in , , ,

Siri gani inayompa ushindi Oliver Glasner

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu England amefungwa mechi tatu mfululizo. Mechi mbili amefungwa kwenye EPL na moja amefungwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Liverpool ya Arne Slots imekumbana na vipigo hivyo kwa sababu tofauti. Zipo sababu za ndani ya klabu yenyewe na zile za nje. TANZANIASPORTS inachambua moja ya mechi ya EPL ambayo ilifunga mlango wa kufungwa kwa Liverpool. Mechi hiyo ilikuwa dhidi ya Crystal Palace ambako Liverpool walikubali kipigo cha 1-0, kabla ya kukutana na vipigo vingine viwili; Chelsea walipata ushindi 2-1 katika mfululizo wa EPL na Galatasaray waliibuka na ushindi wa 2-1. Katika kipigo kutoka klabu ya Cryastal Palace ndiko aliko kocha Oliver Glasner. Je nini kilichitokea?

Sababu ya ndani ya Liverpool

Katika klabu ya Liverpool msimu huu, kama ambavyo TANZANIASPORTS ilivyochambua mara baada ya mchezo huo, kuwa wanakabiliana na changamoto ya mawinga. Liverpool walimuuliza Luiz kwenda Bayern Munich, lakini hawana mchezaji mwenye kasi kama nyota huyo. katika njia ya kukabiliana na changamoto hiyo Liverpool wanamtumia Gapko kama winga wa kushoto ili kuleta matokeo chanya kwa klabu yao. Liverpool wana kibarua kingine katika eneo la kiungo mshambuliaji ambako McAlister ndiye mchezaji anayeelewa falsafa ya timu hiyo. Mabadiliko kadhaa yanayofanywa bado wanakuwa na ugumu katika kulainisha mambo.  Ni sababu hii Liverpool imepunguza makali ya safu yake na kuhitaji ongezeko la wachezaji ambao wataleta chachu ya ushindi. 

Siri ya Crystal Palace 

Tanzania Sports
Ni mafanikio yasiyo ya kawaida”: Glasner asifu Crystal Palace baada ya ushindi wa kihistoria wa Kombe la FA

Crystal Palace waligundua namna ya kuwafunga mabingwa wa England. Siri kubwa ilikuwa kwa kocha Oliver Glasner ambaye aliwasoma vijana wa Arne Slot kisha kusabisha wafungwe mechi nyingine mbili. Je ni njia ipi waliyotumia kushinda? Akizungumza na vyombo vya habari katika tathmini yake juu ya mchezo huo, hakujua kama amefungulia njia ya Liverpool kufungwa. Kocha Oliver Glasner alisema, “mfumo wa timu, lazima uwe na wachezaji wanaofaa kutumikia. Kumekuwa na majadiliano mengi kuhusu mifumo ya uchezaji wa mechi kwa timu mbalimbali. Pengine mfumo si kitu muhimu sana ikiwa huna wachezaji wenye kuheshimu kazi yao. jambo muhimu ni kuhusu tabia, ni njia na shauku ya wachezaji kutimiza malengo ya klabu na binafsi. Je wachezaji wanaonesha tabia gani uwanjani, hiki ni kitu muhimu sana.”

Anaongeza kwa kusema, “katika taalamu yangu, nimewatumia wachezaji wengi kwa kila mfumo wa mchezo wa siku husika. nilipopandishwa nchini Austria nilitumia mfumo wa 4-4-2, kisha nilibadilisha na kutumia 3-4-3. Nilipohamia Wolfsburg, ambako tulifuzu Ligi ya Mabingwa kwa mfumo wa 4-2-3-1. Wakati nikiwa Frankfurt walicheza kwa mfumo wa mabeki watatu kabla, na tuliendeleza mfumo huo ukawasaidia wachezaji kucheza vizuri,”

Je nini kilichotokea kwenye mchezo wa Crystal Palace dhidi ya Liverpool?

“Siku zote naangalia mfumo ambao unawafaa wachezaji na kupata ubora wao. Mfumo wnagu ninaopenda ni 4-4-2, lakini je tunao wachezaji sahihi wa kutumikia mfumo huo? Kabla ya kupata majibu, tunazungumza kwa kina kuhusiana na mifumo hii na aina ya wachezaji waliopo, tunazungumzia kuhusu tabia zetu, jinsi tunavyokabiliana na changamoto au jinsi tunavyoweza kujisimamia na kusimamia miongozi ya kimfumo. Kwahiyo ni suala la kuzungumzia kwanza tabia zetu kuliko mfumo wa kucheza. Dhidi ya Liverpool, mfumo wetu ni laini na rahisi sana. ni muhimu kwa wachezaji kufahamu nini tunachotaka kwa mchezo husika na wafanye nini kuamua kuhusiana na mfumo wenye kuwaletea mafanikio. Eneo la kwanza lilikuwa kuvunja kiungo cha ushambuliaji, na la pili mabeki wa pembeni na tatu kasi yetu katika mfumo huo. Kucheza kwa kasi dhidi ya Liverpool unawalazimisha kufuata mfumo wako. Kwetu mechi inakwisha pale refa anapopuliza filimbi, kwhaiyo si ajabu kufunga goli dakika za mwisho. Ni suala la tabia za wachezaji wenyewe,”

Crystal Palace iliwashangaza maelfu ya mashabiki wa soka England kuwa timu yenye uthubutu kuwashambulia bingwa mtetezi. Gumzo hilo limeendelea hadi sasa kwani ni timu ambayo imewashangaza na kuonyesha namna ya kuwafunga. Katika mazingira hayo Oliver Glasner anakuwa kocha mwenye kufuatiliwa zaidi napengine kuhusishwa kwenda kufundisha timu kubwa zaidi ndani ya England. Haijulikani kama ataweza hilo, lakini kila kitu kinawezekana.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tarryn Allarakhia

Tarryn Allarakhia apewa mitano tena Taifa Stars

Tanzania Sports

Mataifa 20 tayari yamefuzu Kombe la Dunia 2026