in

LoveLove SurprisedSurprised

Simba, Kaze Na Farid Kumtimua Kazi Zlatko

Zlatko Krmpotic

Nilikuwa nasubiri mechi tano ili niongee jambo juu ya kocha wa Yanga Zlatko Krmpotic ila naona kama nachelewa ngoja niyateme tu najua nitatukanwa itafahamika baadae.

Mechi tatu za Yang zote zijazo  watacheza uwanja wa Mkapa wataanza na Coastal Union, watakuja na Polisi Tanzania kisha wataumana na Simba Oktoba 18.

Endapo kocha huyu akiharibu zote tatu tiketi yake ataikuta uwanjawa ndege.

Ila baada ya kufanya tathimini juu ya muelekeo wa timu mechi ya Simba ndio itatoa jibu kama kweli anafaa kuendelea au kutimuliwa kazi.

Mkataba wake na Yanga wa mwaka mmoja kuna kipengele cha kumuongezea ila Yanga wameangalia mbali wana mapenzi nakocha Cedric Kaze hivyo kuna uwezokano mkubwa kama atatimuliwa hivi sasa watamrudia Kaze kama amemaliza matatizo yake.

Endapo bado basi kocha atakaye kuja hatopata mkataba mrefu atapewa kumalizia ligi na baada ya hapo Kaze atachukua hatamu.

Lakini pia kumuweka nje Farid Mussa huku viongozi wakisema anaumwa Malaria wakimkingia kifua kocha na hadhi ya siri ya timu nayo itakuwa sababu ya tatu kumtimu kazi.

Tanzania Sports
Zlatko Krmpotic

Maelezo marefu juu ya hawa watatu watakaomfukuzisha kazi kocha huyo yapo chini wewe endelea kusoma.

Unapotaka ugomvi wa matusi hapa Tanzania basi chokoza watu hawa wafuatao, Ali Kiba, Diamond, Yanga na Simba.

Hao ni miongoni wa watu na vitu vilivyo na wafuasi wengi sana ndani yake, na kama ilivyo ada ya Wabongo, ukizaliwa wewe Yanga au Simba, na katika muziki hivyo hivyo Ali Kiba na Diamond ‘Topic’  yao nitakuja nayo.

Kuna wakati kweli kabisa  watu wanaowasema wanakosea ila kuna wakati huwa wanapatia lengo kuweka mambo sawa.

TUMCHAMBUE  ZLATKO KRMOTIC

Mseribia Zlatko Krmpotic ndio kwanza ana siku 23 tangu achukue majukumu yakuifundisha timu ya Yanga ‘ Wananchi’, lakini mechi nne alizokaa kuwa mkuu wa benchi la ufundi bado kama kuna kitu hakieleweki.

Tangu afike amefanikiwa kucheza michezo 6 miwili ikiwa ya kirafiki na minne ligi kuu Tanzania bara.

Tulia, shusha punzi, haya twende sasa, ameshinda michezo yote ya kirafiki, ule wa kwanza katika siku ya Mwananchi  Yanga ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir Makamba ya Burundi.

Japo alikaa katika benchi alisema kuwa majukumu yote atamuachia Mwambusi kwa kuwa yeye ndio kaanza kufanya nayo mazoezi.

Bahati nzuri timu ilishinda 2-0  hivyo tunamtoa katika zile mechi alizosimamia.

Vipi ndugu yangu unaelewa nini naenda kukieleza hapop chini , basi usichoke wewe tiririka namie utaunga tela na tutaelewana.

Baada ya hapo ligi kuu Tanzani Bara ikaanza na mchezo wa kwanza na majukumu yake mapya dhidi ya Tanzania Prisons, mfumo aliotumia hasa wa Mwambusi lakini tunaanza kumpa yeye majukumu maana alikubali zigo la mwiba.

Bahati nzuri akaambulia alama moja katika mchezo ule uliomalizika kwa goli 1-1. Goli la Yanga limefungwa na Michael Sarpong huku la Prisons limefungwa na Lambert  Sabiyanka.

Tuangalie mbinu aliyotumia mchezo huo

Katika viungo aliwapanga Feisal Salum na  Zawadi Mauya  ambao waliutambaliza mpira chini, washambuliaji walikuwa Farid Mussa, Michael Sarpong na Ditram Nchimbi.

Mechi ya kwanza walicheza mpira kwakweli na nafikiri alitumia mbinu ile ile ya Juma Mwambusi ilimsaidia sana hasa kwa ugumu wa Tanzania Prisons.

Hili likapita wengi walisema tumpe muda ili tuone akiunganisha timu  maana kila mchezaji alikuwa anatumia uwezo wake binafsi.

Baada ya wiki timu hiyo ikaingia tena uwanjani kucheza  na Mbeya City  akabadilisha sehemu ya kiungo alimuweka  Mukoko Tonombe na Feisal Salumu balaa likaanzia hapa sasa.

