Mourinho anamtaka Pogba
Kocha mpya wa Manchester United, Jose Mourinho anafikiria kutoa ofa
kwa Juventus ili kumsajili kiungo wake, Paul Pogba, 23, ambaye
japokuwa si rasmi, anaelekea kuwekwa sokoni kwa ajili ya usajili.
Mourinho anataka kukisuka upya kikosi cha United, ambapo inadhaniwa
kwamba atamuuza Juan Mata kama alivyopata kumwondosha Chelsea na
kumuuza kwa United. Inaelezwa kwamba mabingwa wa Hispania, Barcelona,
wanamtaka mchezaji huyo.
Kadhalika, Mourinho anataka Rio Ferdinand arejee Old Trafford ili
wafanye kazi pamoja kwenye benchi la ufundi lakini mlinzi huyo wa
zamani inaelezwa kwamba bado kufanya uamuzi wakukubali au kukataa kazi
hiyo. Hatima ya Ryan Giggs aliyekuwa msaidizi wa Louis van Gaal
haijajulikana pia.
Bosi huyo Mreno anataka Man U wamnunue kiungo wa Atletico Madrid, Saul
Niguez, 21 kwa pauni milioni 54. Man United wanaendelea kumfuatilia
golikipa wa Sunderland, Jordan Pickford, 22, kwa ajili ya kumsajili.
Mtendaji Mkuu wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke anasema kwamba
taarifa kuwa mshambuliaji wao, Pierre-Emerick Aubameyang, 26,
ataondoka klabuni hapo ni upuuzi mtupu.
Mshambuliaji wa Napoli, Gonzalo Higuain, 28, angependa kujiunga na
Liverpool wakati huu anapojaribu kushinikiza ili aondoke huko Italia.
Chelsea wanafikiria kumsajili mlinzi wa River Plate, Emanuel Mammana,
20, kwa pauni milioni nane, lakini wanakabiliana na ushindani kutoka
kwa klabu za Italia za Inter Milan na Fiorentina.
West Ham wamewasilisha mezani dau la pauni milioni 11.4m kwa ajili ya
kumpata kiungo mchezeshaji wa Juventus, Roberto Pereyra, 25, lakini
mabingwa hao wa Serie A wanataka pauni milioni 13.
Mazungumzo ya kuuzwa kwa Swansea kwa kundi la wawekezaji kutoka
Marekani unaelekeaukingoni.
Sunderland wanamfuatilia mlinzi wa QPR, Steven Caulker, 24, anayeuzwa
kwa pauni milioni 4.5 wakati beki wa kati wa Borussia Dortmund, Nevan
Subotic, 27, anaweza kutolewa kwa mkopo kwa msimu mzima.
Mabingwa wa Uturuki, Besiktas wanataka kumsajili kipa namba mbili wa
Arsenal,’ David Ospina, 27, kwa pauni milioni tatu.
Mabingwa wa Ujerumani wanakataa kmuuza mshambuliaji wao, Robert
Lewandowski, 27, licha ya wakala wake kufanya mazungumzo na mabingwa
wa dunia, Real Madrid.