in , ,

Simba vinara, Al Ahly ni vibonde tena?

Baada ya kupandwa na hasira za kuchapa chapwa na Simba, hatimaye Al Ahly walimsajili nyota Luis Miquissone…..

ZIMEBAKI siku ngapi? Bila shaka msomaji jibu unalo kuwa Simba watapepetana na Al Ahly lini na wapi. Kwa mara nyingine tena mabingwa wa soka wa zamani wa Tanzania, Simba wanatarajiwa kuingia dimbani kupimana ubavu na mabingwa wa Misri klabu ya Al Ahly katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya African Football League.

TANZANIASPORT imebaini kuwa Simba ni mwakilishi wa Tanzania mwenye rekodi za aina yake, na kwamba mashindano hayo yameipa thamani nyingine mbele ya vigogo wa soka barani Afrika. Simba wanaongoza katika rekodi ya kufika robo fainali kwenye mashindano mawili ya Afrika, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho. Simba imefanya hivyo kwa nyakati tofauti huku ikiwa imeoneshana umwamba na vilabu vikubwa kama Kaizer Chiefs,Orlandpo Pirates na Wydad Casablanca.

Mguu sawa wa Simba

Kwa mara kwanza Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi wa African Football League, na kuifanya kuwa klabu ya kwanza kushiriki mashindano hayo ya vigogo watupu kwenye soka. Simba wanaingia uwanjani wakiwa na hasira ya kulikosa Taji la Ligi Kuu Tanzania misimu miwili mfululizo. Lakini kwenye mashindano ya Kimataifa ni klabu yenye kuvitisha vigogo vingi. Simba wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na uzoefu mkubwa wa kuchuana na Al Ahly. Nahodha John Bocco, anatarajiwa kuwaongoza nyota wenzake Shomari Kapombe, Mohammed Hussein,Cletous Chama,Kennedy Juma watakuwa na kibarua cha kurejesha furaha kikosi cha Simba. Simba wanaingia kwenye mchezo huo wa ufunguzi wakiwa wanaongoza Ligi.

Al Ahly kibonde wa Simba

TANZANIASPORTS katika tathmini yake inathibitisha kuwa mabingwa wa kandanda barani Afrika Al Ahly ni vibonde wa Simba kwenye mashindano ya Kimataifa waliyokutana. Mara ya mwisho klabu ya Simba ilikutana na Al Ahly kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi msimu wa 2020/2021, ambapo vijana wa Tanzania waliibuka na ushindi wa bao 1-0. Rudi nyuma tena angalia, msimu wa 2018/2019 Simba waliizaba tena Al Ahly bao 1-0. Baada ya kupandwa na hasira za kuchapa chapwa na Simba, hatimaye Al Ahly walimsajili nyota Luis Miquissone. Winga huyo alikuwa moto wa kuotea mbali katika mechi alizokutana na Al Ahly. Wakati Al Ahly wakimsajili Mquissone, wenzao RS Berkane walimsajili kiungo mshambuliaji Cletous Cha,ma. Hata hivyo nyota wote wawili wamrudi Simba na wapo tayari kuoneshana umwamba na Al Ahly.

Mashabiki wapewe maua yao

Pamoja na timu za Tanzania kufanya vizuri kwenya mashindano ya Kimtaifa, lakini mashabiki wanastahili pongezi. Kila mechi wachezayo Simba, uwanja wa Benjamin Mkapa unajaza mashabiki wengi kiasi kwamba baadhi hulalamikia tiketi chache. CAF na FIFA wanatambua kuwa soka la Tanzania lina mvuto, lina pesa na Zaidi linasisimua Zaidi kutokana na klabu zake kuonesha ubabe barani Afrika. Popote penye mashabiki wengi na mvuto wa soka pamoja na mchanganyiko wa wachezaji wa kigeni na wazawa pana pesa.

Kujazana kwa mashabiki ndani ya viwanja maana yake CAF na FIFA wana uhakika wa kuvuna fedha nyingi kutoka kwa mashabiki wa Tanzania. Mpira ni mashabiki, kwahiyo wale wa Simba nao wapewe maua yao. Kama unabisha, jiulize sababu za CAF na FIFA kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mechi ya AFL. Mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 20 kwenye dimba la Benjamin Mkapa mechi ya marudiano itachezwa Oktoba 24 jijini Cairo nchini Misri.

Timu gani zingine zinazoshiriki AFL?

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF kwa kushirikiana na FIFA limeteua timu kadhaa kushiriki mashindano hayo mapya kutoka kila kanda. Ukanda wa  Afrika mashariki unawakilishwa na Simba (Tanzania) na TP Mazembe(DR Congo). Wakati ukanda wa Afrika magharibi unawakilishwa na klabu ya Enyimba ya Nigeria. Ukanda wa kusini mwa  Afrika unawakilishwa na klabu za Mamelodi Sundowns (Afrika kusini), Petro  DE Luanda (Angola). Ukanda wa Afrika kaskazini unawakilishwa na Al Ahly (Misri),Esperance (Tunisia), Wydad Casablanca (Morocco).

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Wakubwa wanaona aibu kisasi cha Yanga, Simba

Tanzania Sports

Akili ya Walid Regragui inafikiriaje Taifa Stars?