwenye michuano ya Coppa Italia.

Zipo habari pia kwamba Benitez anataka kurudi Ligi Kuu ya England, alikopata kukaa kwa mafanikio makubwa Liverpool na kama kocha wa muda Chelsea.

Golikipa Pepe Reina aliyecheza chini yake katika klabu za Liver na Napoli kabla ya kwenda Bayern Munich amesema Mhispaniola huyo anaelekea kurudi England.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Walcott Liverpool, Sterling Arsenal?

Penati iliyorudiwa siku tano baadaye