Timu ya soka ya Namungo FC msimu uliopita ilifanya vizuri sana kwa mara ya kwanza inaingia katika ligi na inafika nafasi ya nne pia inapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa katika kombe la Shirikisho.
Mwenendo wa timu hii katika ligi msimu huu sio mzuri sana wala sio mbaya sana kwani katika michezo mitano timu hiyo imeshinda miwili na imepoteza mitatu.
Imefungwa magoli 3 imefunga magoli mawili hivyo inaondoka na alama sita ikiwa na ndeni la goli moja.
Namungo hii ndio inayotazamiwa kucheza michezo ya kimataifa ya kombe la Shirikisho.
Kila mmoja anabakia kuwa na swali ni kweli inaweza kufanya vizuri kama ilivyokuwa hapo awali katika ligi au ndio wanaenda kushiriki sio kushindana.
Baadhi ya viongozi wao wameweka wazi kuwa kuna tatizo kwa wachezaji pamoja na viongozi huku kocha naye akiwa na matatizo.
Kwa kauli hii unaweza kufikiria nini juu ya timu hii inayoenda kucheza michezo migumu zaidi ya hii ya ligi kuu Bara.
Hilo swali litabakia kuwa kitendawili hadi hapo watakapo tegua wenyewe ndio tutajua kuwa imejipangaje, ila Waswahili wanasema biashara asubuhi jioni mahesabu.
Endapo Namungo wakitaka kufanya mabadiliko basi kipindi hiki ndio sahihi kwao wafanye haraka iwezekanavyo vinginevyo itawagharimu.
Lakini kama bado wanaimani na kila kinachoendelea hivi sasa basi watoe ushirikiano kwa asilimia zote ili kuipeleka timu katika sehemu nzuri.
Hatutaki kuona vipingo vikubwa vikirudi bongo, tunachotaka mpira mzuri pamoja na matokeo uwanjani, hayo ndio matarajio ya kila mmoja kwa timu zinazocheza nyumbani kasoro Yanga na Simba.
Yanga na Simba hata zikicheza wapi hazitakiani mema ndio maana nimetaja kasoro timu hizo.
Huenda hela haikuwepo kuweza kuwabakisha baadhi ya nyota wao waliofanya vizuri msimu uliopita.
KWANINI IWE SINGIDA UNITED ILIYOCHANGAMKA
Wakati Singida United ilipopanda dara tena miaka minne nyuma 2016 ila ilishuka daraja tangu mwaka 2000 wengi hawakuamini uwekezaji uliofanyika pamoja na wadhamini waliopatikana.
Singida ilikuwa miongoni mwa vilabu vilivyokuwa mfano wa kuigwa kwa kupata wadhamini wengi.
Msimu ule waliopanda daraja alifanya vizuri sana walitikisa soka la Tanzania, walifika hadi zile tano bora VPL.Timu hii ilishuka taratibu na baadae ikatoweka kabisa.
Tena wakati inashuka ilianza na matokeo ya ajabu sana na baadae msimu uliopita imeondoka VPL na kutupwa ligi daraja la kwanza (FDL).
Kwa namna navyoiona Namungo kama vile nayo inaelekea kuwa Singida United kwa msimu huu au hata ujao.
Hii itatokana kama hawajaweka mambo sawa wakizubaa wataangukia pua.
TUUNGE NA HISTORIA YA VPL
Mpira wa miguu ni mchezo wa wazi haujifichi kila kitu kinaonekana na muelekeo wa timu unaonekana uwanjani wakati mchezo unachezwa.
Ligi kuu ya Tanzania Bara tangu itambulike rasmi miaka 55 iliyopita hii ina maana ligi hii imeanza kutambulika mwaka 1965.
Yanga na Simba ndio timu pekee ambazo zimefanya vizuri na zimechukua ubingwa wa ligi mara nyingi zaidi, katika miaka 55 timu nne pekee zilizochukua ubingwa hapo katikati ambazo ni Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union na Tukuyu Stars.
Tuhesabu sasa Yanga imechukua mara 27 wakati Simba imechukua mara 21 ukijumlisha hapo unapata 49 , hizo sita zilizobaki ndio timu nne zimechukua.
Mtibwa Sugar imechukua mara 2 mwaka 1999 na 2000 wakati Tukuyu Stars imechukua mara moja, Azam FC nayo imechukua mara moja mwaka 2014 pamoja na Coastal Union 1988.
Msimu huu kuna utofauti kidogo miamba mitatu iko kamili yaani Azam inayoongoza ligi kwa alama 15 ikitafuna michezo yote 5, huku Yanga na Simba zikishika nafasi ya pili zikiwa na alama 13 ila Simba ikiwa mbele kwa magoli mengi ya kufunga.
Je Ubingwa unaenda kwa Zakazakazi au kwa Nugaz ama utabik wa Manara ? ni swala la muda tu tusubiri.
Comments
Loading…