in

Natamani MESSI acheze na RONALDO

Messi

Mungu ametoa baraka yake kwenye macho yetu kuwashuhudia Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Hili ndilo jambo kubwa na la kwanza ambalo tunatakiwa kushukuru.

Tunatakiwa kushukuru kwa sababu tumeshuhudia miaka zaidi ya kumi ya wanadamu wawili bora uwanjani kwenye kizazi hiki cha hivi karibuni.

Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa sababu tumeshuhudia miguu minne isiyo tetereka kwenye viwanja vya mpira wa miguu. Miguu miwili ya Lionel Messi ilikuwa miguu hodari sana ndani ya miaka kumi iliyopita.

Miguu miwili ya Cristiano Ronaldo ilikuwa miguu bora ndani ya miaka kumi iliyopita.  Kwa pamoja miguu yao minne haijawahi kuchoka kirahisi.

Ni miguu ambayo kila uchwao imekuwa na njaa ya kufunga magoli. Miguu ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa na uadui na magolikipa na ikajenga urafiki na nyavu za magoli.

Miguu ambayo sanaa ya mpira wa miguu ilikuwa ndiyo sehemu pekee ambayo ilizaliwa na kuishi. Kila aina ya sanaa ya mpira wa miguu ilikuwa inapatikana kwenye miguu ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Ndani ya miaka kumi wamefunga kwa kutumia miguu yao yote minne kwa pamoja. Kwa miaka kumi wamefunga magoli kwa kutumia vichwa vyao viwili. Kwa kifupi sanaa ya kufunga magoli ilikuwa ndani yao.

Kwa miaka kumi iliyopita walihakikisha wanatengeneza magoli mengi kwa wachezaji wenzao. Hawakuwa wachoyo kwa wachezaji wenzao. Walihakikisha wanatengeneza nafasi kwa wenzao ili wafunge magoli.

Kwa miaka kumi iliyopita Cristiano Ronaldo na Lionel Messi waliigawa dunia katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni Cristiano Ronaldo na upande wa pili ni Lionel Messi. Waliwagawa mashabiki wa mpira wa miguu pande hizi mbili.

Kwa miaka kumi iliyopita walihakikisha wanazitawala tunzo mbalimbali za mpira wa miguu. Tunzo mbalimbali  hazikuwa na maana yoyote bila ushindi wa Cristiano Ronaldo au Lionel Messi.

Ndiyo maana Ballon D’or walikuwa wanagawana wenyewe kwa wenyewe kwa muda wa miaka kumi mfululizo. Hawa ndiyo magwiji wa mpira wa miguu kwa miaka ya hivi karibuni.

Wameshinda makombe mengi, wamefanya vitu vingi kwenye mpira wa miguu . Vitu ambavyo wengi wetu tunajivunia kuwa sehemu ya kuvitazama hivo vitu.

Kuna jambo moja ambalo binafsi nalitamani lifanyike kwao. Natamani kuwaona Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakicheka timu moja.

Natamani kuiona safu ya ushambuliaji kali inayoongozwa na wachezaji wawili wenye uwezo wa kufunga magoli zaidi ya 60 ndani ya msimu mmoja.

Natamani kuona safu ya ushambuliaji yenye uwezo wa kutengeneza magoli zaidi ya 50 ndani ya msimu mmoja. Safu ya ushambuliaji yenye makali ambayo yanaogopesha.

Safu ya ushambuliaji yenye njaa. Yenye urafiki na nyavu za golini na uadui mkubwa na magolikipa pamoja na mabeki wa timu pinzani. Naitamani sana hii siku itokee.

Siku ambayo wale mashabiki waliogawanywa ndani ya miaka kumi iliyopita wakaungana tena kwa pamoja kuwashabikia Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao watakuwa wanacheza timu moja.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
kikosi cha yanga

Yanga bado inaomba omba?

Tanzania Sports

Yanga, Simba, Arsenal Ndani Ya Tukio Moja