in , ,

Sterling kwenda Man City

Raheem Sterling amekataa kufanya mazoezi na Liverpool

*Van Persie sasa atua Uturuki
* Schneiderlin kutuua United

Manchester City na Liverpool wanafikia makubaliano ya mshambuliaji, Raheem Sterling kuhama Anfield kwa dau la pauni milioni 49.

Sterling alikataa mkataba mpya wa pauni 100,000 kwa wiki, akagomea mazoezi kwa siku mbili na kukataa ziara ya Australia na Asia.

Liverpool walikuwa wakikataa kumuuza Sterling, 20, wakisema watabaki naye kwa gharama yoyote au kumuuza kwa pauni milioni 50 lakini sasa wameona bora aondoke maana hana nia njema nao.

Sterling sasa atakuwa ndiye mchezaji ghali zaidi Mwingereza anayecheza nchini England na alikuwa bado na mkataba na Anfield hadi 2017.

Tayari alikuwa ametajwa kwenye kikosi cha watu 30 kwa ajili ya ziara ya Thailand, Australia na Malaysia lakini jina lake liliondolewa baadaye.

Wachezaji kadhaa wa zamani wa Liverpool, akiwamo nahodha aliyepita, Steven Gerrard wamempinga Sterling kwa uamuzi wake wa kuwagomea Liverpool wakisema bado ni mdogo na si nyota kama anavyotaka kuonekana na hata kufikia kumwambia kocha Brendan Rodgers na Ofisa Mtendaji, Ian Ayre kuwa anataka aondoke.

SCHNEIDERLIN AKARIBIA UNITED

SCHNEIDERLIN
SCHNEIDERLIN

Kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin anakaribia kukamilisha hatua za kujiunga na Manchester United.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga Old Trafford kwa ada inayokadirwa kuwa zaidi ya pauni milioni 25 na Saints wamethibitisha kwamba wameshakubaliana na United.

Schneiderlin atakuwa ingizo jipya baada ya Mjerumani Bastian Schweinsteiger aliyetoka Bayern Munch, mshambuliaji wa zamani wa PSV, Memphis Depay na mlinzi wa Torino, Matteo Darmian.

Mshambuliaji wa kati wa Manchester United, Robin van Persie, 31, amewasili nchini Uturuki kwa ajili ya kujiunga Fenerbahce.
Alipokewa na washabiki wengi uwanja wa ndege wa Istanbul tayari kwa mazungumzo ya mwisho ya kujiunga huko.

RVP ameanguka katika kikosi cha Man U baada ya kocha Louis van Gaal kuona kwamba hana msaada kwake na alimwambia wazi asipojiimarisha kwa kiwango hatapata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Alisajiliwa United na Alex Ferguson akitoka Arsenal kwa pauni milioni 24 mwaka 2012 lakini sasa anaondoka kwa pungufu ya pauni milioni tano.

Ataungana na mchezaji mwenzake wa United, Nani, aliyejiunga huko wiki iliyopita baada naye kutupiwa virago United na kukataa kubaki Sporting Lisbon alikokuwa kwa mkopo msimu uliopita.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

MANCHESTER UNITED WAAPA

SCHWENSTEIGER NA SCHNEIDERLIN SI SULUHISHO KAMILI