Msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara unaanza rasmi Septemba 6 viwanja mbalimbali vitawaka moto huku timu nyingi zikiwa na matumaini ya kupata mafanikio kutokana na usajili uliofanyika.
Msimu uliopita mfungaji bora alichukua Meddie Kagere kutoka timu ya Simba ambaye alifunga magoli 23.
Kitendawili kikubwa msimu huu nani ataibuka mfungaji bora na kwa magoli mangapi.
Tumeonaa baadhi ya mechi za kirafiki timu zikiwa zinatesti mitambo je ni kweli zitafanya maajabu.
Wachezaji wanaowania ufungaji bora ni wengi hapa tunawataja wachache ambao kila mmoja anaweza kuhisi kwa upande wake.
Japo vita abado itabaki mitaa ya kariakoo Kagere wa Simba na Michael Sarpong ingizo jipya la Yanga.
Yusuph Mhilu- Kagera Sugar
Ni nyota mzawa raia wa Tanzania, alifunga magoli 13 msimu uliopita na aliongoza kwa ufungaji bora kwa wachezaji wa ndani kilichonifanya nimpendekeze tena heshima yake katika kulinda kiwango chake huku akiwa na jitihada za hali ya juu.
Mhilu alitoka Yanga na ilisemekana msimu huu ulioisha baada ya Korona Yanga walipiga hodi tena kuhitaji huduma yake.
Lakini vipengele vyake vikawa vigumu kimoja wapo mdogo wake naye asainiwe huko anapoenda.
Obrey Chirwa- Azam FC
Wengi wanaweza kumpuuzia nyota huyu msimu uliopita alifunga magoli zaidi ya kumi alifanya vizuri kwa nafasi yake.
Uwezo wake wa kupambana pamoja na kasi itaweza kumrudisha kuwa katika kinyang’anyiro hiko cha ufungaji bora.
Chirwa aliwahi kucheza Yanga kwa mafanikio aliwahi kufunga magoli 24 katika kipindi chote alichochezea timu hiyo huku akiwa tegemezi.
Huduma yake hivi sasa iko Azam FC ongezeko la wachezaji ndani ya timu hiyo linaweza kumpa nafasi ya kufanya vizuri zaidi.
Waziri Junior- Yanga
Msimu uliopita alifunga magoli 13 akiwa na timu ya Mbao FC alifanya vizuri sana tatizo hakukuwa na wapishi wazuri hivyo kuungana na jopo la wachezaji walio na uwezo mkubwa linaweza likamuongezea nafasi ya kufunga kama atapata nafasi.
Meddie Kagere- Simba
Inawezekana akaweka historia ya kuwa mfungaji bora mara tatu mfululizo msimu huu tunaoanza nao kama akipata nafasi.
Tukumbuke kuwa alifungaa magoli 23 msimu uliopita na huu pia alifunga magoli 22 uwezo wake kila mmoja anafahamu.
Imani yangu ni kwamba kama atapata nafasi ataweza kufanya kile alichokifanya misimu miwili ya nyuma.
Kagere ni mchezaji hodari sana licha ya wengi kumsema kuwa na umri mkubwa lakini anachokifanya uwanjani kinaweza kutafasiriwa kwa namna nyingine.
Uhodari wake wa kujiweka katika nafasi na kujua muda gani mpira unafika kwake ndio sababu ya kuona kuwa anaweza kupambana na kuwa mfungaji bora tena.
Kikubwa kwake apate nafasi nzuri ya kuchezo hilo litakuwa halina ubishi kabisa.
John Bocco- Simba
Ni kiongozi kwa maana aaya kapteni wa Simba hajawahi kushuka kiwango kwa miaka 13 sasa tangu tumfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2008.
Ni mchezaji wa daraja la juu kwa wazawa, pia mfungaji bora wa muda wote ligi kuu Tanzania Bara kwa rekodi zilizopo hivi sasa.
Uzuri wake kocha wa Simba Sven anamuamini na kuona kuwa ndio chaguo sahihi hivyo kama atapata nafasi anaweza kuipita rekodi yake aliyoiweka msimu wa 2013 alipofunga magoli 19.
Michael Sarpong- Yanga
Sarpong ni ingizo jipya Yanga la bado shabiki wa Yanga hawajaona uwezo wake halisi lakini rekodi ndio hasa zimenifanya nimuorodheshe katika kundi hili hii kuwa anaweza kupambana na kuwa mfungaji bora.
Hii inatokana na mafundi ambao wako Yanga msimu huu hivyo naye tunamuingiza humu.
Sarpong alifunga magoli 16 katika msimu wa 2018-19 akiwa na timu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda kwa uwezo wake na nguvu anaweza kuwa mtetezi wa Yanga msimu huu.
Ikumbukwe kuwa baada ya timu ya Wanacnhi kuondoka kwa Heritier Makambo hakuna mshambuliaji aliyekuwa anatisha zaidi hadi sasa.
Msimu uliopita mfungaji bora alikuwa David Molinga ambaye alifunga magoli 12 lakini alicheza mechi chache zaidi.
Hivyo Sarpong na Yacouba Sogne wanakazi kubwa ya kuwafanya wana Yanga kusahau kilio cha upachikaji wa mabao msimu huu unaoanza Jumapili.
Benard Morrison – Simba
Amejiunga na Yanga katika dirishadogo la usajili na lilikuwa pendekezo la kocha Luc Eymael baada ya hapo kilichofuata ni historia kwani ameibukia upande wa pili wa Simba.
Uwezo wake mzuri wa kukimbia na mpira kutoa pasi pamoja na kufunga huku naye anajua harufu ya mpira katika kujiweka katika nafasi ya kufunga.
Msimu huu atasumbua sana hasa akiacha ukaidi wake ni mchezaji mzuri sana na anaweza kufunga zaidi ya magoli 15.
Waachezaji wengine ambao wanaweza kutazamiwa kuwa wafungaji bora ni pamoja na Tuisila Kisinda kutoka Yanga huyu kasi yake na uwezo wake wa kufunga pia tunaweza kumjumuisha humu.
Chris Mugalu naye nyota anayechezea Simba anaweza kufanya makubwa kutokana na kutumia vizuri nafasi anapokuwa golini.
Wengine ni Tariq Seif, Marcel Kaheza wanacheza Polisi Tanzania na Charles Ilamfia kutoka timu ya Simba.
Rekodi inayosubiriwa kwa hamu ile ya kufunga magoli 25 aliyoifanya Mohamed Hussein mwaka 1999.
Nani atafunga zaidi ya magoli hayo kwa maana ya 26 awe mfungaji bora wa muda wote kwa msimu mmoja.
Tufahamu kuwa kuna mfungaji bora wa muda wote kwa msimu yote ambaye ni John Bocco lakini pia kunamfungaji bora wa muda wote kwa msimu mmoja ambaye ni Mohamed Hussein alifunga akiwa Yanga msimu wa 1999.
Comments
Loading…