in , ,

Ronaldo ampa wakala kisiwa

 

Mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo amempa wakala wake, Jorge Mendez zawadi ya kisiwa.

 

Ronaldo ambaye ni milionea na mchezaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, amempa Mendez kisiwa kilichoko Ugiriki kama zawadi katika siku yake ya harusi.

 

Kisiwa hicho bado hakijatajwa, lakini inaelekea kwamba kitakuwa kimenunuliwa kwa mamilioni ya pauni na kwamba Ronaldo anakifahamu vyema kisiwa hicho kwani alikuwa akienda huko kwa starehe wakati wa likizo.

 

Mendes alifunga ndoa na Sandra Barbosa Jumapili hii nchini mwake Ureno, ambapo kati ya wageni waliohudhuria harusi ni aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.

 

Kocha huyo mkongwe ndiye alimsajili Ronaldo Old Trafford 2003 alikokaa hadi 2009 akamuuza Real Madrid. Ameshinda tuzo ya mchezaji bora duniani mara tatu.

 

Ronaldo ndiye alikuwa msimamizi katika harusi hiyo ya Mendes, 49, ambaye ni mmoja wa mawakala waliofanikiwa zaidi katika soka. anaendesha biashara iitwayo Gestifute kwa minajili ya kuendeleza vipaji vya soka.

 

Kuna visiwa kadhaa nchini Ugiriki ambavyo vinauzwa na katika tovuti inaonekana kwamba kisiwa kimoja kinaweza kugharimu euro kuanzia milioni tatu.

 

Sherehe za harusi hiyo zilifanyika kwenye eneo la makazi jijini. Mendez na Sandra wana watoto watatu; wameishi pamoja tangu 2005.

 

Baadhi ya wanasoka kutoka Hispania na Ureno walihudhuria, akiwamo pia Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, Rais wa Benfica, Luis Filipe Vieira na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.

 

Kwa mujibu wa tovuti ya Hispania, ABC, Mendes ni mmoja wa matajiri wakubwa zaidi nchini Ureno, akimiliki euro milioni 100 hivi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

PAZIA LA MSIMU ENGLAND:

English Premier League 2015-2016 Kuanza