Simba ya Dar es Salaam jana ilivunja mwiko wa kutoshinda kwa muda mrefu katika uwanja wa Sokoine jijini hapa baada ya kuifunga Prisons kwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Bara uliochezwa kwenye uwanja huo.
Bao hilo pekee lililofungua minyonyoro ya Simba lilifungwa na David Naftal katika dakika ya 72 akiingia baada ya kutokea benchi akichukua nafasi ya Mohamed Kijuso.
Kwa mara ya mwisho Simba iliifunga Prisons kwenye uwanja huo mwaka 1997 kwa mabao ya Nteze John na Madaraka Selemani, ambapo tangu mwaka 2006 Simba ilikuwa ikifungwa bao 1-0 kila inapoganya kwenye uwanja huo.
Dakika ya 36 Simba ilipata pigo baada ya mchezaji wake hatari Danny Mrwanda kuumizwa vibaya juu ya jicho la kulia na David Mwantika na kukimbizwa hospitali na nafasi yake kuchukuliwa na David Naftal.
Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo, lakini aliwataka waamuzi kuwalinda wachezaji wanapochezewa rafu baada ya kuumizwa kwa Mrwanda na Mussa Mgosi.
Alisema kuwa mwamuzi Kamwaga Tambwe kutoka Ruvuma aliwaachia wachezaji wa Simba kuchezewa rafu bila hata ya kutoa kadi.
Naye kocha wa Prisons Hassan Mlwilo alisema kuwa timu yake ilicheza vizuri lakini itajitahidi kufanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya African Lyon utakaofanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine.
Prisons:Abdulrazak Jackson, Dickson Oswald, Henry Mwalugala, David Mwantika, Mbega Daffa, Sudi Ahadi, Said Mtupa/Seleman Msengi (dk. 74), Hashim Kahongo, John Matei, Benjamin Asukile na Ramadhani Katamba/Shaban Mtupa (dk.54).
Simba:Juma Kaseja, Salum Kanoni, Juma Jabu, Kelvin Yondan, Juma Nyoso, Mohamed Banka, Nico Nyagawa, Hillary Echesa, Mussa Hassan Mgosi/Adam Kingwande (dk. 78), Emmanuel Okwi/Mohamed Kijuso (dk. 61) na Danny Mrwanda/David Naftal (dk.39).
Naye Nathan Mtenga kutoka Ruvuma anaripoti wenyeji Majimaji ya Songea jana waliendelea kutoa pointi tatu kwa wageni baada ya kukubali bao 1-0 kutoka kwa JKT Ruvu katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji mjini humo.
Bao hilo pekee la JKT Ruvu lilifungwa na Hussein Bunu katika dakika ya 18, katika mchezo huo wa kuvutia.
mwaka huu hao yeboyebo watulie tu ni mwaka wetu sisi wekundu wa msimbazi,sababu kila kitu ni kizuri kuanzia timu mpaka uongozi uko sawasawa
sio hao prison tu hata hao yeboyebo wasubiri kilio chao