in , , ,

Pellegrini atisha kwa washambuliaji

 

*Wametimia wanne, Chelsea, Man U nao waja

*Kazi bado ipo Arsenal, Liverpool, Tottenham

 

 

Manchester City wameshatumia karibu pauni milioni 100 katika usajili unaoendelea, kwa kunasa wachezaji wanne tu.

 

Kocha mpya Manuel Pellegrini ameingiza wachezaji hao, wawili kati yao wakiitia makali safu ya ushambuliaji.

 

Baada ya Mario Balotelli kuuzwa AC Milan Januari na Carlos Tevez kutimkia Juventus, zote za Italia, safu ililegea na tayari Pellegrini amepenyeza karibu pauni milioni 45 na kuwanasa Alvaro Negredo na Stevan Jovetic.

 

Hao wanaungana na Sergio Aguero na Edin Dzeko waliokuwapo na kuwafanya Manchester City kuwa na washambuliaji wanne wenye vipaji vya aina yake katika Ligi Kuu ya England (EPL).

 

Jovetic anaweza kucheza nyuma ya namba tisa, akanasa umiliki wa mpira katika vyumba vya ndani, na kwa ujumla anaelekea kuwa kiungo kizuri miongoni mwa washambuliaji watatu pale mbele.

 

Hana ajizi katika kufunga pia, maana katika misimu miwili iliyopita akiwa na Fiorentina alipachika mabao 27.

 

Kwa upande wa Negredo, hakuna shaka kwamba ni mshambuliaji mahiri, namba tisa asiyeulizwa swali, hivyo ni wazi patakuwa na shughuli pevu ndani ya eneo la penati.

 

Aguero ana kila kitu, anashusha mpira chini, ana nguvu na uwezo wa kuwavuka walinzi, hata kama wanaonekana ni ‘msitu’. Hana tabu hata akichezeshwa nyuma kidogo ya namba tisa.

 

Dzeko anajulikana mikiki yake, hadi akaitwa ‘super sub’, kwa jinsi alivyowanusuru City kwenye mechi nyingi ama kwa kupachika mabao ya kusawazisha au ya ushindi. Tusubiri tu ligi ianze mwezi ujao.

 

Kwa kuzingatia kiasi cha fedha kilichotumika kuwasajili Negredo na Jovetic, inaweza kutarajiwa kwamba ndio watakuwa wakianza mechi nyingi, kama watakuwa fiti. Aguero naye anaweza kuanza mechi nyingi na Dzeko akatulia, maana hana tatizo.

 

 

 

CHELSEA NAO SI HABA
photou

 

 

 

Iwapo Chelsea watafanikiwa kumsajili Wayne Rooney, nao wanaweza kujidai kuwa na washambuliaji wanne wazuri.

 

Wanao Romelu Lukaku, Fernando Torres na Demba Ba ‘wenye mabao miguuni’ mwao, lakini bado huwezi kulinganisha na wale wa City.

 

 

 

MANCHESTER UNITED WANAJIVUNIA RVP

 

 

 

Manchester United, kwa sasa, wanao washambuliaji wanne, Rooney akiwa mmoja wao, ambapo ni yeye na Robin van Persie tu ambao ni washambuliaji kwa maana halisi ya jina lenyewe.

 

Javier Hernandez ‘Chicharito’ amekuwa chanzo cha mabao misimu kadhaa iliyopita pia na wa nne ni Danny Welbeck, lakini bado hajaonesha makali ya kuwa mshambuliaji wa kati, zaidi ya kuwezea kwenye winga.

 

 

ARSENAL, LIVERPOOL, SPURS BADO
IMG_0349

 

 
Arsenal bado wanahangaika na kumpata Luis Suarez kwa sababu ya upungufu wa washambuliaji mahiri.

 

Wanaweza kumweka Theo Walcott kama mpachika mabao, lakini ukweli ni kwamba huyu ni winga. Anayetegemewa ni Olivier Giroud nap engine Lukas Podolski.

 

Ipo kazi ya kuinoa fowadi yao, kwa maana ya kutafuta watakaochukua nafasi za akina Park Chu-Young, Marouane Chamakh na Nicklas Bendtner.

 

Liverpool wana washambuliaji wawili wazuri kabisa, Suarez na Daniel Sturridge, lakini Suarez haelekei kubaki. Tottenham Hotspurs nao wana wawili tu, ndio maana wanapambana kupata wengine.

 

Kwa msingi wa kiwango na eneo, City katika muda huu wameshafanikiwa kuinoa safu yao ya ushambuliaji na inatarajiwa kuwa tishio kwa wapinzani wao, na ndiyo sababu hadi sasa Pellegrini anatabasamu.
Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

‘£9bn zilitumiwa vyema Olimpiki’

Lewis Hamilton ashinda Hungary