in , , ,

Rafa Benitez amchana Mourinho

Maneno mengi anayotoa Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho dhidi ya wenzake yanazidi kujibiwa, safari hii Kocha wa Napoli, Rafael Benitez amemchana Mreno huyo.

Benitez amemkata ngebe Mourinho ambaye alidai kuwa Chelsea iliyumba chini ya Benitez katika kipindi cha miezi sita alichokuwa kocha wa muda. Hata hivyo, baada ya Benitez kuchukua mikoba ya Roberto di Matteo aliyefukuzwa kazi, aliwapatia Chelsea ubingwa wa Ligi ya Europa.

Benitez amemshangaa Mourinho ambaye sasa anajiita ‘The Happy One’, akisema kwamba anapenda sana kuzungumza juu ya wenzake, lakini Mhispania huyo akasema yeye anapenda zaidi kuzungumza kwa takwimu, bila kujali zinamgusa nani.

47506526_benitezferg1_pa

Mourinho amepata kumbwatukia Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akidai kwamba ni mtaalamu wa kufeli mambo, na pia dhidi ya Manuel Pellegrini wa Manchester City, lakini Pellegrini aliamua kukaa kimya, akisema anamuunga mkono Wenger.

Katika mechi iliyopita dhidi ya Chelsea, Wenger alishasema hangesalimiana na hasimu wake huyo, lakini kabla mechi haijaisha Mourinho akaondoka uwanjani, na baadaye akasema kazi dhidi ya Arsenal ilikuwa rahisi kama kupiga mswaki, ambapo walishinda 6-0.

Benitez kwa upande wake, anasema lazima Mourinho amheshimu kwa sababu zama za Liverpool waliwanyoa Chelsea na kuwaondoa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, japokuwa kikosi cha Liverpool kilikuwa na nusu tu hivi ya thamani ya kile cha Chelsea kilichokuwa chini ya Mourinho.

Wawili hao wamekuwa wakirushiana maneno tangu Liverpool walipowatoa Chelsea kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2005 kwa bao la Luis Garcia, wakati huo ikiwa ni awamu ya kwanza ya Mourinho Stamford Bridge kabla ya kurudi msimu huu akitoka Real Madrid.

Chini ya Benitez, Chelsea walimaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu, ambapo Ijumaa hii Mourinho alidai kwamba Mhispania huyo alisababisha Chelsea kuchechemea msimu wa 2012/13.

“Chelsea hawakuwa na msimu mzuri chini yake. Walikuwa na matatizo ya kufuzu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakaja kujikuta wakicheza Ligi ya Europa bila Benitez kujua madhumuni ya kikosi kile kusukwa yalikuwa yapi. Hata mwaka huu Juventus wakishinda Ligi ya Europa haitakuwa na maana yoyote kwa sababu waliundwa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,” akasema Mourinho kwa kebehi.

Benitez sasa anafundisha Napoli ya Italia baada ya muda wake kumalizika Chelsea, ambapo aliondoka akilalamika kwamba kuna mtu alikosea kwa kuandika cheo chake kuwa ni kocha wa muda, wakati makubaliano yalikuwa ni kocha.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

La Liga ya farasi watatu

Liverpool kileleni