1:Huwezi sema kadi haikuwa sahihi, au haikutakiwa kutolewa kwa sababu
ilikuwa mechi kubwa, kosa alilofanya Ander Herrera lilikuwa
linastahili kadi ya njano, bahati mbaya kwake ilikuwa kadi ya pili ya
njano.
Kutolewa kwa Ander Herrera kulibadilisha vitu viwili kwenye mchezo wa jana.
Moja, Chelsea waliacha kushambulia kwa kushtukiza, waliamua kusogea
zaidi kwenye eneo là timu ya Manchester United na kuanza kutia presha.
Pili, Manchester United waliamua kujilinda muda mwingi wa mchezo.
Na walikuwa imara sana, walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendana na
presha ya mashambulizi ya Chelsea.
Hawakulazimishwa kufanya makosa, walicheza kwa utulivu na nidhamu kubwa sana.
2:De Gea anaweza akawa mhimili mkubwa sana kwa Manchester United
kipindi ambacho timu haichezi, na Zlatan Ibrahimovich ni mchezaji
muhimu sana kipindi ambacho timu inacheza.
Na hiki kitu kilionekana sana kwa kiasi kikubwa. Jana De Gea amechomoa
michomo ambayo iliifanya Manchester United iendelee kuwepo kwenye
mchezo kwa muda mrefu. Lakini kitu kilichokuwa kinakosekana mbele ni
ukomavu wa idara ya ushambulizi.
Kuna wakati timu ilikuwa inapata nafasi za kushambulia lakini ilikuwa
inashindwa kufanya maamuzi ya kubadilisha nafasi kuwa magoli kwa
sababu ya kukosekana kwa ukomavu, mfano kuna nafasi ambayo Rashford
aliipata akiwa na kipa akashindwa kufunga,ile presha ya mchezo
ilimnyima utulivu wa kufanya maamuzi. Ndipo hapo maana yangu
inapozaliwa ya Zlatan ni mtu wa muhimu wakati United ikiwa
inashambulia .
Uwepo wake ungemfanya awe na utulivu kwa sababu ni mkomavu katika
kutuliza presha ya mpira ndani yake.
3:Chelsea Wametumia masaa 168 Yani siku 7 kujiandaa dhidi ta
Manchester United .
Ndani ya hizo siku 7 Manchester Unités walisafiri kwenda Rusia umbali
wa masaa 12 mpaka kufika. Wakapumzika wakacheza mechi n’a Rostov.
Baada ta mèchi wakasafiri kurudi England masaa 12 tena mpaka wachezaji
kuja kumpumzika jumla wametumia masaa 114.
Kwa haraka haraka wametumia masaa 54 kujiandaa kucheza na chelsea.
Wachezaji ni binadamu wanahitaji kupumzika ili kupumzisha viungo na
kuregain fitness. Mechi 3 ndani ya siku 7 Chelsea mechi 1 ndani ya
siku 7. Ilikuwa ngumu kwao ikizingatia walikuwa wanakutana na timu
kubwa na bora kama Chelsea.
4: Viwango vya baadhi ya wachezaji wa Chelsea jana kilikuwa bora sana
hasa kina Hazard, Kante na wengine.
Hali iliyowapa ugumu kwa kiasi kikubwa Manchester United kumiliki
mpira wakati walipokuwa pungufu baada ya Herrera kutoka.
Martin Kiyumbi.