in , , ,

Rushwa ya FIFA inatisha

Alfredo Hawit, Raisi wa Concacaf, 9kushoto), na Juan Ángel Napout, Raisi wa Conmebol, walitiwa mbaroni jijini Zurich, siku ya Alhamis.

 

*Kigogo wake alilipwa pauni mil. 6.6

*Makamu wenyeviti wasimamishwa

SHIRIKA la Ujasusi la Marekani (FBI) limeng’amua kwamba kigogo mmoja wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) alikula mlungula wa pauni milioni 6.6.

FBI inamrejea ofisa huyo kama ‘co-conspirator 17’, na inaelezwa kwamba alikabidhiwa kitita hicho baada ya kuratibu kwa mafanikio mpango wa kuhakikisha kura zinatosha ili Afrika Kusini wawe wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 2010.

Kigogo huyo ni mmoja wa waliokwishafunguliwa jalada nchini Marekani, na ni kati ya wale ambao Wizara ya Sheria ya Marekani ilitoa maelezo juu ya jinsi mchwa walivyokuwa, kwa miongo kadhaa, wakitafuna bila huruma fedha za umma.

Yumo katika kundi linalowajumuisha pia makamu wenyeviti wawili wa FIFA, Alfredo Hawit na Juan Angel Napout waliokamatwa Alhamisi wiki hii jijini Zurich walikokuwa kwa ajili ya vikao vya uongozi wa juu wa FIFA.

Walidakwa na mamlaka za Uswisi, lakini kwa maombi ya mamlaka za Marekani, ambapo katika ujumla wake, uchunguzi unaendeshwa na nchi mbili hizo juu ya jinsi mlungula ulivyotembea kwa wajumbe ili kupitisha nchi kadhaa kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia, lakini pia katika kuuza haki za matangazo ya mashindano mbalimbali.

Inaelezwa kwamba kiwango hicho cha fedha kililipwa, pamoja na mambo mengine, kama ‘uwezeshaji’ kwa wapiga kura wa FIFA, makamu mwenyekiti wa zamani, Jack Warner na msaidizi wake, Chuck Blazer, huyu wa mwisho akikiri yote hayo.

Septemba Warner alipigwa marufuku na FIFA kujishughulisha na shughuli zozote za soka kutokana na mwenendo wake, Kamati ya Maadili ya FIFA ikisema kwamba alikosa uaminifu katika matukio yaliyokuwa yakiendelea na kujirudia rudia.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Nidhamu ya FIFA imechukua hatua za kuwasimamisha makamu wake wawili – Hawit na Napout kwa siku 90, wakitakiwa kutojishughulisha na mambo yoyote ya soka. Huko nje wanaungana huko nje na Rais wa FIFA, Sepp Blatter na Makamu wa Rais wa FIFA.

Almahisi kulikuwa na kikao cha FIFA kwa ajili ya kujadili masuala ya mageuzi ya shirikisho hilo na upigaji kura. Blatter mwenyewe alisimamishwa akiwa katika kile alichodai kupanga mageuzi na matarajio yake yalikuwa kuachia ngazi Februari mwakani, baada ya uchaguzi wa kupata mrithi wake.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Loretta Lynch amezungumzia hatua zinazoendelea katika uchunguzi na jinsi matukio ya ufisadi yanavyochefua.

“Usaliti huu unaofanywa na watu walioaminiwa ni aibu kubwa. kiwango cha rushwa kinachotuhumiwa hapa hakimithiliki. Na huu (hatua ya kuwakamata na kufungua mashitaka) ni ujumbe wa wazi kwa kila mmoja anayehusika ambaye bado hajatiwa nguvuni akitumaini kukwepa upelelezi wetu:hamtaweza kutusubirisha; hamuwezi kukwepa mwelekeo wetu.”

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

PSPF wapeleka huduma mpya ya Bima ya Afya Majira, Mwananchi

Tanzania Sports

Chelsea, Man City chali