Mchakato wa ratiba ya Ligi Kuu ya England (EPL) umekamilika na kuwekwa hadharani, ambapo Manchester City wataanza kutetea ubingwa wao ugenini kwa Newcastle Agosti 16.
Msimu wa 2014/15 unaanza kilaini kwa Manchester United ya Louis van Gaal tofauti na ilivyokuwa kwa David Moyes aliyekabiliana na timu kubwa za Chelsea, Liverpool na Manchester City katika mechi tano za mwanzo.
Msimu huu mpya Man U hawatakutana na vigogo hao hadi Oktoba. Mashetani Wekundu wataanza kwa kuwakaribisha Swansea.
Kocha mpya kabisa Ronald Koeman wa Southampton ataanza kwa mtihani nyumbani kwa Liverpool.
Timu iliyopanda daraja ya Burnley itaanza kwa kuwakaribisha Chelsea huku Tottenham wakianza na bosi wao mpya, Mauricio Pochettino dhidi ya West Ham.
Klabu nyingine yenye kocha mpya, West Bromwich Albion ambaye ni Alan Irvine watasafiri kukabiliana na Sunderland ya Gus Poyet.
Mabingwa wa msimu uliopita wa Ligi Daraja la Pili, Leicester watavaana na Everton wa Roberto Martnez
Mzee Harry Redknapp atawaongoza Queen Park Rangers (QPR) nyumbani Loftus Road watakapowakaribisha Hull.
Arsenal walimaliza ukame wa kombe wa miaka tisa wataanza kampeni yao dhidi ya Crystal Palace katika dimba la Emirates.
Ndani ya raundi tatu za mwanzo, Man City watakabiliana na walioshika nafasi ya pili, Liverpool dimbani Etihad.
Everton watakuwa na safari mfululizo dhidi ya Arsenal na Chelsea na wapo kwenye Ligi ya Europa pia.
EPL itachezwa hata mwaka mpya, siku mbili tu kabla ya raundi ya tatu ya Kombe la FA litakaloshirikisha timu zake. Timu za ligi ya chini hazitacheza mwaka mpya.
Timu tatu zilizoshika nafasi za juu msimu uliopita, yaani Man City, Chelsea na Arsenal watamalizia nyumbani mechi zao Mei 24 mwakani huku Liverpool wakiwa na safari ya kukabiliana na Stoke.
RATIBA KAMILI YA RAUNDI YA KWANZA:
Arsenal v Crystal Palace
Burnley v Chelsea
Leicester City v Everton
Liverpool v Southampton
Manchester United v Swansea City
Newcastle United v Manchester City
Queens Park Rangers v Hull City
Stoke City v Aston Villa
West Bromwich Albion v Sunderland
West Ham United v Tottenham Hotspur
Comments
Loading…