KAZI ya kuwa kocha wa timu ya Taifa ni ngumu pale masuala ya siasa yanapoingizwa na kuwakosesha uhuru makocha wake. kwa kuona hili kocha wa England ameonesha dhahiri hataki siasa kwenye kazi ya kuinoa timu hiyo. Thomas Tuchel ameonesha kuwa hana mpango wa kuingiza wala kusikiliza siasa za mpira kwenye kazi yake ya ukocha wa timu ya Taifa ya England na amesisitiza mbele ya vyombo vya habari kuwa kutakuwa na faida kubwa ikiwa atakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kocha huyo amesomba wadau wa mpira wa miguu na viongozi wa kisiasa kumwacha ajikite kwenye kazi yake kwa uhuru kuliko kumwingiza kwenye masuala ya siasa ambayo ameai yanavuruga utaratibu wa utendaji wake, hivyo hataki. Ifahamike kuwa hapa England sualala siasa kuingizwa kwenye mchezo wa soka hasa Timu ya Taifa limekuwa jambo la kawaida na ambalo kwa namna moja au nyingine linawakera makocha wengi ingawaje baadhi wanachagua kunyamaza. Kipindi cha miaka 8 ya ukocha ya Gareth Southgate alikumbana na matatizo ya siasa na utamaduni kwenye kikosi chake cha Taifa. Mara kadhaa alilazimika kujibu ay kutolea maelezo masuala ambayo yalihusishwa na siasa za mpira kuliko kazi yake ya ukocha.
Hata hivyo kwa upande wake Thomas Tuchel, ameweka msimamo wake kwamba yeye si mwanasiasa na hataki siasa kwenye kazi yake. Tangu alipokuwa kocha wa Chelsea alikuwa kocha mgumu kuwekwa mezani kuzungumzia masuala ya siasa. Kipindi alichokuwa kocha wa Chelsea anatajwa hakuwa mtu rahisi kuzungumzia uvamizi wa Russia uliofanywa huko Ukraine baada ya Roman Abramovich kuondolewa katika usimamizi wa kila siku wa klabu hiyo.

Alipoulizwa kabla ya mchezo wa kwanza akiwa kocha wa England wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Albania kwenye dimba la Wembley, kama anaweza kuelewa ishara za kisiasa za England katika kazi yake ya ukocha alisema, “Awali ya yote, nafikiri mkataba wangu umenitaja kama kocha mkuu na sio meneja wa timu. Ninajaribu na ninafuraha kwamba Mkurugenzi wa ufundi John McDermott na Afisa Mtendaji Mark Bulligham wananiunga mkono katika kazi yangu, ambao pia wanatekeleza majukumu yao katika chama cha mpira cha England, FA na wanazungumza na mimi juu ya maslahi ya FA. Nafikiri ninapata nafasi nzuri ya kufanya kazi kwa uhuru kama kocha na kuelekeza akili yangu kwenye mpira wa miguu.”
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 raia wa Ujerumani aliongeza kwa kusema, “Naelewa kulingana na mtazamo wako pengine upo umuhimu wa nafasi hii kuzungumzia siasa au kuhusishwa nayo, lakini naweza kujiweka pembeni kidogo kuzungumzia siasa, siwezi kuzungumzia kila kitu kinachotokea kwenye nchi yenu, na kwa heshima hiyo napenda kuelekeza akili yangu kwenye mpira wa miguu.”
Matukio ya siasa kuingizwa kwenye timu ya Taifa yamewahi kutokea mwaka 2022 wakati wa Kombe la Dunia ambapo England ilitaka kuvaa utepe wa upinde ambao unahusisha masuala ya mapenzi ya jinsia moja. Mpango huo ulilenga kufanya kampeni dhidi ya wenyeji wa kombe la dunia Qatar ambao wana sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja. Hata hivyo FIFA waliamua kupiga marufuku mpango huo.

Tuchel amesema kwamba kwa suala hilo hawezi kuzungumzia kwa sababu si sehemu ya mipango yake, badala yake anasema yuko tayari kuzungumzia mpira na masuala ya kiufundi yanayohusiana nayo. “nadhani unaweza kutoa maoni yako mara moja au kadhaa, lakini kwa kiasi fulani lazima niruhusiwe kufanya kazi yake kwa ajili ya timu, mfano ilibidi kushughulikia timu iliyopelekwa Qatar kwenye kombe la dunia kama timu ya mpira wa miguu na sio kutoa matamko ya kisiasa, ama shughuli za kisiasa kwenye timu ya mpira w amiguu, hilo hapana. Kuwa mtu wa kutoa matamko ya siasa na kufanya akzi ya siasa kwa namna yoyote ile inaweza kuendelea bila kuhusisha timu ya Taifa England. Kama havitenganishwi hivi maana yake inakuwa timu ya kisiasa na watu wa chama cha soka FA wanapaswa kuzungumzia maoni yao, tuzingatie nafasi za utednaji. Nipo hapa kusaidia ili mwishoni wenye uamuzi wafanya kwa ajili yenu na mpira wa miguu, lakini kuzungumzia siasa kwa mchezaji wa mpira wa miguu inamsaidia nini katika kazi yake? Au kocha atafanya nini na hiyo siasa kwenye timu ya Taifa?”
Msimamo wa Tuchel unadhihirisha kuwa changamoto ya England ni kuendekeza siasa kwenye mchezo wa soka. Gareth Southgate amewahi kupitia wakati mgumu ikiwemo masuala ya utamaduni ambapo ubaguzi ulichukua mkondo mkubwa kwa baadhi ya wachezaji wenye asili ya Kiafrika wlaibaguliwa kwa sababu ya kukosa penati kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, maarufu kama Euro.
Comments
Loading…