ASIKWAMBIE mtu, iwe kiongozi, mchezaji, kocha au shabiki wa timu yoyote mafanikio makubwa yanajenga dharau. Hii ni ile dharau ambao inajitengeneza pasipo mwenye dharau kujua kama anakwenda kuangamia.
Mafanikio ya kutwaa mataji yote muhimu katika Ligi Kuu Ufaransa na kuonesha kuwa wao ni miamba ya soka Barani Ulaya kwa kutwaa Taji la Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Inter Milan, ni dhahiri yalijenga na kuwavimbisha PSG kuwa wao wanaweza kutwaa kutwaa kila taji.
Historia inaonesha kuwa PSG haikuwahi kunyakua taji la Ulaya licha ya kuwa na wachezaji wakali kama vile Ronaldinho an Jay Jay Okocha. Walicheza msimu huu wakiwa na kasi ya aina yake lakini walikuja kukwama kwa timu ya Liverpool wakiwa nyumbani jijini Paris.
Wakiwa nchini Ufaransa walikubali kipigo cha 1-0 na kumalzia dakika 90 wakiwa na hamu ya kushinda mchezo wa marudiano. Na ukweli ni kwamba katika dakika 90 za marudiano PSG waliibuka na ushindi wa 1-0 katika dakika 120 kabla ya kupata ushindi kwa matuta. Kutinga tua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa kulipwa motisha ya kiwango bora na ujuzi wa kocha huyo katika kuongoa kundi la wachezaji wenye vipaji vya hali juu.
Je, wapi PSG ilikwenda kombo?

Ili kuifunga PSG unatakiwa kuwazuia wachezaji watatu haraka; Osmane Dembele, Achraf Hakimi na Nuno Mendes. Hakimi na Mendes ni mabeki wa kulia na kushoto ambao ni wachezaji hatari katika kikosi hicho. Rekodi zinaonesha jinsi wanavyotengeneza mabao na kufunga pia.
Katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mbaingwa Hakimi alifunga boa zuri sana akiwa eneo la mshambuliaji kana kwamba yeye ndiye namba 9. PSG wanacheza vizuri pale Hakimi na Mendes wanapokuwa huru. Lakini katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la klabu kocha wa Chelsea alikuwa na mbinu rahisi mbili; kuwapanga Enzo na Coicedo wote wakiwa na jukumu la kucheza katikati ya mstari wa uwanjani kurudi nyuma wkaielekea upande wa kulia wa PSG aliko Hakimi.
Kitendo cha kumrundikia wachezaji wawili kilisababisha Achraf Hakimi akose nafasi ya kupande mbele kwani alilazimika kuwazuia akina Enzo wasitengeneze hatari. Lakini mpango wa pili ulikuwa wa aina yake, wakati eneo la Enzo na Coicedo wakiwa wanazurura kwenye dimba la kati, walitumia nafasi nyingine kupiga mipira mirefu kuelekea eneo la kushoto la PSG.
Yaani walipochukua mpira mita chache kutoka katikati ya mstari wa uwanja kushoto wao, walipiga pasi ndefu kuelekea kushoto kwa PSG ambako Nuno Mendes alikuwa aanaacha eneo kubwa likiwa wazi kwa sababu ya kutumikia mbinu ya kushambulia. Joao Pedro alikuwa mchezaji hatari katika eneo la winga wa kulia wa Chelsea kwa sababu Mendes hakuwa katika nafasi ya kulinda zaidi kwani alilenga kushambulia. Hakimi kila alivyojaribu kuvunja ukuta wa kiungo cha Chelsea alijikuta amepokonywa mpira kisha Chelsea kucheza kwa kasi kwa mashambulizi ya kushtukiza.
Nani angekuwa mchezaji bora?
Cole Palmer alifunga mabao mawili. Joao Pedro alifunga bao moja kwa kutengenezewa pasi murua na Cole Palmer. Lakini tuzo ya mchezaji bora wa mchezo ikaenda kwa Joao Pedro. Kiufundi Pedro alikuwa ametekeleza vyema majukumu ya kocha wake kumrudisha nyuma Mendes na kumnyima nafasi ya kushambulia mara kwa mara. Kwahiyo Cole Palmer alifunga mawili na kutengeneza moja pengine ndiye angekuwa mchezaji bora mechi. Lakini uamuzi wa FIFA nao uheshimiwe.
Je udhaifu wa Chelsea ni upi?
Chelsea unaweza kushindwa kuwafunga kwa mipira ya krosi, faulo na ile ya juu. lakini katika mfumo wa kujiloinda wanaanzia katikati ya dimba ambako Enzo na Moise Coicedo wanakuwa hapo kusaidiana na wachezaji watatu wa mbele na kuunda ukuta wa wachezaji 6 ambao wanakuwa na jukumu la kuanza linda.
Bahati mbaya Chelsea linapofika suala la kushambuliwa kwa kushtukiza wanaweza kubamizwa mabao mengi. Wanapocheza mtindo wa kuacha mchezaji mmoja nyuma hasa Cucurella ili kukabiliana na’dropping balls’ changamoto yake hana kasi ya kuwamudu wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kukaa na mpira mguuni. Changamoto nyingine ya Chelsea ni safu ya ulinzi hasa nambari 2, 4 na 5 zinaonekana kutokuwa na mwenyewe, yaani hakuna komb
Kibonde cha timu za EPL
PSG wamemaliza msimu huu wakiwa wamefungwa na timu za England. PSG walikutana na Lverpool ambao waliwatupa nje ya mashindano ya Ulaya. Kisha wakaja kukutana na Arsenal katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa ambao waliichapa miamba hiyo ya London na kutinga fainali.
Katika mchezo wa fainali walikutana na miamba ya Italia na kuibuka na ushindi. Lakini kufungwa kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la klabu kumeweka rekodi kuwa PSG licha ya kuzitupa nje timu mbili bado ilikuwa na kibarua kigumu kwa miamba ya England.
Ni PSG hiyo hiyo iliwahi kuchapwa mabao 3 na Tottenham Hotspurs. Ni PSG hii iliwahi kuchapwa mabao mawili ndani ya dakika 10 katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Aston Villa. Hii maana yake PSG wamekuwa wakihangaishwa na timu za England na kwamba msimu huu wamekuwa kwenye kiwango kizuri lakini jumapili wamekumbana na kipigo kikali kutoka timu ya EPL, Chelsea.


Comments
Loading…