Yanga na Simba zilianzishwa mwaka 1935 na 1936 baada ya kutokea mvurugano baina ya viongozi wa pande hizo mbili.
Yanga ndio timu kongwe zaidi Tanzania ilianza 1935 wakati Simba ikitokea ubavuni mwa Yanga baada ya mvurugano huo na kuunda timu nyingine inayoitwa Sunderland.
Lengo sio kutaja historia bali kuwakumbusha ubingwa wa Tanzania bara timu gani zimechukua tangu itambulike na kuitwa ligi kuu Tanzania Bara.
Ligi kuu Tanzania Bara rasmi ilianzishwa mwaka 1965 baada ya miaka minne ya Uhuru wa Tanzania ndipo ligi hiyo ilianzishwa.
Yanga na Simba ndizo zilizo chukua ubingwa mara nyingi zaidi kuliko nyingene zote hapa Tanzania Bara.
Ikiwa timu zote mbili zimechukua mara 48 wakati mara 6 pekee ndio zimechukua timu nyingine.
Timu nyingine zilizochukua katika miaka 54 ya ligi kuu Bara ni pamoja na Coastal Union, Tukuyu Stars, Azam FC na Mtibwa Sugar ambayo imechukua mara mbili.
Timu za Simba na Yanga ndizo timu zilizochukua ubingwa mara nyingi kuliko timu nyingine nchini tangu mwaka 1965 mpaka 2020 kama nilivyotangulia kusema huko juu.
Yanga ndiyo iliyochukua mara nyingi zaidi ubingwa huo ikifuatiwa kwa karibu na Simba ambayo zamani ilijulikana kama Sunderland Sports Club.
Yanga imechukua mara 27 Simba mara 21 mchuano ni mkali kweli kweli.
Msimu huu wa mwaka 2017/18 mbio zinaonekana kuwa mikononi mwa timu mbili za Simba na Yanga ambapo Simba walionekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuuchukua ubingwa wa msimu huo na kweli ilichukua.
Mwaka huu bado mambo magumu sana haijulikani timu ipi itavuna na ipi itaambulia mabua, Yanga , Simba na Azam FC ndizo zinazonekana kuwa karibu na taji hilo msimu huu.
Hapa chini tumekuwekea orodha kamili ya historia ya ubingwa huo tangu mwaka 1965:
Hapa sasa utagundua hii ya kuchukua mara nyingi kumbe ilianza muda mrefu na huwa Yanga na Simba wanalipana timu hiz ziliwahi kuchukua ubingwa mara tano mfululizo na nyingine mwaka uliofuata ikachukua mara hizo hizo.
Tuanze na msimu wa mwaka 1965 Sunderland (Simba SC), 1966 Sunderland, 1967 Cosmopolitan.
Baada ya hapo Yanga iliichukua mara tano mfululizo yaani 1968 Young Africans , 1969 Young Africans, 1970 Young Africans , 1971 Young Africans , 1972 Young Africans, 1973 Simba SC, 1974 Young Africans, 1975 Mseto SC.
Simba ililipa kuchukua mara tano mfululizo 1976 Simba SC, 1977 Simba SC, 1978 Simba SC, 1979 Simba SC, 1980 Simba SC, 1981 Young Africans, 1982 Pan Africans, 1983 Young Africans, 1984 Simba SC, 1985 Young Africans, 1986 Tukuyu Stars, 1987 Young Africans, 1988 Coastal Union, 1989 Young Africans, 1990 Simba SC, 1991 Young Africans, 1992 Young Africans, 1993 Young Africans, 1994 Simba SC, 1995 Simba SC, 1996 Young Africans , 1997 Young Africans na 1998 Young Africans .
Mtibwa imeingia katika historia kwa kuchukua ubingwa Karne ya 20 na 21 yaani 1999 Mtibwa Sugar na 2000 Mtibwa Sugar
Wakati 2001 Simba SC, 2002 Young Africans , 2003 Simba SC, 2004 Simba SC, 2005 Young Africans , 2006 Young Africans, 2007 Simba SC, 2007/08 Young Africans , 2008/09 Young Africans, 2009/2010 Simba SC, 2010/2011 Young Africans Sc, 2011/2012 Simba SC, 2012/2013 Young Africans Sc, 2013/2014 Azam FC, 2014/2015.
Yanga wamerudia tena kuchukua mara tatu mfululizo Young Africans, 2015/ 2016 Young Africans , 2016/ 2017 Young Africans .
Mapigo ya kuchukua mara tatu mfululizo yamerejea kwa Simba nao 2017/ 2018, 2018-19, 2019-20.
Swali linabaki pale pale msimu huu timu ipi itachukua ubingwa kulingana na usajili wa wachezaji bora kwa vikosi vya Simba, Yanga na Azam.
ILI UZIONE VIZURI ANGALIA HAPA
1965 Sunderland (Simba SC)
1966 Sunderland
1967 Cosmopolitan
1968 Young Africans
1969 Young Africans
1970 Young Africans
1971 Young Africans
1972 Young Africans
1973 Simba SC
1974 Young Africans
1975 Mseto SC
1976 Simba SC
1977 Simba SC
1978 Simba SC
1979 Simba SC
1980 Simba SC
1981 Young Africans
1982 Pan Africans
1983 Young Africans
1984 Simba SC
1985 Young Africans
1986 Tukuyu Stars
1987 Young Africans
1988 Coastal Union
1989 Young Africans
1990 Simba SC
1991 Young Africans
1992 Young Africans
1993 Young Africans
1994 Simba SC
1995 Simba SC
1996 Young Africans
1997 Young Africans
1998 Young Africans
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba SC
2002 Young Africans Sc
2003 Simba SC
2004 Simba SC
2005 Young Africans Sc
2006 Young Africans Sc
2007 Simba SC
2007/08 Young Africans Sc
2008/09 Young Africans Sc
2009/2010 Simba SC
2010/2011 Young Africans
2011/2012 Simba SC
2012/2013 Young Africans
2013/2014 Azam FC
2014/2015 Young Africans
2015/ 2016 Young Africans
2016/ 2017 Young Africans
2017/ 2018 Simba
2018-19 Simba
2019-20 Simba
2020-21 ???
0620406342