in

Ratiba VPL Simba, Yanga Uso kwa Uso

Yanga Simba

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ratiba ya mechi za ligi kuu Tanzania Bara itakayoanza Septemba 6 katika viwanja mbalimbali hapa nchini.

Mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Simba na Yanga utakaopigwa uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

TFF imeweka wazi kuwa mchezo huo utapigwa Octoba 18 katika Uwanja wa Taifa ambao kwa sasa unaitwa Uwanja wa Mkapa baada ya kubadilishwa jina.

Itakuwa mara ya kwanza tangu uwanja huo ubadilishwe jina na kuzikutanisha timu mbili kubwa Yanga na Simba.

Kwa mujibu wa TFF hiyo itakuwa raundi ya 7 ambapo vigogo hao watakwaana na kuoneshana umwamba.

Hii itadhihirisha namna gani vikosi vya timu hizo zimesajili na inapotokea mechi kubwa kama hizi kila kitu kina simama na watu husema mechi ya Yanga na Simba.

Katika ratiba iliyotolewa na TFF mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wataanza na Ihefu FC ambayo imepanda daraja msimu huu.

Tanzania Sports
Mzunguko wa kwanza wa VPL

Wakati wapinzani wao Yanga wataanza nyumbani kuikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.

Huku Azam FC ambayo imeshika nafasi ya tatu ita kwaana na Polisi Tanzania wakati walioshika nafasi ya nne Namungo FC watacheza dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Majaliwa .

Ratiba ya mechi za mzunguko wa kwanza ni kama ifuatavyo Mechi za kwanza za Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21

Septemba 6

Namungo vs Coastal – Uwanja wa Majaliwa, Lindi,  Biashara vs Gwambina – Uwanja wa Karume, Mara, Ihefu Vs Simba – Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Mtibwa vs Ruvu Shooting – Uwanja wa Gairo, Morogoro, Yanga Vs Prisons – Uwanja wa Mkapa, Dar, KMC vs Mbeya City – Uwanja wa Uhuru, Dar, Azam Vs Polisi Tanzania – Azam Complex.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mwakinyo

Tinampay Amembadilisha Mwakinyo

PSG

Neymar, Mbappe na Di Maria ni MSN ndani ya PSG