in , ,

ROSS BARKLEY ATACHEZAJE KWENYE MFUMO WA CHELSEA?

Chelsea katika dirisha hili dogo la usajili wamefanikiwa kumchukua
kiungo Ross Barkely kutoka katika timu ya Everton.

Wana idadi kubwa ya viungo wa kati kama Kante, Bakayoko, Fabregas,
Danny Drink-Water.

Viungo wote hawa kuna kitu Chelsea wanakosa katika eneo hili la kiungo ?

Hebu tujaribu kuwatazama viungo waliopo kwa sasa.

Kante : Kazi kubwa ya Kante ni kuilinda safu ya ulinzi ya Chelsea na
kuanzisha mashambulizi.

Kazi hii Kante amekuwa akiifanya kwa kiwango kikubwa sana.

Fabregas: Kazi kubwa ni kutengeneza nafasi za magoli kutokea katikati
ya uwanja, hana kasi ya kukimbia kutoka katikati kwenda mbele ila ana
uwezo wa kupiga pasi ndefu na za mwisho akitokea katikati ya uwanja.

Kazi hii anayoifanya Fabregas haipishani na kazi ambayo imemleta Danny
Drink-Water na ndiyo maana aliletwa kwa madhumini ya yeye kuja kuwa
mbadala wa Fabregas.

Kante na Fabregas wanatimiza vizuri majukumu yao, ila kinachokosekana
ni kiungo ambaye anakimbia kuanzia nyuma mpaka mbele ( kiungo
atakayesaidia eneo la ulinzi na eneo la ushambuliaji).

Bakayoko ndiye ambaye ameletwa kwa ajili ya kufanya hiyo kazi lakini
anakosa kitu kimoja, nacho ni ubunifu wa kutengeneza nafasi za kufunga
na uwezo wa kufunga.

Hiki ndicho kinachokosekana na hapa ndipo mahali ambapo Ross Barkely
atakapokuwa na msaada mkubwa.

Je anawezaje kucheza katika mifumo ya Conte?

Conte amekuwa akitumia 3-4-3 na 3-5-2.

Nyuma akiwa na mabeki watatu ambao ni Cahil, Azplicueata na Andreas Christensen.

Ili kumfanya Ross Barkely aingie katikati basi itamlazimu acheze na
Kante, Fabregas/Drink-Water na yeye. Huku kwenye wingback ya kushoto
akicheza Marcus Alonso na Wingback ya kulia akicheza Victor Mosess.

Na mbele wanacheza Hazard, Morata na Pedro

Hapa ni kwenye mfumo wa 3-5-2

Kwenye mfumo 3-4-3 pia, Ross Barkely anaweza akacheza pembeni eneo la
Willian/Pedro.

Hivo mabeki wanabaki wale wale watatu ( Cahill, Azplicueta na Christensen).

Eneo la katikati wakacheza Kante, Fabregas/Drink-Water. Huku wingsback
ya kushoto akacheza Marcus Alonso na Wingback ya kushulia akacheza
Victor Mosess.

Na mbele akacheza Hazard ,Morata na Yeye mwenyewe Ross Barkely.

Pia na kwenye huu mfumo wa 3-4-3 pia Ross Barkely anaweza akawa
anatokea katikati.

Yani mabeki wanabaki walewale watatu niliowataja hapo juu, viungo wa
kati anakaa Kante na Ross Barkely. Mbele waweza kutumia njia mbili ,
njia ya kwanza ni ya kumfanya Fabregas acheze, hivi unampeleka nyuma
ya mshambuliaji wa mwisho na umbo linakuwa 3-4-1-2 huku Hazard
akicheza kama mshambuliaji huru na Morata kubaki kama mshambuliaji wa
mwisho. Huku wingbacks wakibaki wale wale Alonso na Mosess upande wa
kushoto na kulia.

Umbo la pili ni umbo ambalo litamuondoa Fabregas na kuwaweka Willian
au Pedro kule mbele (3-4-3). Mabeki wanabaki wale wale watatu.
Wingback wanabaki wale wale. Katikati anabaki Kante na Ross Barkely ,
mbele ndiyo wanakuwa Hazard , Morata na Pedro/Willian.

Upi ni ubora wa Ross Barkely?

Kukaa na mpira, hii inaweza ikaonekana kama hasara ila ni faida sana.

Mchezaji anapokaa na mpira husaidia wachezaji wenzake watafute sehemu
zenye uwazi ili wawe huru kupokea mpira.

Uwezo wa Barkely kukaa na mpira kutakuwa na msaada mkubwa kwa
wachezaji wa Chelsea kuwa na nafasi ya kutafuta sehemu zilizo wazi ili
wapokee mipira.

Kuunganisha na kuanzisha mashambulizi ni faida nyingine ya Ross Barkely.

Huwa anatabia ya kushuka chini kuchukua mpira nyuma na kusaidia
kuunganisha timu kwa kuanzisha mashambulizi.

Mtu wa aina hii alikuwa anakosekana Chelsea ndiyo maana kuna kipindi
Hazard huwa anashuka kuchukua mipira chini, uwepo wa Ross Barkely
kutamfanya Hazard asiwe anashuka mara kwa mara chini.

Ross Barkely pia anauwezo wa kutengeneza nafasi kwa ubunifu mkubwa.
Bakayoko amekuwa siyo mtu mbunifu kwenye kutengeneza nafasi.

Kuna kitu ambacho kinambeba sana Ross Barkely, nacho ni uwezo wake wa
kufunga ndani na nje ya box .

Anauwezo wa kufunga kwa mashuti akiwa nje ya box,na hiki kinambeba sana.

Kwa hiyo, baada ya Bakayoko kukosa ubunifu mkubwa katika eneo la
mwisho , Ross Barkely atakuja kuongeza ubunifu ambao ulikuwa
unakosekana wakati wa Bakayoko

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

ALEXIS SANCHEZ MAFANIKIO HAYAKUFUATI, YANATAFUTWA

Tanzania Sports

TUMSAIDIENI KUJIBU SANCHEZ, AENDE KWA PEP AU MOURINHO ?