in , , ,

TETESI USAJILI DIRISHA DOGO

Messi atajwa Manchester City

*Mourinho anamuwania Varrane

*Arsenal wanamzengea Hummels

*Man U kwa Marquinhos wa PSG

Huku nusu ya muda wa usajili katika dirisha dogo ukiwa umepita, inadaiwa kwamba Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini amefungua mlango ili mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani, Lionel Messi aingie.

Pellegrini, anadaiwa kwamba angependa kuwa na Messi, baada ya kuwa amemsajili mfungaji bora wa Swansea, Wilfried Bony kwa pauni milioni 28.
Hata hivyo, kuna wakati mgumu wa kuweza kumpata Messi, kwani bei iliyowekwa kwa raia huyo wa Argentina inadaiwa kuwa pauni milioni 480, kiwango cha juu mno.
Arsenal wameanza mazungumzo kwa ajili ya kuwasajili nyota wawili wa Borussia Dortmund kwa kitita cha pauni milioni 63.

Wakitaka kujiimarisha kwenye ulinzi na kiungo, Arsene Wenger anadaiwa kuandaa ofa kwa ajili ya beki wa kati Mats Hummels (26) na kiungo Ilkay Gundogan (24). Arsenal hawajasajili beki wa kati tangu kuondoka nahodha Thomas Vermaelen, lakini wanahitaji pia mabeki wa pembeni, hasa baada ya kuumia kwa beki wa kulia, Mathieu Debuchy majuzi.
Klabu ya Palermo wa Italia wnasema kwamba wamekataa ofa ya Manchester United kwa mshambuliaji wao mwenye umri wa miaka 21, kutoka Argentina, Paulo Dybala wanaoona ana thamani ya pauni milioni 30.
messssssi

Klabu za Paris Saint-Germain (PSG), Porto na Juventus zinapigana vikumbo ili kumsajili kwa mkopo winga wa Man United, Adnan Januzaj (19).
Wakati huo huo, Crystal Palace wanakaribia kufikia makubaliano na Swansea ili kumsajili mshambuliahi wao, Bafetimbi Gomes kwa pauni milioni nane.

Kocha wa West Bromwich Albion, Tony Pulis anataka kumsajili kiungo mkongwe wa Manchester United, Darren Fletcher (31) anayedaiwa kwamba huenda akatupiwa virago mkataba wake ukimalizika.
Swansea waliopata kitita kw akumuuza Bony, wanatarajia kuwekeza fedha hizo kwa kumnunua kiungo wa Stuttgart, Alexandru Maxim (24) kwa pauni milioni tano.

Manchester United wanadaiwa kuanza mazungumzo na PSG kwa ajili ya kumsajili mchezaji wa Brazil, Marquinhos (20) kwa pauni milioni 30.
Mshambuliaji wa QPR, Charlie Austin (25) ameziweka klabu kadhaa mikono wazi kwa kukataa kuhuisha mkataba wake hapo.

Liverpool wanalenga kumsajili kipa raia wa Australia, Mathew Ryan (22) kutoka Bruges kwa ajili ya kutoa ushindani kwa kipa wao chaguo la kwanza aliyeanza kuwa legevu, Simon Mignolet. Tottenham wameingia kwenye vita na watani wao wa kaskazini mwa London, Arsenal kumfukuzia mlinzi wa West Ham mwenye umri wa miaka 26 kutoka New Zealand, Winston Reid.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho yupo tayari kuondokana na hasara kwa kuwauza Andre Schurrle (24) na Mohamed Salah (22) ili amnunue beki wa Real Madrid, Raphael Varane (21).
Mshambuliaji wa Everton, Kevin Mirallas (27) amesema anahitaji muda kuamua atacheza wapi msimu ujao, kwa kuwa mkataba wake unakaribia kumalizika.
Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino amesema mshambuliaji wao, Emmanuel Adebayor (30) bado ana nafasi hapo White Hart Lane licha ya kutopata muda mwingi wa kucheza huku mkataba wake ukielekea ukingoni.

Kiungo Xherdan Shaqiri (23) amesema alikataa ofa za kucheza England ili ajiunge na Inter Milan nchini Italia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wajumbe wa Arsenal kutua Tanzania

TETESI ZA USAJILI LEO IJUMAA