in , , ,

Soka: Maslahi ya mabepari yanavyoiua

wawekezaji na wamiliki wa man City

Kimsingi kwa sasa soka inaendeshwa na uchu na maslahi binafsi ya mabepari, ikiwa tunataka kusema ukweli.

Hicho ni moja ya vitu vinavyoangusha hadhi ya soka na kwa hakika hiki na vinginevyo, vinahitaji uchunguzi na uchambuzi wa kina. Vyanzo vya habari karibu na Manchester City vinadokeza kwamba jamaa hao wa Etihad wameadhibiwa kwa sababu ya mwenendo ulioanza kuchukuliwa na kundi la klabu zenye ukwasi – kusajili wachezaji pasipo kufuata uungwana wa kanuni za fedha.

Inaleta udadisi sana juu ya hali inayoonekana kwamba Man City wameamua kuwa sehemu ya kundi la klabu hizo na kwamba wameshaingia kwenye mjadala wa kuanzisha ligi nyingine Ulaya – European Super League.

Mpango huu ni wa klabu kubwa za Ulaya kutoka ligi mbalimbali na umekuwa ukitumiwa kama tishio kwa klabu nyingine na mamlaka za soka za Ulaya pale kundi hili linapoona mijadala iliyo dhidi ya maslahi yao inaibuliwa.

Maofisa wa klabu hiyo, hasa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), Ferran Soriano – wamekuwa wakijielekeza pamoja na wale wengine wa klabu kubwa za Ulaya kuona kwamba rasilimali zinagawanywa kwa wingi zaidi kwa klabu hizo kubwa ambazo ni tajiri.

Sasa Man City wameadhibiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) kutoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) kwa misimu miwili kuanzia msimu ujao, kwa makosa ya kudanganya juu ya udhamini na ufadhili lakini pia kutumia kiasi kikubwa cha fedha kinyume na kanuni za uungwana wa matumizi yake lakini zaidi kukataa kutoa ushirikiano kwa shirikisho hilo wakati wa uchunguzi.

Suala hili la mabepari kuiteka soka na kuichukua ‘roho’ yake linawaudhi baadhi ya watu wanaoamini katika soka safi, akiwamo mwanahistoria wa soka anayeheshimika sana, David Goldblatt.

“Nafikiri kuna matarajio hasi kwa kweli. Klabu za soka zilikuwa zikijielekeza vyema kwenye mambo haya miaka iliyopita na hii ilikuwa muhimu sana hasa kwa nchi hii (England) ambako taasisi za ndani na utawala vinaonekana kuwa dhaifu. Tutapoteza au vinginevyo hadhi itashuka sana,” anasema Goldblatt.

“Haya ni matoke ya wakubwa wachache wanaotaka kuwa sawa – ubepari wa dunia unaoingizwa kwa nguvu kwenye mfumo. Maono makubwa ya utandawazi yanaonesha kwamba daimahuwa kuna washindi na washindwa, ikijenga watu wachache wenye maslahi pia kisiasa na watu wakabaki kudai kwamba haiwezekani kuwaingilia na sasa haya ni matokeo yake,” anaongeza.

Hata hatua ya FFP ya Uefa kuwafungia Man City ushiriki wa UCL inaweza kuligawa gemu, kutokana na hatua ya wamiliki na viongozi wa klabu hiyo kutokukubaliana na Uefa na kuamua kuendelea na shauri hilo mbele kwa rufaa, ikimaanisha ni vita ya kisheria. Ni suala jingine linaloweza kuwa kwamba fedha inaitawala na kuamua soka iendeshwe vipi, kwa kiwango kikubwa kuliko ilivyopata kutokea hapo awali.

Soko la soka linazidi kuwa kubwa zaidi na zaidi lakini si kwamba eti mshindi anachukua vyote kama msemona mantiki vilivyo, bali kagenge kadogo na matajiri. Soka inazalisha kiasi kikubwa sana cha kipato kutokana na udhamini au haki za televisheni lakini asilimia kubwa yake inanyakuliwa na klabu chache kubwa zikiacha zile ndogo zikichechemea.

Suala jingine muhimu la kutazama ni ule ukweli kwamba klabu hizi kubwa na matajiri wanasonga mbele na kujilundikia zaidi na zaidi kutokana na kutokuwapo na mfumo wa usambazaji wa mara ya pili, kwa mfumo wa kodi kwenye faida au vinginevyo; masikini wanazidi kuwa masikini, hata katika nchi tajiri.

Kuhusiana na ukosefu wa usawa kwenye soka ya Ulaya, Umoja wa Ulaya (EU) na Uefa wana mamlaka ya kutosha kuratibu soka, lakini ukitazama klabu kubwa za Ulaya na tamaa yao ya fedha, unajiuliza kuna maana gani hata? Na iwapo hata mamlaka husika zitathubutu kutunisha misuli yao dhidi ya klabu hizo. Kila mmoja sasa anajifikiria mwenyewe wala hakuna anayetafakari juu ya miradi ya pamoja.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Soka imeharibiwa isivyo kifani

Tanzania Sports

Uingereza kuzuia wasio na ujuzi kuingia