Sterling : anaumiza vichwa vya Arsenal na Man City....

*Sterling apigiwa chapuo

Arsene Wenger, anadaiwa kutumia kukwama kwa mazungumzo baina ya Liverpool na mshambuliaji wao, Raheem Sterling kumchukua. Inaelezwa kwamba Sterling amekataa kusaini mkataba mpya na Liverpool, na klabu hiyo pia imeamua kwamba haitamuuza msimu huu. Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amemwelezea Sterling (20) kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi chipukizi wa Ulaya.

Sterling ni mchezaji mwenye kasi na uwezo binafsi wa kujipanga na kuwapita mabeki wa timu pinzani na hali hii inakuja wakati Jumamosi hii Liverpool wanacheza na Arsenal katika dimba la Emirates. Sterling apigiwa chapuo Arsenal Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, anadaiwa kutumia kukwama kwa mazungumzo baina ya Liverpool na mshambuliaji wao, Raheem Sterling kumchukua. Inaelezwa kwamba Sterling amekataa kusaini mkataba mpya na Liverpool, na klabu hiyo pia imeamua kwamba haitamuuza msimu huu. Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amemwelezea Sterling (20) kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi chipukizi wa Ulaya.

Hali hii inakuja wakati Jumamosi hii Liverpool wanacheza na Arsenal katika dimba la Emirates. Sterling anachezea pia Timu ya Taifa ya England, akiwa na asili ya Jamaica lakini amekulia nchini hapa, ambapo kwa muda ameshikilia nafasi ya Mwingereza mwenzake, Daniel Sturridge aliyekuwa majeruhi. Sturridge alijitoa kwenye kikosi cha England kilichokuwa katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2016 na mechi ya kirafiki kwa maelezo kwamba alikuwa na majeraha ya paja.

Mechi ya Jumamosi ni muhimu kwa ajili ya timu hizo kuwania kufuzu kwa nafasi nne za juu, Arsenal wakiwa kwenye nafasi nzuri zaidi, kwani wana pointi 60 katika nafasi ya tatu, huku Liver wakiwa nazo 54 katika nafasi ya tano. Chelsea wanaongoza wakiwa na pointi 67 Manchester City wapo nafasi ya pili kwa pointi 61 huku Manchester United wakiwa ya tatu kwa pointi zao 59 na wamecheza mechi 30 isipokuwa Chelsea wenye moja mkononi.

Hata hivyo, ikiwa Arsenal watafanikiwa kumnasa Sterling, inaelezwa kwamba wachezaji kadhaa watakuwa katika tatizo la kukosa namba au hata kuondoka klabuni, ikiwa ni pamoja na Theo Walcott mwenye historia ya kukabiliwa na majeraha. Hata katika Timu ya Taifa ya England, Walcott (26) huwa nyuma ya Sterling katika uchaguzi wa Kocha Roy Hodgson na si ajabu hali hiyo ikamkuta klabuni ikiwa Mwingereza mwenzake ataungana naye.

Wachezaji wengine ambao Wenger anajivunia kuwa nao ni pamoja na wale wapya wa msimu uliopita wa kiangazi, Alexis Sanchez na Danny Welbeck. anachezea pia Timu ya Taifa ya England, akiwa na asili ya Jamaica lakini amekulia nchini hapa, ambapo kwa muda ameshikilia nafasi ya Mwingereza mwenzake, Daniel Sturridge aliyekuwa majeruhi. Sturridge alijitoa kwenye kikosi cha England kilichokuwa katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2016 na mechi ya kirafiki kwa maelezo kwamba alikuwa na majeraha ya paja.

 

Raheem Sterling
Raheem Sterling

Mechi ya Jumamosi ni muhimu kwa ajili ya timu hizo kuwania kufuzu kwa nafasi nne za juu, Arsenal wakiwa kwenye nafasi nzuri zaidi, kwani wana pointi 60 katika nafasi ya tatu, huku Liver wakiwa nazo 54 katika nafasi ya tano. Chelsea wanaongoza wakiwa na pointi 67 Manchester City wapo nafasi ya pili kwa pointi 61 huku Manchester United wakiwa ya tatu kwa pointi zao 59 na wamecheza mechi 30 isipokuwa Chelsea wenye moja mkononi.

Hata hivyo, ikiwa Arsenal watafanikiwa kumnasa Sterling, inaelezwa kwamba wachezaji kadhaa watakuwa katika tatizo la kukosa namba au hata kuondoka klabuni, ikiwa ni pamoja na Theo Walcott mwneye historia ya kukabiliwa na majeraha. Hata katika Timu ya Taifa ya England, Walcott (26) huwa nyuma ya Sterling katika uchaguzi wa Kocha Roy Hodgson na si ajabu hali hiyo ikamkuta klabuni ikiwa Mwingereza mwenzake ataungana naye. Wachezaji wengine ambao Wenger anajivunia kuwa nao ni pamoja na wale wapya wa msimu uliopita wa kiangazi, Alexis Sanchez na Danny Welbeck.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

PSG wamtega Di Maria

England, Italia hakuna mbabe