in ,

Simba walikuwa sahihi kupeleka kikosi cha kwanza MAPINDUZI

Kuna mengi yameanza kuzungumzwa sana baada ya mchezaji wa Simba, Erasto Nyoni kupata majeraha kwenye michuano ya kombe la mapinduzi.

Wengi wanalaumu sana na wengi wanawanyoshea vidole viongozi wa Simba kwa kupeleka kikosi cha kwanza katika michuano ya kombe la mapinduzi.

Michuano ambayo inaonekana haina umuhimu mkubwa kama michuano mingine. Michuano ambayo inaonekana kama bonanza kwa sasa.

Na kibaya zaidi Simba ina mechi za ligi ya mabingwa barani Afrika kuanzia tarehe 12 mwezi huu kwanza. Hapa ndipo lawama nyingi zinavyoanza.

Wiki ijayo kuna mechi muhimu, lakini wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza cha Simba wameanza kuumia.

Kiuhalisia lazima kama shabiki uchanganyikiwe na uanze kutoa lawama tu, lakini kiufundi Simba hawastahili lawama za aina yoyote.

Kwanini nasema hivo ?, kama Simba isingetumia michuano ya kombe la mapinduzi kwa kupeleka kikosi cha vijana kama Yanga walivyofanya ingekuwa hasara kubwa kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Kwanini nasema ?, wachezaji wa kikosi cha kwanza wangekaa bila mechi kwa kipindi cha wiki mbili. Bila kucheza mechi yoyote.

Kipi kingetokea kama wangekaa wiki mbili bila mechi yoyote? , timu ingepoteza umbo lake halisi (team sharpness).

Kukaa wiki mbili bila mechi yoyote ingemlazimu kocha wa timu ya Simba kurudisha umbo la timu kwenye mechi ya mashindano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Hapa ingekuwa hasara kubwa sana kwa Simba, kwa sababu wapinzani wake wangekuwa na umbo halisi la timu yao kwa sababu ya kucheza mechi za mashindano kabla.

Lakini Simba ndiyo wangekuwa wanahangaika kurudisha umbo la timu yao baada ya kupotea kwa kutocheza mechi ya mashindano kwa muda mrefu.

Pili, kwa sasa najua Simba inatumia kombe la mapinduzi kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi inayokuja ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Najua kwa sasa Simba inatumia muda mwingi kuwatazama wapinzani wao walivyo na namna ya kuwakabili.

Na kombe la mapinduzi wanalitumia kama njia moja wapo ya kujifunza namna ya kuwakabili wapinzani wao.

Kitu cha tatu ambacho ni kama mfano halisi ni kwa waoinzani wao waliowatoa yani Nkana Red Devil ambavyo waliathirika kwa kukosa mechi za mashindano.

Nkana Red Devil ni timu bora sana kuzidi Simba. Lakini moja ya sababu kubwa ambayo iliwafanya watoke kwenye michuano hii ni wao kukosa mechi ya mashindano.

Tazama ambavyo walivyokuwa wanacheza, walikuwa wanacheza kama timu ambayo inatafuta muunganiko.

Hawakuwa na ule muunganiko bora wa kitimu kwa sababu tu ya wao kutokuwa na mechi ya mashindano kwa muda mrefu.

Muunganiko wa timu wameanza kuutafuta kwenye mechi za mashindano ya kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika.

Kitu ambacho kilikuja kuwakuta na hiki. Wakati wao wanatafuta muunganiko wa timu kupitia mechi za mashindano ya klabu bingwa barani Afrika.

Wenzao walikuwa wameshapata muunganiko tayari kwa sababu ligi kuu Tanzania bara ilikuwa inaendelea.

Na ilikuwa imewasaidia Simba kutopeteza lile umbo lake halisi la timu. Ikawasaidia Simba kutopoteza ule muunganiko halisi wa timu kwa ujumla.

Kwa hiyo Simba ambayo tayari ilikuwa na muunganiko halisi , iliyokuwa na umbo lake halisi ilikutana na timu ambayo ilikuwa imepoteza umbo lake.

Timu ambayo ilikuwa inahangaika kutafuta umbo lake kwa kipindi hicho, hivo ikawa moja ya sababu ya Simba kupata matokeo chanya.

Moja ya madhara makubwa kwa timu kupoteza umbo lake halisi ni kuwa timu huwa na makosa mengi binafsi ambayo huyagharimu timu husika.

Pili, timu hukosa ile nidhamu ya kimpira , tatu timu hupoteza muunganiko wa idara zake zote uwanjani.

Aina hii ya timu ikikutana na timu yenye umbo halisi mechi huwa ngumu kwa timu ambayo haikuwa na mechi nyingi za mashindano kabla ya mechi husika.

Kwa hiyo naamini kabisa kiufundi Simba ilikuwa sahihi kabisa kupeleka kikosi cha kwanza katika mashindano ya kombe la mapinduzi.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Mwisho wa awamu ya tatu ya GALACTICO, tusubiri awamu ya nne ya GALACTICO

Tanzania Sports

Tumkabidhi rasmi Rashford jezi namba 10