Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu ligi mbalimbali zimerejea na kila timu imeanza harakati ya kutafuta utimamu wa mwili kabla ya mechi zenyewe, ambapo Tanzania Bara ligi itarejea Juni 13.
Arsenal ya England imeanza mechi ya kirafiki imemtandika Charton Athletics mabao 6-0 hii haina maana kuwa wapo bora au ndio tafasiri halisi ya kitakachotokea Juni 17 dhidi ya Manchester City majira ya saa nne na robo usiku kwa saa za Arika Mashariki.
Hayo ni maandalizi tu walimu wanaangalia wapi kuna mapunguu ili wapate kujaza zile nafasi vizuri, huu ni utamaduni wanchi zote duniani.
Yanga wamecheza michezo miwili ya kirafiki wa kwanza waliwatandika Transit Camp mabao 3-1, magoli yakifungwa na Mrisho Ngasa, Benard Morrison pamoja na Fesal Salum ‘Fei Toto’.
Mchezo wa pili ulichezwa siku ya jumapili dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni yaani Kinondoni Municipal Council (KMC), Yanga ilikubali kichapo cha magoli 3-0.
Tuanzie hapo sasa, huu mchezo ulikuwa kipimo halisi cha timu hiyo kwani kila mmoja ameona mapungufu makubwa ya utimamu wa mwili kwa baadhiya wachezaji wake lakini pia inaonekana hakukuwa na ufuatiliaji mzuri wa programu zilizo achwa na makocha wa timu hiyo.
Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa aliweka wazi kuwa timu haikuwa vizuri na wachezaji wake walikosa utimamu wa mwili na zile progamu hazikuwafaa au hawakuzifuata.
‘’Ni kweli wachezaji wangu hawakuwa vizuri kimchezo hawakuwa ‘fit’ kabisa, ila sasa tumeona mapungufu yetu na kupitia mchezo huu tutayafanyia kazi hatimaye tutarejea katika ubora,”alisema.
Udhaifu mkubwa ulikuwa kila sehemu kwani kuna baadhi ya nyota walicheza vizuri kipindi cha kwanza kilipoanza cha pili walichemka huku wengine waliboronga cha kwanza cha pili walirudi mchezoni.
Hii ‘Lockdown’ imewatibulia sana Yanga wanatakiwa wafanye nguvu ya ziada kwa kipindi kilichobaki ili warudi katika uwezo wao.
Mkwasa anatakiwa aangalie haya matatu, beki kukatika, viungo kushindwa kuelewana pamoja na ushambuliaji kuwa butu kabisa.
Katika mchezo wao dhidi ya KMC upande wa beki alikaa Kelvin Yondani na Andrew Vicent, hawakuwa katika wakati mzuri kabisa na ilionekana wazi Andrew Vicent alikosa utimamu wa mwili akifanya makosa mengi na kipindi cha pili alitolewa.
Katika kiungo aliweka watu watatu Feisal Salum,Haruna Niyonzima pamoja na Juma Makapu wote hawakufanya vizuri kabisa kipindi cha pili Feisali aliamka kidogo na kuonesha kauwezo japo sio kwa alivyozoeleka.
Katika sehemu ya ushambuliaji aliwaweka Ditram Nchimbi,Tariq Seif pamoja Balama Mapinduzi wanaonekana wazito sana huku wakishindwa kujiweka katika nafasi za kufunga nako anatakiwa aweke nguvu kubwa sana ili afikie malengo.
Mechi hizi ni muhimu mno kwa hizi timu zetu nandio utaratibu sahihi zitaweza kuwajenga sana kuelekea kurejea kwa ligi kuu bara.
Simba leo wamecheza mechi mbili za kirafiki ya kwanza ilikuwa asubuhi dhidi ya Transit Camp ambapo waliitandika magoli 4-2, magoli ya Simba yalifungwa na Deo Kanda, Fraga,Tairone na Meddie Kagere.
Jioni kikosi hiko kimeingia tena uwanjani kuchezana KMC katika uwanja wao wa mazoezi huko Bunju Complex Dar es Salaam.
Bado pia utimamu hauko vizuri sana japo kuna utofauti kidogo na watani wao jadi,kwa wahezaji wa Simba kila mmoja alionekana kuhitaji kurejea katika wakati mzuri .
Wote wamefanya uamuzi wa busara juu ya changamoto za kila timu zinaonekana na wengi walitarajiakuona haya yakiendelea kutokana na utamaduni wa Waafrika kupenda kujiachia.
Pongezi pekee ziwaendee KMC ambao wameonekana wanahitaji kubaki ligi kuu huku wakiwa ‘fit’ sana, timu hii inauwezo sana na huenda ikafanya vizuri katika ligi kila mchezaji anaonekana yupo vizuri.
Ndio maana walianza kutangulia kufunga goli dakika ya 32 goli limefungwa Charles Ilamfia ambaye hata mchezo wa Yanga alifunga pia lakini John Boko alijibu mapigo kwa kusawazisha goli zuri kabisa kipindi cha kwanza kimeisha kwa sare ya 1-1.
Kwa namna nilivyouona mchezo huu hapa Bunju KMC wapo vizuri sana huku Simba bado wanaonekana wako vizuri, na hii ndio tafasiri sahihi ya wachezaji kufanya mazoezi wenyewe kwa kufuata programu za walimu, ngumu sana ni bora kucheza ka pamoja.
Hadi mwisho wa mchezo huo Simba wameshinda magoli 3-0 John Bocco ameibuka kuwa shujaa wa mchezo huo kwa kuunga magoli mawili huku Ibrahimu Ajibu akiandikia goli la tatu.
Comments
Loading…