David De Gea

Klabu ya Real waliomkosa kipa waliyemtarajia, David De Gea kutoka Manchester United, wamesema bayana kwamba walifanya kila waliloweza kukamilisha usajili huo lakini Mashetani Wekundu ndio walikwamisha mchakato.

Katika taarifa yao, Madrid wanasema kwamba United walifungua mazungumzo juu ya kumtoa kipa huyo ili nao wamchukue wa Madrid, Keylor Navas lakini United wakachukua saa nane nzima kujibu masuala ya mikataba ya wawili hao.

Madrid waliomruhusu kipa wao namba moja, Iker Casillas aliyekuwa pia nahodha wao ajiunge na Porto wa Ureno, wanasema kwamba walifikia makubaliano haraka na United juu ya usajili, na kwamba saa 7:39 mchana wa Jumatatu waliwatumia Man U mikataba husika,lakini United wakakaa kimya hadi saa 3:43 usiku walipowatumia marekebisho kidogo.

Taarifa ya Real Madrid
Taarifa ya Real Madrid

Wahispania hao wakazidi kudai kwamba United walijaza maelezo kumhusu De Gea lakini hawakufanya hivyo kuhusu yale ya Navas kwenye Transfer Matching System (TMS) ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Wanazidi kulalamika kwamba nyaraka kutoka Man United ziliwafikia dakika mbili baada ya dirisha la usajili kufungwa rasmi nchini Hispania. Dirisha la England linafungwa usiku wa leo.

Hata hivyo, Manchester United wanadai kwamba walipeleka kila kitu ndani ya muda, lakini Madrid walishindwa kuzifungua kwa sababu ya matatizo ya teknolojia na kwamba Real hawakupeleka nyaraka hizo kwa Shirikisho la Soka la Hispania.

Kwa hali ilivyo hakuna dalili za Real kukata rufaa, maana wanakiri wenyewe kwamba nyaraka zilifika zikiwa zimechelewa kwa dakika mbili, na hiyo itamaanisha kwamba De Gea atabaki United kwa msimu huu wa mwisho na ataondoka kama mchezaji huru bila United kuingiza senti tano.

De Gea alijiunga na Man United 2011 akitoka kwa Atletico Madrid ambao ni mahasimu wakubwa wa Real katika Jiji la Madrid. Alisajiliwa Old Trafford kwa pauni milioni 18.9 na ilikuwa jana arudi Hispania kwa pauni milioni 29, ambapo United wangefaidi.

Hivi sasa United, kama mambo yatabaki yalivyo, watakuwa na makipa wanne, ambao ni De Gea, Sergio Romero, aliyeanza mechi zote za msimu huu, Victor Valde ambaye dili lake la kujiunga Besiktas lilikwama huku akiwa amekosana na kocha Louis van Gaal. Kipa mwingine aliyekuwa wa akiba mechi za msimu huu ni Sam Johnstone.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

TIMU YA WIKI EPL

VAN GAAL BADO ANATENGENEZA TIMU