in , , , ,

Ronaldo, Ribery na Messi wawania tuzo


*Arenal na Spurs Kombe la FA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetaja majina ya wachezaji watatu watakaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia.
Wachezaji hao ni Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ya Hispania, Frank Ribery wa Bayern Munich ya Ujerumani na Lionel Messi wa Barcelona ya Hispania.

Majina hayo yametokea wakati pakiwa na maoni tofauti juu ya mchezaji anayeweza kunyakua tuzo hiyo, kutokana na Messi aliyeitwaa mara kadhaa kutokuwa fiti kwa muda mrefu.

Hadi sasa Messi alikuwa nyumbani kwao Argentina akijiuguza na kujipanga kurejea upya dimbani, lakini tayari ameelezwa kuanza mazoezi mepesi. Ronaldo naye alipata majeraha hivi karibuni lakini amesema yupo fiti.

Ribery alitokea kutajwa kwamba ana uwezekano wa kutwaa tuzo hiyo badala ya wawili hao wanaochezea timu hasimu za Hispania, lakini Ronaldo muda wote amekuwa akiamini kwamba yeye ndiye.

Rais wa Fifa, Sepp Blatter amepata kutoa kauli ya utani kumhusu Ronaldo kwamba anapenda zaidi kuvaa vizuri na kujiweka kimitindo kuliko anavyocheza na Mreno huyo alitishia kususia tuzo za mwaka huu.

Rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa), Michel Platini amesema hivi karibuni kwamba tuzo ya mwaka huu ni ngumu zaidi katika historia.
Makocha walioteuliwa kuwania tuzo ya kocha bora ni Jupp Heynckes aliyestaafu Bayern Munich kumpisha Pep Guardiola na ndiye aliipa klabu hiyo makombe ya ndani pamoja na ubingwa wa Ulaya msimu uliopita.

Makocha wengine ni Alex Ferguson aliyestaafu Manchester United baad aya kuwapa mafanikio na mataji mengi katika ukocha wake wa miaka 26.

Mwingine ni Jurgen Klopp aliyewaongoza Borussia Dortmund msimu uliopita hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia amewafikisha pazuri msimu huu.

ARSENAL NA SPURS KOMBE LA FA

Droo ya raundi ya tatu ya Mashindano ya Kombe la FA imetoka, ambapo Arsenal na Tottenham Hotspur wamepangwa kuumana katika Uwanja wa Emirates.

Mechi za raundi hiyo zitafanyika katika wiki ya kwanza ya Januari mwakani ambapo Manchester United watacheza na Swansea City katika dimba la Old Trafford.

Norwich watakwaana na Fulham wakati Chelsea watasafiri kwenda kuchuana na timu ya daraja la pili ya Derby County huku Manchester City wakiwa wageni wa Blackburn Rovers.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo, Wigan watakuwa wenyeji wa timu ya Milton Keynes (MK) Dons wakati timu zisizokuwa katika ligi rasmi za Kidderminster na Macclesfield zitaumana na Peterborough na Sheffield Wednesday katika mtiririko huo.

West Bromwich Albion wamepangwa kucheza na Crystal Palace, Cardiff watakuwa na Newcastle wakati Liverpool watakuwa nyumbani wakicheza na timu ndogo za ama Oldham au Mansfield zinazotoka League One na League Two.

Mara ya mwisho kwa Arsenal na Spurs kukutana kwenye Kombe la FA ilikuwa katika nusu fainali ya 2001, ambapo Robert Pires alifunga bao la ushindi pale Washika Bunduki walipowapiga wenzao wa London Kaskazini kwa 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Droo hii ilifanywa na mpachika mabao wa zamani wa England, Teddy Sheringham na mwanawe anayechezea AFC Wimbledon kama mshambuliaji, Charlie.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Matatani kwa kupanga matokeo England

Manchester United yasababisha kifo Kenya