in

MWELEKEO WA RASHID JUMA NI UPI?

Rashid Juma

Mtandao wa habari wa gazeti maarufu la michezo nchini Tanzania la mwanaspoti mnamo Aprili mosi ulichapisha habari ambayo inasema kwamba timu ya poilisi Tanzania imetoa adhabu za kinidhamu kwa wachezaji wake. Mojawapo ya wachezaji waliopewa adhabu hiyo ni ikiwemo na mchezaji ambaye aliwahi kuchezea wababe wa msimbazi kariakoo yaani hapa namzungumzia Rashid Juma. Rashid juma ni mojawapo ya wachezaji waliochipukia katika misimu ya hivi karibuni na baadhi ya wachambuzi walimuona kama ni mojawapo ya mategemeo ya soka la Tanzania katika siku za huko usoni. Hata kocha wa simba wa wakati huo Patrick Aussems alikuwa ana matarajio makubwa kwake na ndio maana akawa anampa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kwa mujibu wa mtandao huo wachezaji hao wamekutwa na makosa ya kinidhamu na kwa pamoja wote walichelewa kurudi kambini baada ya kupewa likizo ya siku kadhaa. Mojawapo ya wachezaji waliopewa adhabu hiyo ni pamoja na Pius Buswita. Kuchelewa kufika kambini ni kosa kubwa sana la kimichezo na mchezaji ambaye huwa anafanya kosa hili huwa anapaswa kuwa na sababu zenye kujitosheleza kuweza kumakinisha benchi la ufundi kumsamehe. Kuchelewa kwake huwa kunaweza kuifanya timu isiweze kujiandaa vizuri katika maandalizi yake katika mechi ambazo inaziendea.

Adhabu hiyo ambayo amepewa Radhid Juma inamuweka katika wakati mgumu kwani kama ikitokea ametemwa na kikosi cha polisi Tanzania basi atakuwa amejiwekea doa ambalo litakuwa limeanza kumchafua na pia atakuwa amejipa wakati mgumu kupata timu kubwa ambayo itaweza kumchukua huku akiwa kwenye hali kama hiyo.  Angejifunza kwa makinda kama Moise kean wa Everton ambaye aliposajiliwa na timu hiyo hakuwa na msaada mkubwa sana hadi ikapelekea kuuzwa kwa mkopo na kwenda kucheza timu ya PSG ufaransa huko PSG amejituma sana na amejikuta ni anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara. Licha ya kean anaweza kumuangalia mchezaji wa timu ya Manchester United ambaye anachezea timu ya west ham kwa mkopo namzungumzia Jesse Lingard. Lingard toka msimu uanze alikuwa hapati muda mzuri wa kucheza na hata akicheza alikuwa anachezeshwa dakika chache basi akaamua kuhamia zake katika kilabu cha west ham chenye makazi yake katika jiji la London. Na wakati akiwa London amerudisha makali yake ya huko awali ambayo yaliwawezesha mashetani wekundu kuweza kubeba kombe la UEFA ndogo. Kasi ile imemfanya kuweza kurudisha nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa.

Rashid hana budi kuomba radhi kwa uongozi wa timu ya Polisi Tanzania na awapigie magoti kwani kwa adhabu waliyompatia ni kubwa kama ukiangalia kwa jicho la mbali nay eye hatakiwi kuvimba kwani yeye ndiyo mhitajia zaidi wa kucheza timu hiyo kuliko wao kumhitajia kama mchezaji. Ni wazi uongozi wa timu hiyo umeona mapungufu kadhaa katika uchezaji wake na sio tu kosa hilo tu alilofanya bali yawezekana kilabu hicho kimeona huduma anayotoa ni ndogo sana kuliko wao kama kilabu wanavyomhudumia. 

Binafsi namuona Rashid ana fursa nzuri ya kurekebisha makosa yake na anaweza kufika mbali kama ataamua kuwa mpole, mnyenyekevu na kujituma zaidi katika mazoezi na huku akiwa anasikiliza maelekezo ya makocha wake. Kiumri bado ni mdogo na ana miaka kadhaa ya kuendelea kucheza soka la ushindani kama akibadilisha tabia yake na kama asipobadilika basi atacheza katika soka la ushindani kwa mda mfupi sana na anaweza asifike mbali kwani soka la sasa linahitajia zaidi nidhamu kuliko kipaji kwani tumeona wachezaji wengi tu ambao walikuwa na vipaji vizuri lakini nidhamu mbovu walipotea mapema sana na hawakuweza kufika mbali na vipaji vyao. Mifano ya wachezaji wa haiba hiyo ni kama vile Mario Balloteli, Hatem Ben Arfa, na wengineo wengi. Bado sisi mashabiki tuna Imani ana nafasi ya kujirekebisha na kasha kurudisha makali yake.

Report

Written by Kahema Fimbo

Mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uzoefu wa kuandika kuhusu habari za michezo anayeishi Dar es salaam Tanzania. Ana uzoefu wa miaka 2 wa kufanya kuandika na kasha kuchapisha Makala zake katika mitandao kadhaa nchini Tanzania. Ni mpenzi na pia ni mdau wa michezo. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vya michezo nchini Tanzania ikiwemo katibu mkuu taifa chama cha mchezo wa kabaddi Tanzania (Tanzania kabaddi sport association), mwenyekiti kamati ya habari chama cha shule za michezo Tanzania (Tanzania sport centres and academies association- TASCA) na pia makamu mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mkuranga( Mkuranga district football association- MDFA).
Nje ya michezo ni mwanajamii na amewahi kujitolea na pia kuwa kiongozi katika taasisi mbalimbali nchini Tanzania za vijana kam vile YOA, TYVA, YUNA, na kadhalika.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
SIMBA SC

Takwimu za Simba zinatisha

TP Mazembe

Nini kimewatokea TP Mazembe?