in

Robin van Persie kwenda Fenerbahce


*Raheem Sterling sasa agomea mazoezi

Mshambuliaji wa kati wa Manchester United, Robin van Persie anatarajia kujiunga na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce baada ya klabu mbili hizo kukubaliana juu ya ada ya uhamisho ya pauni milioni 4.7.

Mdachi huyu analazimika kuondoka kwa sababu hana uhakika wa namba msimu ujao baada ya bosi Louis van Gaal kumwambia itategemea atakavyoongeza kiwango chake. Zipo habari kwamba Van Persie (31) alitarajia kufanyiwa vipimo vya afya jijini London Alhamisi hii.

Mkataba wake unamalizika mwaka ujao na United hawana nia ya kumwongezea mkataba ma pia hawangependa kuona akiondoka kama mchezaji huru na wao wakikosa hata senti tano wakati walimnunua kwa pauni milioni 24 miaka mitatu iliyopita.

Habari ni kwamba Mholanzi huyu atasaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo na atajiunga na winga aliyekuwa naye Manchester United miaka miwili ya mwanzo, Nani, aliyekamilisha usajli akitokea Sporting Lisbon kwa mkopo na hakutakiwa tena United kwa sababu ya kiwango kidogo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita tetesi za Van Persie kuuzwa zilizagaa lakini United walidai hapakuwa na kitu kama hicho, huku taarifa nyingine zikisema kwamba tangu Januari United walikuwa wakiwasiliana na klabu mbalimbali ili kumwondosha RVP Old Trafford.

Raheem Sterling amekataa kufanya mazoezi na Liverpool
Raheem Sterling amekataa kufanya mazoezi na Liverpool

Katika tukio jingine, Raheem Sterling amekataa kufanya mazoezi na klabu yake, akisema kutokuaminiana baina yake na kocha Brendan Rodgers kumemfanya asitake tena kucheza Anfield.

Hata hivyo, alipiga simu klabuni na kusema kwamba alikuwa ‘mgonjwa sana’ kiasi kwamba hawezi kufanya mazoezi na wenzake. Alipokutana na Rodgers akitoka likizo,alimwambia kwamba hataenda na wenzake ziarani Australia na Asia kwa maelezo kwamba hayuko sawa kisaikolojia.

Jana Jumatano asubuhi alipiga simu akisema alikuwa anaumwa na leo pia amepiga simu akisema kwamba hataweza kufanya mazoezi ya kabla ya msimu, lakini hiyo inaelekea ni mbinu ya kulazimisha aondoke.

Anatakiwa na Manchester City ambao inaelezwa wapo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 50 baada ya kima cha chini ya hapo kukataliwa na Liverpool wanaosema mchezaji huyo hauzwi. Sterling, 24, amekataa kusaini mkataba mpya Anfield, ambapo angekuwa akilipwa pauni 100,000 kwa wiki.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Chelsea kuhamia Wembley

MZOZO WA MLUNGULA FIFA