in , , ,

NAFASI NZURI KWA MAKAMPUNI KUNUFAIKA KIBIASHARA NA SERENGETI BOYS

Nafasi hutokea kwenye maisha ya mwanadamu kila siku, hakuna mwanadamu
àmbaye hajawahi kupata nafasi yoyote katika maisha yake.

Wingi au uchache wa nafasi zinatokea katika maisha ya mwanadamu hazina
maana yoyote kama hakuna matumizi sahihi ya hizo nafasi.

Matumizi sahihi ya nafasi ndicho kitu cha muhimu katika maisha kuliko
wingi au uchache wa nafasi unazozipata. Hata kama ukipata nafasi moja
unachotakiwa ni kuitumia ipasavyo hiyo nafasi kwa faida ya maisha
yako.

Na kuna wakati nafasi inaweza ikaja katika maisha yako na ukashindwa
kuiona kama ni nafasi mpaka pale utakapooneshwa na mtu mwingine.

Tunatofautiana kutazama vitu, hali ambayo inapelekea pia tutofautiane
kutafasri vitu tunavyovitazama katika maisha, jicho lako là nyama
linaweza likawa halioni katika usahihi wake na ukahitaji jicho jingine
kwa ajili ya kuoneshwa njia sahihi ya kupitia.

Moja ya sehemu ambayo inahitaji kuwa na jicho là ziada ni kwenye
biashara, kila uchwao kuna ongezeko kubwa là biashara. Hâta vitu
ambavyo tulikuwa tunaviona kama huduma kwa mwanadamu,leo hii
vinafanyika kama biashara.

Watu wenye jicho là ziada walilitazama suala là elimu katika jicho là
biashara na siyo katika jicho là huduma ndiyo maana waliamua kujenga
shule na kufanya biashara, vivyo hivo kwa watu watoaji huduma ya Afya,
wameshageuza huduma ya afya kuwa biashara. Hii yote inaonesha kila
sekunde hutoa nafasi kwa mwanadamu kugeuza changamoto kuwa biashara
kubwa katika maisha yake.

Kama ilivyo kwenye huduma ya Afya na Elimu, mpira siku hizi ni zaidi
ya burudani kama ilivyokuwa zamani. Mpira ni biashara kubwa sana.
Biashara ambayo inawafanya matajiri mbalimbali kutoka America, Afrika,
Ulaya, Uarabuni na kila sehemu kuwekeza katika mpira ili wapate faida
katika uchumi wao.

Kuna tofauti kubwa sana kati yetu na wao, wakati kwao hakujawahi kuwa
na giza katika akili zao lakini kwetu sisi akili zetu zimefunikwa na
giza kila sekunde ndiyo maana tunakimbia kwa kasi ya kinyonga kwenye
maendeleo ya kila sekta.

Dawa kubwa ya giza ni mwanga, mwanga ni msaada sahihi kwa mtu
aliyekatika giza kuona kwa ufasaha. Mpira ni mwanga sahihi kwenye
biashara ya mtu yoyote, ukiwekeza sehemu inayoungwa mkono na watu
wengi amini sehemu hiyo ni nuru ya biashara yako.

Wafanyabiashara tunao wengi lakini hawataki kujipambanua vizuri
biashara zao kwa faida.

Tumekuwa na zoezi là kuwachangia vijana wa timu ya taifa ya vijana
walio chini ya umri wa miaka 17 tukiwa na kampeni inayosema twende
zetu Gabon mpaka India.

Hili ni jambo jema sana na là kheri sana kwa sababu linaweka
ushikamano wetu pamoja kwa vijana hawa. Lakini ni jambo là aibu sana
kwa wafanyabiashara wenye biashara kubwa hapa nchini kuona mpaka sasa
hivi hakuna hâta mmoja aliyeona hii ni kama fursa ya kibiashara.

Tupo katika duniani ambayo watu tunaishi kwa kuamini kuwa changamoto
ndiyo chanzo cha utajiri wa mwanadamu.

Watanzania tunachangamoto kwenye hili, ila wafanyabiashara wamekaa
kimya na kutokuona hii changamoto kama inaweza ikawa sehemu nzuri kwao
kupanua biashara zao.

Kuna faida nyingi sana kwa mfanyabiashara kama akiamua muda huu
kuwekeza biashara yake kwenye timu hii ya Taifa ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 .

Timu hii inaenda Gabon, na Mungu atasaidia itaenda India kwenye kombe
la dunia là vijana waliochini ya umri wa miaka 17. Hii ni nafasi kubwa
sana kwa mfanyabiashara ambaye ataamua kuwadhamini hawa vijana kwa
sababu kupitia hii safari ya Gabon na India mfanyabiashara huyo
atakutana na wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi mbalimbali kitu
kitakachosaidia kwake yeye kupata marafiki wapya wa kibiashara.

Muda huu Watanzania wanaumoja wa hali ya juu na hamasa kubwa sana
kwenye timu yao hii ya Taifa, na hii ni hali nzuri kwa mfanyabiashara
yoyote kupata faida kubwa na kupanuka zaidi nchi nzima.

Tumekuwa mashuhuda ni jinsi gani ambavyo makampuni mbalimbali yalivyo
kua kwa kasi kubwa na kupata faida kubwa kipindi ambacho waliwahi
kuwekeza kwenye timu ya taifa ya wakubwa kipindi cha Maximo ambapo
walikuwepo Serengeti baadaye wakaja TBL kupitia bia yao ya
Kilimanjaro, wote wawili walipanuka kwa kiasi kikubwa kwa sababu
kipindi kile Watanzania walikuwa wamoja waliunga timu ya Taifa kwa
umoja na nguvu zote hali iliyopelekea kila mtu aliyekuja kuwekeza
biashara yake kwenye timu ya Taifa, Watanzania walimuunga mkono kwa
nguvu zote.

Kwa wakati huu ambao Watanzania wengi wanaiunga Serengeti boys kwa
nguvu zote ni wakati sahihi kwa Mfanyabiashara kuingiza pesa yake
maana atakuwa na uhakika wa kuungwa mkono na hatopata hasara.

Ni wakati mzuri wa kwa Kampuni kama Halotel ,TTCL kujitanua na
kujikuza zaidi na kuwa katika madaraja ya kina Vodacom ,Tigo, Airtel
ambao wako muda mrefu kwenye tasnia hii ya mawasiliano.

Pia hâta kina Vodacom, Airtel, Tigo hii ni fursa nzuri kwao
kujiimarisha zaidi kibiashara kwa sababu muda huu Watanzania wako
tayari kumuunga mkono yoyote anayekuja kumtunza mtoto wao Serengeti
boys.

Kitu kizuri ni kwamba muda huu kwenye shirikisho hakuna migogoro ya
uongozi katika shirikisho là mpira wa miguu yani TFF tofauti na
kipindi cha FAT na hii inaonesha kuwa pèsa za mdhamini yoyote
atakayekuja kuwekeza kwenye timu ya Serengeti boys itakuwa katika
mikono salama.

TFF wamejitahidi sana kupigana kwa nguvu zao zote kuitunza hii timu
mpaka kufikia hapo ilipo. Ni wakati sahihi kwetu sisi kuwatua huu
mzigo na kujitwisha.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

NILICHOKIONA KWENYE BAADHI YA MECHI ZA EPL WIKI ILIYOPITA

ASANTE TFF NA MARCH, APRIL IBEBE MAY