*Arturo Vidal ajipeleka Manchester United

*Arsenal wanamtaka kiungo Juan Quintero

*Samuel Eto’o atakiwa West Ham United
 

Kiungo bora wa Chile, Arturo Vidal anadaiwa kufanya na kufaulu vipimo vya afya katika klabu ya Manchester United akiwa nchini mwake, licha ya kwamba bado Juventus hawajatoa ruhusa ya kuondoka kwake.

Vidal(27) aliye likizo kwao anatakiwa na Kocha Louis van Gaal hapo Old Trafford na kuna tetesi kila mahali kwamba atajiunga nao kwa gharama ya pauni milioni 47, pauni milioni 10 zaidi ya walizomnunua nazo Juan Mata kutoka Chelsea msimu uliopita.

 Wakala wake, Fernando Felicevich aliwasili Manchester Alhamisi hii kukamilisha mambo. Inadaiwa kwamba Vidal atalipwa £120,000 na kwamba atavaa jezi namba saba iliyovaliwa na nyota George Best, Cristiano Ronaldo na David Beckham hapo Old Trafford.

Man U walikuwa pia wamefikia pazuri katika mchakato wa kumsajili mlinzi wa Mats Hummels (25) wa Borussia Dortmund, klabu ambayo imeshawasiliana na Liverpool kwa ajili ya kumchukua kwa mkopo Tiago Ilori kuziba nafasi yake.

Arsenal wamemtoa kwa mkopo West Ham United beki wao wa kulia, Carl Jenkinson kutokana na kuwa na wachezaji wa kutosha wa kuaminika kwenye eneo hilo.

Kadhalika wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Colombia, Juan Quintero (21) anayecheza Porto ya Ureno na kuna habari kwamba atatua London Jumatatu hii kukamilisha dili linalodhaniwa kufikia pauni milioni 15.8.

Iwapo Quintero ataingia Emirates, inaweza kumaanisha kwamba Santiago Cazorla ataondoka kwenda Atletico Madrid anakotakiwa kwa muda sasa, ikizingatiwa Hispania ni nyumbani kwake pia.

Hata hivyo, Porto wametoa angalizo kwa Arsenal kwamba ikiwa wanamhitaji, itabidi wafikie kiwango cha pauni milioni 32 kilichooneshwa kwenye mkataba wake iwapo wanataka kumchukua. Wakala wa mchezaji huyo, Ricardo Calleri amesema itabidi Arsenal waongeze fedha.

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amethibitisha kwamba klabu yake inamuwania kiungo asiyetakiwa Manchester United, Marouane Fellaini, japokuwa bado mjadala ni iwapo ndiye sahihi au wasajili mwingine.

Liverpool wanaendelea na biashara ya usajili, safari hii wakitaka kuchukua walinzi wa Kihispania, Alberto Moreno wa Sevilla na Javier Manquillo wa Atletico Madrid.

Kocha Sam Allardyce wa West Ham anadaiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Cameroon aliyemaliza mkataba na kuachwa na Chelsea, Samuel Eto’o (33) lakini pia wanafikiria kumpata mshambuliaji wa Besiktas, Hugo Almeida.

Bosi wa mabingwa wa Hispania, Atletico Madrid, Diego Simeone anadaiwa kuandaa kitita cha pauni milioni 14 kwa ajili ya kiungo wa Manchester United, Shinji Kagawa baada ya kuwa tayari wameulizia juu ya uwapo wake.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

La Liga kuibomoa England

Lampard kutua Man City