in , ,

Sanchez anaenda Milan

*Ibrahimovic azungumzia kurudi Ma United

Wakati Manchester United wakikubali kumtoa mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez, kwenda Inter Milan Italia, mshambuliaji wao wa zamani, Zilatan Ibrahimovic amezungumzia kurudi Old Trafford.

United walioanza msimu kwa hali mchanganyiko, wakichechemea kiasi chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, wamekubali kumwachia nyota huyo kwa Inter wa Italia kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Sanchez alijiunga Man U akiwa moto Januari 2018 kutoka Arsenal wakibadilishana na Henrikh Mkhitaryan, wakati huo Man U wakiwa chini ya kocha Jose Mourinho lakini haukupita muda akaanza kugeuka garasa.

Bosi wa Inter, Antonio Conte amekuwa akitaka sana kumsajili mchezaji huyo kabla ya dirisha la usajli la Ulaya kufungwa Jumatatu. Ikiwa hatua zote zitakamilika na Sanchez kwenda huko, ina maana atakutana na mchezaji mwenzake wa zamani Man U, Romelu Lukaku aliyesajiliwa kwa pauni milioni 74 akivunja rekodi ya klabu hiyo.

Conte alikuwa bosi wa Chelsea na uhamaji na kukutana tena katika nchi au klabu kwa wachezaji na makocha ni dhihirisho kwamba maisha yanabadilika sana. Inter hawajakubali dili la kumnunua mchezaji huyo mwishoni mwa mkataba wa mkopo mwakani.

Sanchez ndiye mchezaji wa Man U anayelipwa bei ghali zaidi, ambapo kwa wiki anapata £400,000, kiwango ambacho hakipo kwenye mfumo wa malipo wa Inter. Imeshauriwa kwamba Man United wachangie kwenye mshahara wa mchezaji huyo ambapo Inter walisema wanaweza kulipa £150,000 lakini United wakataka zaidi.

Sanchez amekuwa na miezi 19 ya tabu Old Trafford, ambapo katika mechi 45 amefunga mabao matano tu. Msimu uliopita alifunga mabao mawili tu kwenye mechi za Ligi Kuu ya England (EPL). Solskjaer anapanga kumtumia zaidi tineja Mason Greenwood, ambaye ameshacheza mara kadhaa na wakubwa.

Ibrahimovic kwa upande wake, amesema mkataba wake ukimalizika nchini Marekani anaweza kurudi Manchester United. Jamaa huyu mwenye umri wa miaka 37 bado yupo timamu kimwili na amefunga mabao 46 katika mechi 49 za Major League akiwa na klabu ya Soccer tangu Machi mwaka jana.

“Naweza kucheza vizuri sana kwenye Ligi Kuu, kwa hiyo ikiwa United wananitaka nipo tayari,” akasema mchezaji aliyefunga mabao 28 katika msimu wa 2016/17 akiwa na United kabla ya kupata majeraha makubwa ya goti na kuwa mwisho wake kuchezea Man U kabla ya mkataba wake wa miaka miwili kukamilika.

“Nilifanya kazi yangu Ulaya. Niliifurahia, nina makombe 33 niliyokuja nayo hapa na natumaini naweza kutoa kitu hapa. Baada ya hapa tutaona wapi pa kwenda kumalizia,” akasema na kuongeza kwamba bado hutazama mechi za Man United na anafikiri katika mechi ya mwisho hawakuwa na bahati.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Sanchez: Mshahara pasua kichwa

Tanzania Sports

Ni Vigil van Dijk