Badala ya mpira kuchezwa chini ikawa pasi inatoka kwa kipa Metacha Mnata hadi kwa Sarpong.

Yaani inapita juu kwa juu nikawa najiuliza kazi ya viungo ni nini ? sikupata jibu nikawa nafikiria je kweli timu itaunganishwa kwa mfumo huu ? basi nikaamua kukaa kimya niangalie mechi nyingine huenda akabadilika.

Kwa namna mpira ule labda angecheza nje ya Dar es Salaam ambapo hakuna viwanja vizuri ningemuelewa butubutu ilikuwa nyingi kila mchezaji anauwezo wake binafsi.

Mbungi ikaja Kaitaba Kagera ambako nako kuna nyasi nzuri za bandia yaani uwanja mkeka kama kawaida.

Katika mechi ambayo ilibaki kidogo niseme kuwa huyu jamaa kama tukijaliwa uhai na punzi Krismasi hatuli naye bongo ila nikaamua kuchuna nione mchezo  unaofuata.

Katika michezo miwili Mbeya City na Kagera timu imeshinda ila ndo vile kanyaga twende.

Tukuja hapa Morogoro ambapo Yanga ilifanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar. Amejaza viungo wenye kaliba moja ambao hawana ufundi wa kupenyeza rupia ili Sarpong afunge.

Kibaya zaidi baada ya kuona Mukoko anaweza kufunga kamsogeza namba kumi ili afunge kamali yake imeliwa hakufunga na mara zote tulimuona akirudi nyuma kufanya majukumu yake tuliyomzoea.

Mbungi ya Morogoro ilikuwa mbovu sana lakini huenda pia uwanja ila dalili ya kuunganisha timu haikuwepo .

Angalia alivyofanya viungo wakabaji kawaweka Zawadi Mauya na Feisal wanacheza mshabala huku Mukoko ambaye pia mkabaji amesogezwa mbele jamani!!!.

Yote hayo yakapita baada ya mechi kocha msaidizi Juma Mwambusi ametamba na kusema kuwa ipo  siku timu itaungana na kufunga magoli 10  nimemuangalia nikaona moyoni anatamni kweli iwe hivyo ila kwa mfumo wa bosi wake anajua kabisa kazi itakuwa ngumu.

KWANINI YANGA WATAMUONDOA ZLATKO?

Kuna mechi mbili hapa kabla ya kukutana na Simba Yanga watacheza na Coastal Union kisha wataumana na Polisi Tanzania.

Bahati yake nzuri ashinde michezo hiyo yote asubirie nini kitatokea dhidi ya Simba ila akipoteza hiyo miwili na ule wa mtani wao nao kama akipigwa safari ya Serbia itamuhusu asubuhi na siku kuu ya Krismas huenda tukaila wenyewe kama tukiwa hai.

Viongozi wa Yanga watamuangalia muelekeo wake juu ya kuinganisha timu kwa michezo saba ambayo minne tayari imepita  watakuwa wameona kila kitu na dalili yake juu yakikosi hiko.

Sababu namba mbili itakayo muondoa Yanga wakati bado anaipenda  kumuacha nje Farid Mussa.

Afisa muhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz alisema kuwa nyota huyo aliumwa Malaria kabla ya mechi yao dhidi ya Kagera Sugar  hivyo isingekuwa rahisi kucheza.

Maelezo ya ndani kabisa juu ya sakata la Farid Mussa zinasema kuwa yeye mwenyewe haelewi kwanini kocha anamuweka benchi ila yuko fiti.

Basi sie kazi yetu kuangalia tu huu mchezo kama tulivyomuandika alivyokuja na akiondoka pia tutaeleza.

Cedric Kaze

Yanga wajanja nyie Zlatko wamempa mkataba wa mwaka mmoja lakini kuna mazungunzo  yalienda vizuri juu ya kocha waliyekuwa wanamuhitaji tatizo la kifamilia likamfanya  asitue Yanga .

Imefahamika kuwa Yanga wanamuangalia kocha huyu kwa mwaka mmoja na wakati huo Kaze huenda matatizo yake na familia yatakuwa yameisha kabisa akaja kuchukua kazi Yanga.

Mkiona nawadanganya subirini muone , chukueni kipnde hiki bakieni nacho kisha yakitimia nitawaambia.

Na endapo Zlatko akifukuzwa kabla ya mwaka mmoja watarudi kumuuliza Kaze kama bado huyo atakaye chukua jukumu atasainishwa mkataba wa muda mchache.

Na nasema kuwa Zlatko atafukuzwa mapema zaidi kuliko   Sven Vandenbroeck, huyu jamaa ‘Movie’ yake itamjia ligi ya Mabingwa Afrika.

Vipi mmetosheka hapo au bado povu lipo , basi ‘Comments’ za povu ziwe fupi fupi.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

75 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Carlos Carlinhos

Carlinhos hafanyi mambo mengi..

Man city

Ni lini Man City watajifunza kwa makosa yao?