in

POGBA ALIRUDI NA TIMU YAKE, POCHETTINO MAJERAHA YALIMMALIZA..

Mohamed Salah, Callum Wilson and Paul Pogba wote wamekuwa na wiki njema kwenye EPL , isipokuwa kwa Hugo Lloris

Manchester United ilienda mechi kadhaa bila uwepo wa kiungo wake ghali Paul Pogba, ambaye alikuwa na majeraha.

Jumamosi alifanikiwa kurudi, na akafanikiwa kufunga goli moja pamoja na kutengeneza goli moja.

Kipi ambacho Manchester United walikuwa wanakikosa kwa Paul Pogba?

Uwepo wa Paul Pogba ulikuwa msaada kwenye maeneo yafuatayo ambapo awali yalikuwa yanapwaya.

Pogba alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuunganisha eneo la kiungo cha kati cha kuzuia na eneo la kiungo cha kushambulia kwa kusukuma mipira kwenda mbele.

Kitu ambacho kilisababisha kuwepo na wingi wa nafasi ambazo zilitengenezwa tofauti na kipindi ambacho yeye hakuwepo.

Ander Herrera alikuwa hana uwezo mkubwa wa kuisikuma timu kwenda mbele na kutengeneza nafasi nyingi .

Kitu hiki Paul Pogba alikifanya kwa kiasi kikubwa.

Pia ubunifu katika eneo la mwisho la kushambulia ulikuwa mkubwa tofauti na kipindi ambacho Paul Pogba hakuwepo.

*Katika mchezo wa wapinzani wa jadi wa London ya Kaskazini ( North London Derby), kipi ambacho kiliwasaidia Arsenal kwa kiasi kikubwa?*

Kabla ya mchezo huu kocha Mauricio Pochettino alikuwa akikabiliwa na majeraha katika maeneo muhimu kwenye timu.

Mfano katika eneo la kiungo, kiungo wake ambaye ameonekana kama nguvu muhimu katika eneo la kiungo la Tottenham Hotspur’s, Danny Winks alikuwa na majeraha.

Hali ambayo ilimpelekea Mauricio Pochettino kumwanzisha Dembele ambaye hakuwa mzima kwa asilimia mia (100%).

Demebel aliwekwa mahususi kwa ajili ya kushinda mipira yote ambayo ilikuwa katika eneo la katikati na kuiamrisha timu yake.

Zoezi hili lililuwa gumu kwake, hivo kumpelekea Sissoko kuwa mtu ambaye alikuwa akiziba na kufukia mabonde.

Sissoko siyo mchezaji ambaye anafunga sana, siyo mchezaji ambaye anapiga pasi za mwisho kwa sana, siyo mchezaji ambaye anapiga pasi nyingi sana na siyo mchezaji ambaye anapiga chenga za maudhi ambazo mashabiki wengi hufurahia.

Lakini Sissoko ni mtu ambaye anafanya kazi ambayo siyo rahisi kwa mtu kuiiona.

Katika mchezo huu , Dembele alishindwa kwa kiasi kikubwa kutimiza majukumu yake ya msingi kwa asilimia kubwa.

Hali ambayo ilimlazimu Sissoko kuleta uwiano katika eneo la katikati ya uwanja.

Sissoko alilazimika sana kufanya kazi ya kushinda mipira na kuiamrisha timu kwa wakati mmoja, alikuwepo kila mahala ambapo mpira ulikuwepo.

Shkodran Mustafi akifurahia bao lake la kwanza dhidi ya mahasimu wao wakubwa Tottenham

Hali ambayo ilimsaidia Erricksen kutokushuka chini saaana kuifuata mipira na kuendelea na kazi yake ya kuiunganisha safu ya ushambuliaji na safu ya kiungo. Sema kilichoharibu ni wachezaji ambao walicheza eneo la mbele hawakuwa wazima kwa asilimia mia (100%).

*Kulikuwa na faida kwa Mauricio Pochettino kuwaanzisha Delle Ali na Harry Kane kwa pamoja ilihali walikuwa na majeraha?*

Inawezekana aliwaza kuhusu *fear factor* , aliamini kabisa kuwepo kwa hawa nyota wawili kungesaidia kutia hofu kwa mabeki wa Arsenal.

Kitu ambacho hakikusaidia kwa sababu kutokuwa kwao fiti kwa asilimia kubwa kulifanya waonekane kama mzigo.

Haikuwa na ulazima wa wao kwa pamoja kuanza pamoja.

Bora angemwanzisha Harry Kane peke yake na akamfanya acheze na Son.

Hii ingemsaidia sana Kane kwa sababu, Son anakitu kimoja ambacho Mara nyingi kinambeba Kane nacho ni kasi yake.

Kasi ya Son ina msaada sana, kama angeanzishwa Son ingewalazimu mabeki wa Arsenal kukabia eneo ambalo Son angekuwepo.

Angewalazimisha kuwasukuma sehemu ambayo angekuwa anakimbilia, hii ingesaidia mabeki wa Arsenal kumfuata na wakati wanamfuata wangeacha uwazi ambao Harry Kane ungemsaidia kufanya Kazi yake bila kutumia nguvu yoyote.

Lakini hii ilikuwa tofauti kwani Delle Ali na Harry Kane wote hawakuwa wazima asilimia kubwa hivo ikawa ngumu kwao kuleta madhara makubwa.

Mail to : [email protected]

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MAURICIO POCHETTINO ATAVUNJA MWIKO WA ARSENAL KUTOFUNGWA MECHI 10 NYUMBANI?

Tanzania Sports

NI MAPEMA MNO KUWAKATIA TAMAA REAL MADRID