in , , ,

Schweinsteiger huyoo Man United

Kiungo wa Bayern Munich na Ujerumani, Bastian Schweinsteiger anaelekea kukamilisha uhamisho kujiunga na Manchester United.
Schweinsteiger, 30, atapewa mkataba wa miaka mitatu, ikiaminika kwamba atachuma kadiri ya pauni milioni 7.2 kwa mwaka.

Mchezaji huyu mwenye uwezo mkubwa anatajwa kufurahishwa mno alipopata habari kwamba Man U walikuwa wakimuwania, na ada ya uhamisho ni kwenye pauni milioni 5.75.

Schweinsteiger alikuwa katika kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia nchini Brazil mwaka jana. Kuingia kwake United kutaimarisha kwa kiasi kikubwa sehemu ya kiungo.

United wameshamsajili pia Memphis Depay ambaye ni mshambuliaji kwa ajili ya kunoa safu hiyo ambayo kocha Louis van Gaal anasema ni tatizo kubwa.

Misimu miwili iliyopita United walikuwa doro licha ya kuwa na washambuliaji kama Wayne Rooney na Robin van Persie na msimu uliopita wakamwongeza kwa mkopo Radamel Falcao na bado hawakufanya vyema.

Kusajiliwa kwa Schweinsteiger kunaweza kumaanisha kwamba United wataachana na mipango yao ya kumsajili kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin, 25.

Huyu angewagharimu fedha nyingi, kwani ofa yao ya pauni milioni 20 ilikataliwa na Saints waliodai ilikuwa kama utani. Hata hivyo, kwa umri wake angeweza kuwafaa zaidi ya Schweinsteiger anayeelekea ukingoni.

Sakata la mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling, 24, limeingia hatua mpya kwani licha ya kuwasili kwenye mazoezi inadhaniwa kwamba atatupwa kikosi cha akiba.

Wamiliki wa Liverpool wanaona kwamba afadhali wabaki naye licha ya kwamba anataka kuondoka kwa nguvu, kuliko kumuuza kwa bei ndogo.
Manchester City wanataka kumsajili lakini inaelekea kiwango wanachotaka Liverpool ni pauni milioni 50 ambazo bado City hawajatoa ofa kubwa kiasi hicho.

Kwa siku mbili mfululizo Sterling hakuingia mazoezini na badala yake alipiga simu asubuhi kueleza kwamba alikuwa anaumwa.

Hajajulikana iwapo atasafiri na timu kwa ajili ya ziara ya kabla ya kuanza msimu Australia na Asia, safari itakayoanza Jumapili hii.
Katika hatua nyingine, Chama cha Wanasoka wa Kulipwa (PFA) kimesema kipo tayari kuwapatanisha Sterling na Liverpool.

Sterling alidai kwamba kuna kutoelewana kati yake na kocha Brendan Rodgers na hivyo hataki tena kuchezea klabu hiyo. Hata hivyo anafungwa na mkataba kwani bado ni mchezaji halali Anfield.

Golikipa wa Arsenal, David Ospina yupo tayari kwenda kuchezea Everton, baada ya nafasi ya kucheza klabu kwake kuonekana kuwa na ushindani mkubwa.

Kusajiliwa kwa Petr Cech kunamweka katika uwezekano wa kutocheza mechi nyingi, kwani moja ya masharti ya kukubali kusajiliwa Arsenal kwa Cech ni kupata fursa zaidi kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuzikosa Chelsea alikokuwa.

Ospina amesema Everton ni timu yenye ushindani mkubwa na kwamba kwenda huko kunawezekana kwa kiasi kikubwa.

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kusikitishwa na klabu hiyo kuonesha kutokuwa na nia ya kumpatia fedha kwa ajili ya usajili.

Mourinho ameitaka bodi ya klabu hiyo kufanya haraka kuamua ili
wampatie raslimali anazohitaji kabla msimu wa usajili haujamalizika au wachezaji anaowataka kuchukuliwa na klabu nyingine.

Tottenham Hotspur wamekataa ofa ya pauni milioni 3.6 kutoka klabu ya Uturuki ya Galatasaray inayotaka kumsajili beki wa kimataifa wa Romania, Vlad Chiriches, 25.

Newcastle wanaelekea kukamilisha usajili wa Georginio Wijnaldum, 24, kutoka PSV Eindhoven kwa pauni milioni 13.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

SIKU YA PSPF YAFANA SABASABA

Serena Williams hana mpinzani