in ,

Hispania, Ureno nguvu moja

ureno

Hispania na Ureno wameamua kuunganisha nguvu kwa ajili ya kuomba kuandaa kwa pamoja fainali za Kombe la Dunia 2030.

Hispania wamesema kwamba wameona hawawezi kupata mshirika mshirika mzuri zaidi kwa ajili ya michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Shirikisho la Soka la Hispania (RFEF) linasema katika taarifa yake kwamba kinachofanyika sasa ni kuweka mikakati ya kufanikisha mpango huo wakati ukiwadia. Mashirikisho hayo yalitia saini makubaliano hayo kabla ya mechi ya kirafki baina yao jijini Lisbon, Ureno.

Katika mechi hiyo, timu hizo zilikwenda suluhu ambapo kwa mara ya kwanza Hispania walimwanzisha mchezaji Adama Traore aliyezalika Hispania kwa wazazi kutoka Mali na kuamua kubaki na uzalendo kwa alikozaliwa badala ya kwa wazazi wake.

“Mambo machache yanaweza kuleta matumaini na matarajio juu ya fursa ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia, nasi hatuwezi kuona mshirika mzuri kuliko Ureno,” ilikuwa kauli ya Rais wa RFEF, Luis Rubiales.

Hispania iliandaa na kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia 1982 na walitoa maombi ya kuandaa fainali nyingine pamoja na Ureno 2018 lakini wakashindwa zikapelekwa Urusi, japokuwa inadaiwa kulikuwa na utolewaji wa mlungula.

Wakati wawili hao wakifanya mpango wa jambo lao hilo, kwingineko Amerika nchi nne za Argentina, Uruguay, Chile na Paraguay zimetangaza kuunda umoja wa kuandaa fainali hizo. Uruguay ndio waliandaa fainali za kwanza za Kombe la Dunia zilizofanyika 1930.

Mashirikisho manne ya soka ya Uingereza yanafikiria nayo kutoa ombi kama hilo kuandaa fainali hizo wakiungana na Ireland. Kwingineko, Bulgaria, Serbia, Ugiriki na Romania nao wanajipanga. Uombaji unaanza rasmi 2022 na Fifa watachagua wenyeji 2024.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Alex Telles

Manchester United taabani

Namungo fc

Namungo ni Singida United iloyochangamka