in , , ,

Ozil, Welbeck wawang’arisha Arsenal


*Liverpool watota kwa vibonde West Ham

Mzunguko wa tano wa Ligi Kuu ya England (EPL) umekuja kivingine, nyota wa Arsenal waliokuwa wakilaumiwa, Mesut Ozil na Danny Welbeck kuwasaidia kupata ushindi wa 3-0 ugenini kwa Aston Villa.
Welbeck aliyesajiliwa kutoka Manchester United msimu huu alimtengea Ozil aliyefunga bao la kwanza dakika ya 32, kabla ya Mjerumani huyo kumpa majalo Welbeck na kufunga dakika mbili baadaye, kisha shuti la beki wa kushoto, Kieran Gibbs kumkuta mlinzi Aly Cissokho wa Villa aliyejifunga.

Arsenal walitawala mchezo kwa 71.4% na pasi zao kwa ujumla zilikuwa 814, ikilinganishwa na 312 za Villa ambao hii ni mechi ya kwanza kupoteza msimu huu, kocha wao, Paul Lambert akisema ni kwa sababu wachezaji wake wana maradhi yaliyosababishwa na kirusi kambini mwao.

LIVERPOOL WAPIGWA NA THE HAMMERS
LONDON_ENGLAND

Liverpool wameendeleza mdororo wa soka baada ya kufungwa 3-1 na timu dhaifu ya West Ham ‘The Hammers’ licha ya kutawala mchezo kwa asilimia 62.
Hiki ni kipigo cha tatu kwa Liverpool katika mechi zake tano za mwanzo, ambapo kocha wao, Brendan Rodgers amesema lazima wachezaji wake wajipange upya. Wanapata matokeo mabaya baada ya kumuuza Luis Suarez kwa Barcelona na mshambuliaji wake pacha, Daniel Surridge kuumia majuzi.

Mabao ya mapema ya Winston Reid na Diafra Sakho yaliwaweka vyema wenyeji licha ya Raheem Sterling kuchomoa moja kabla ya mapumziko huku Morgan Amalfitano akitia msumari kwenye jeneza la Liverpool kwa kufunga la tatu dakikaya 88.

Kocha Sam Allerdyce alikuwa katika shinikizo la kufanya vyema baada ya kupoteza mechi zote mbili za nyumbani msimu huu. Liverpool waliwekwa pabaya kwa Mario Balotelli kupewa kadi ya njano baada ya kutaka kuzipiga na kipa wa The Hammers, Adrian lakini pia Javi Manquillo aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mamadou Sakho.

NEWCASTLE, HULL, SUNDERLAND, BURNLEY SARE

Kocha Alan Pardew wa Newcastle aliye kwenye shinikizo la kufukuzwa kutoka kwa washabiki alikuwa na wakati mgumu Jumamosi hii baada ya kupelekeshwa na Hull, lakini akafanikiwa kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuambulia sare ya 2-2.

Washabiki wa Newcastle walichapisha nakala 30,000 za stika kubwa za kutaka kocha huyo afukuzwe, pakiwa na picha yake na hata baadhi ya magari yameandikwa ujumbe ‘SACKPARDEW.COM’ yenye picha yake pia.

Nikica Jelavic na Mohamed Diame waliwafungia Hull mabao ya mapema, lakini wakati washabiki wa Newcastle wakiendeleza malalamiko dhidi ya kocha wao wakiwa nyumbani, wachezaji walipambana na kufanikiwa kurudisha mabao katika dakika ya 73 na 87 kupitia kwa Papiss Cisse.

Katika mechi nyingine, Southampton waliendeleza makali yao mapya msimu huu licha ya kupotelewa na wachezaji nyota watano, kwa kuwafunga Swansea 1-0 kupitia kwa Mkenya Victor Wanyama.
Swansea walicheza wakiwa 10 kwa zaidi ya nusu ya mchezo kwani mshambuliaji matata Wilfried Bonny alipewa kadi nyekundu baada ya kufanya rafu mbili za kizembe.
Queen Park Rangers (QPR) na Stoke walikwenda sare ya 2-2 huku Burnley na Sunderland wakitoka suluhu. Jumapili hii ni kivumbi baina ya Chelsea wanaocheza ugenini kwa Manchester City jioni ambapo Jose Mourinho amesema anacheza kamari kwa kumwanzisha Diego Costa licha ya kuwa si timamu wa mwili.

Leicester wanawakaribisha Manchester United muda wa mchana sawa na Tottenham Hotspur wanavyokuwa wenyeji wa West Bromwich Albion. Crystal Palace ni wageni wa Everton leo hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Wembley: Fainali Euro 2016

Manchester United waoga kichapo