*Simba waahidi makubwa, Mbeya City hao
*Azam nao wajiwinda kuwapiga Ferroviario

Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) limetoa ruhusa kwa mshambuliaji wa Uganda, Emmanuel Okwi kuchezea Yanga.

Fifa imesema kwamba Okwi ana haki ya kuendelea kucheza na Yanga ni ruksa kutumia huduma zake, kwa sababu kesi iliyopo huko haihusiani na Yanga.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa amesema kwamba Fifa wamewapatia maelezo hayo baada ya wenyewe TFF kuulizia.

Awali TFF iliwashauri Yanga wasimtumie Okwi kwa vile alikuwa anahusishwa na mashauri mawili huko Fifa. Moja ilikuwa Okwi kuidai klabu yake ya zamani ya Etoile du Sahel ya Tunisia na pili klabu ya awali ya Okwi, Simba ya Tanzania kuwadai Etoile mamilioni ya fedha za kumuuza huko Okwi.

Mganda huyo aliyewika kwa kupachika mabao na Simba baada ya kuuzwa Tunisia alirejea nyumbani kwao alikochezea Sports Club Villa nayo ikaja kumuuza Yanga kwenye dirisha dogo la Januari mwaka huu lakini akashindwa kucheza.

Habari za awali zilidai kwamba Okwi angepelekwa Comoro kwa ndege ili kuchezea Yanga kwenye mechi dhidi ya Komorozione lakini habari nyingine zinadai atabaki nyumbani asubiri Ligi Kuu na mechi ya Yanga dhidi ya Al Ahly ya Misri kama watavuka kwa Wacomoro hao.

Simba waahidi kurudia makali

Wachezaji wa Klabu ya Simba wameahidi kurejea kwenye makali yao na kuanza tena kushinda mechi kama awali.

Wachezaji hao walitoa ahadi hiyo walipokutana na Mwenyekiti Ismail Aden Rage baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Mgambo ya Tanga kwa 1-0 wakati mzunguko wa kwanza Simba waliwabamiza 6-0.

Simba walitoka sare na Mtibwa Sugar na walipokwenda Tanga wakaangukia pua na mechi ya tatu mfululizo ya ugenini ni kwa Mbeya City jijini Mbeya.

Wikiendi hii Simba wanakwaana na timu ambayo katika mzunguko wa kwanza haikufungwa na timu yoyote na walikuja kufungwa na Yanga tu walipokutana majuzi kwa 1-0.

Tayari Mbeya City wamewapiga mkwara Simba, wachezaji wakisema kwamba watafia uwanjani kuhakikisha wanachomoza na ushindi kwenye dimba la Sokoine.

AZAM KAZI NGUMU KWA WAMAKONDE

Nao Azam walioshika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu msimu uliopita wikiendi hii wanajitupa uwanjani kurudiana na Ferroviario.

Wana Lambalamba wanacheza nchini Msumbiji kusaka ushindi, suluhu au sare kwa sababu kwenye mechi ya awali walishinda kwa 1-0 kwa bao la Kipre Tcetche.

Jemedari Saidi ambaye ni Meneja wa Azam ameahidi kwamba vijana wake watajituma kwenye mechi hiyo muhimu ili kuvuka.

OLJORO KOCHA MPYA

Timu ya JKT Oljoro imemwajiri aliyepata kuwa mwalimu wa Toto African ya Mwanza kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Hemedi Morocco.

Oljoro wamekuwa wakifanya vibaya kwenye ligi licha ya kuwa timu ya maafande, na Morocco amesema anaachia ngazi kwa sababu ya kutokuwa na mawazo ya aina moja na uongozi.

.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Rio

Man United yanyemelewa na hasara


SIMBA YAGOMA KUKATWA MKIA SOKOINE-MBEYA