in

Plaza kwa Tyson, PTA kwa Matumla, Mwakinyo je?

Hassan Mwakinyo

Ukitokea  unamamsha usingizini Mike Tyson ambaye ni bingwa wa zamani wa mikanda mikubwa WBC, IBF na WBA wapi anapakumbuka zaidi katika historia yake ya masumbwi basi hatosahau kuutaja ukumbi wa Trump Plaza huko Marekani ‘USA’.

Julai 11 mwaka 1985 alipo mtwanga vibaya bondia John Alderson katika ukumbi huo huku tayari akiwa alishampasua bondia mwingine Jack Johnson miezi kadhaa iliyopita.

Ukumbi huo ulikuwa na faida kubwa sana kwake kwani ndani ya mwaka huo Mike Tyson alimtandika vibaya Donnie Long kwa ‘KO’.

Utofauti uliopo na hawa mabondia wa kisasa wakati wa Mike Tyson alikuwa anapigana kwa muda mchache sana yaani wakati mwingine huchukua mwezi mmoja kuingia katika pambano lingine.

Wakati huo mabondia wa sasa wanatumia kujiandaa kwa zaidi ya miezi tisa hadi mwaka kupigana pambano moja, lakini Tyson alipigana mapmbano manne mwaka 1985, tena aliendelea kuutumia vizuri mwaka huo kwa kumbutua Eddie Richardson.

Mwaka 1985 aliumaliza kwa kumgalagaza Sammy Scaff na akaumaliza mwaka huo bila kupigwa, hapo alikuwa na miaka 19 tu amefanya makubwa jina lake likawa kubwa duniani kote na akaweza kujitengenezea ufalme wa aina yake, na nikiri tu hata mie nilikuwa shabiki yake na niliumia wakati alipopigwa na Lenox Lewis mwaka 2002 kwani si dhambi kusema ukweli.

Mwaka uliofuata ulikuwa wake na kutumia vizuri kwa kuwaangusha mabondia wengi tena walikuwa na uwezo mkubwa hadi ilipofikia kwa Frank Bruno ambaye alikuwa na uwezo mkubwa naye amemvuruga vibaya sana.

Hawa wanaotamba hivi sasa kina Anthony Joshua, Deontay Wilder, Tyson Fury na Dilan White, ndio hao wanaotumia muda mwingi kujiaandaa tukifika kushuhudia pambano lenyewe halina mvuto kama ndugu yetu, Floyd Mayweather akirusha ngumi moja yupo Ununio ngumi ya pili anarudi Kinondoni Moscow unakuja kugeuka pambano limeisha na kachukua ubingwa.

Wakati Tyson anafanya makubwa duniani na kutengeneza mashabiki wengi ulimwenguni huku bongo , akaibuka mtu aliyekuwa katika familia ya ngumi, Rashid Matumla ‘Snake Boy’ naye aliweza kuchukua ufalme wake huku kwetu Tanzania.

Matumla ambaye  alianza mchezo huo miaka ya 1980 kwa maelezo yake mwenyewe tena katika majeshi huko ameshiriki mashindano mengi yaliyokuwa na tija kwake kufahamika kimataifa.

Aliweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa lakini naye ukumbi ambao huenda hatousahau ni ule wa PTA Dar es Salaam.

Hapa ndipo yanafanyika mashindano mbalimbali ya mchezo wa ngumi na ndipo sehemu ambayo pana mafanikio ya watu wengi walio katika tasnia ya masumbwi.

Lakini Matumla alikuwa tofauti kidogo na Tyson kwani mwenzake alikuwa anamaliza pambano hata ndani ya sekunde sitini na wengi waliokuwa wanaenda kuutazama mchezo huo wanakosa pambano.

Inawezekana ikawa kama hadithi mpya kwa ambao hawakuweza kuwona mabondia hao wakati wakiwa katika ubora wao ila tu wajue hawakuwa watu wa kawaida.

Kijiti kupokezana sasa yupo Hassan Mwakinyo kutoka Tanga, anakuja vizuri sana ila kitu kimoja ambacho bado anahitaji kujirekebisha na kukiweka sawa nidhamu.

Baadaa ya kushinda pambano lake dhidi ya Mphilipino Anael Tinampay aliweza kuongea maneno mengi baada ya maelezo mafupi ya Rashid Matumla.

Aliongea na huku akitoa maneno mabovu kwa mkongwe huyo ila ile yote ilikuwa ujana pamoja na mafanikio ya ghafla. Baadae aliweza kurudi nyuma na kuomba msamaha na kuweka kila kitu sawa.

mchezo wa ngumi Tanzania hauwezi kufika sehemu yoyote kama viongozi wanaoutawala mchezo huo hawajakaa sawa na kuelewana.

Hata akama waliweza kukaa na uongozi wa juu ila bado kuna baadhi ya viongozi wamekunja roho zao hivyo hauwezi kufika popote.

Ikumbukwe kuwa mchezo huu unahusisha maisha ya watu katika kujitolea, nguvu na miili yao kuweza kuucheza na kuhitaji fedha kwa ajiri ya familia zao.

Kama kutatokea viongozi hawaelewani au kutokukubali mfumo uliopo wanapunguza ajira za watu maana sio jambo sahihi kuweka kauzibe.

Ukitaka kugundua kuwa wamepita wanamichezo wengi wa mchezo wa ngumi walio na vipaji kukosa umakini wa viongozi wanajikuta wakirudi nyuma na vipaji vyao kufa.

Kuhusu maswala ya ubovu wa viongozi tumeshaongea sana sasa wanatakiwa wabadilike na watengeneze ukurasa mpya kama wanahitaji mabadiliko ya kweli.

Labda tu niwakumbushe baadhi ya mabondia waliowahi kufanya vizuri hapa Tanzania, Rashid Matumla, Hassani Matumla, Mbwana Matumla, Francis  Cheka, Francis Miyeyusho, Abdallah Pazi, Awadhi Tamimu na wengine.

Wanaokuja juu sasa Mfaume Mfaume, Hassan Mwakinyo na Ramadhani  Shauri hao ni baadhi, sio wote lakini ukiangalia niliowataja wangeweza kufanya makubwa zaidi ya hapo walipo sasa unadhani tatizo liko wapi ?

Hii nakuachia wewe msomaji lakini huku katika michezo kunatakiwa kuchukuliwe hatua ngumu sana ili mambo yakae sawa na kila mmoja anufaike na anachokifanya, naamini katika hao ukimuuliza amenufaika na nini katika ndondi sijui atakujibu nini.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Klabu za Tanzania zinajua umuhimu wa Physiotherapists?

Tanzania Sports

Vikwazo kurejea EPL