in , ,

Ranieri: Ubingwa Leicester bado

*Spurs wawapiga mweleka Man United
*LVG akataa majuto kutojiunga Sprus
*Liverpool wavuna karamu kwa Stoke

Wakati ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL) ukinukia kwa klabu
iliyochukuliwa kuwa ndogo ya Leicester, kocha Claudio Ranieri amesema
washabiki wanaweza kuuota lakini kamwe siw achezaji.

Mtaliano huyo ametoa kauli hiyo akitaka wachezaji kukaza buti hadi
mechi itakayowapa ubingwa badala ya kubweteka, akisema washabiki ruksa
kuota kwamba wameshaupata.

Alitoa kauli hiyo baada ya ushindi mwingine, safari hii ukiwa ni 2-0
dhidi ya timu nyepesi ya Sunderland wanaosogelea kushuka daraja.

Ranieri ‘Tinkerman’ alishangilia ushindi wa Jumapili hii unaowaacha
wakihitaji ushindi kwenye mechi tatu tu ili kujitangazia ubingwa.

“Wachezaji lazima wajielekeze kwa nguvu zote kwenye kazi hii hadi
mwisho. Unachukulia kazi hii kwa hisia zilizomo ndani lakini ni ngumu
kusema ni za aina gani. Washabiki wanaweza kuendelea na ndoto zao
kwamba sie ni mabingwa hata hivyo,” anasema Ranieri aliyepata
kuwafundisha Chelsea.

Leicester wamebaki kwenye uongozi wa ligi baada ya kufikisha pointi 72
kutokana na mechi 33, huku wakifuatiwa na Tottenham Hotspur wenye
pointi 65 kutokana na michezo kama hiyo.

Wamefika hapo baada ya kuwanyuka Manchester United 3-0 kwenye mechi ya
Jumapili hii na kuwaacha hoi Mashetani Wekundu hao katika dimba la
White Hart Lane.

Kwa hali ilivyo sasa, Leicester, maarufu kwa jina la Foxes, sasa
wamejihakikishia kumaliza ndani ya nafasi nne za juu, lakini bado
hawajajihakikishia kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao.

Kwa nini wakose nafasi ya kucheza Ulaya? Ni ikiwa Manchester City
watatwaa ubingwa wa Ulaya kisha wakamaliza chini ya nafasi nne za juu
huku Leicester wakimaliza wa nne.

Hiyo ingekuwa sawa na ilivyowatokea Spurs wakati Chelsea walipotwaa
ubingwa wa Ulaya.

Spurs waliwaduwaza Man U kwa kuwafunga mabao matatu bila majibu; mabao
yaliyotiwa kimiani na Dele Alli, Toby Alderweireld na Erik Lamela,
kuanzia dakika ya 70 hadi ya 76.

Mechi hiyo ilikawia kwa nusu saa, kutokana na timu ya Man United
kunasa kwenye foleni jijini London wakati wakielekea dimba la White
Hart Lane.

Vijana hao wa Louis van Gaal ‘LVG’ hawakuonesha tishio lolote dhidi ya
Spurs, ambapo ilichukua hadi dakika ya 62 walipoweza kumjaribu bila
mafanikio kipa Hugo Lloris.

Baada ya matokeo hayo yanayowaacha United katika nafasi ya tano na
pointi zao 53, nne nyuma ya Man City, kocha LVG alionekana
kusononeshwa na matokeo.

Hata hivyo, alisema hajutii kwa namna yoyote kukataa kwake mwito wa
kujiunga na Spurs aliopewa kiangazi cha 2014, akijipoza kwa kusema
bado Manchester United ni klabu kubwa zaidi ya Spurs.

United wako pointi 12 nyuma ya Spurs na sita nyuma ya Arsenal na
huenda wakakosa ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) msimu ujao
ikiwa timu zilizo juu hazitateleza.

“Changamoto kwangu katika Manchester United ni kubwa zaidi na itabaki
kuwa kubwa zaidi. Nawasikitikia Tottenham lakini Manchester United ni
klabu kubwa zaidi,” akasema Mdachi huyo baada ya kuulizwa swali na
mwana habari.

Licha ya United kuwa na kipindi kigumu msimu huu, Van Gaal aliyefanya
mazungumzo na Spurs juu ya kuwa kocha wao, anaamini kwamba bado United
wapo mbele ya Spurs.

“Inasikitisha kidogo kwamba umeuliza hilo. Sawa, ni rahisi kuuliza
hivyo lakini; unafurahia,” LVG mwenye umri wa miaka 64 akamwambia
mwana habari aliyemuuliza swali hilo.

Baada ya Van Gaal kusaini mkataba wa miaka mitatu hapo Old Trafford,
ndipo Spurs wakamteua bosi wa zamani wa Southampton, Mauricio
Pochettino kuwa kocha wao, na sasa ana mafanikio kedekede.

Katika mechi nyingine Jumapili hii, Liverpool walifanikiwa kupata
ushindi mkubwa wa 4-1 dhidi ya Stoke.

Divock Origi aliyeingia akitokea benchi dakika ya 45 alifunga mabao
mawili, akiongezea yale ya wenzake Alberto Moreno na Daniel Surridge.

Ushindi huo umewafanya Liverpool kuwavuka Stoke, wakibadilishana
nafasi, Liver wakipanda ya nane na Stoke wakishuka hadi ya tisa. Liver
wana nafasi zaidi kwani wamecheza mechi 31 tu wakati Stoke wamecheza
33. Stoke walisawazisha kupitia kwa Bojan Krkić.

Timu inayoshika mkia imebaki kuwa Aston Villa wenye pointi 16,
Newcastle waliokusanya 25 na Sunderland wenye 27.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Aston Villa, ni kama kwaheri tu, EPL..

Tanzania Sports

LIGI YA MABINGWA ULAYA: