in , , ,

Mwamuzi wa Chelsea vs Arsenal aliharibu mechi

*Anapenda sana kujishaua*

 

Mwamuzi wa mechi kati ya Chelsea na Arsenal Jumamosi hii uwanjani Stamford Bridge, Mike Dean aliuharibu mchezo uliomalizika kwa wenyeji kushinda 2-0.

Pamoja na umahiri wake katika kazi, ana tatizo ninaloona linamsumbua, mara nyingi akitaka aande juu na kuwa nyota katika matukio mengi.

Dean alichukua hatua ya kumpa kadi nyekundu beki wa kati wa Arsenal, Gabriel Paulista mwishoni mwa kipindi cha kwanza, timu zikiwa suluhu, katika hali ambayo hakuna aliyetarajia wala kuhitaji.

Paulista alipewa kadi hiyo baada ya kuchoshwa na kero za mshambuliaji wa kati wa Chelsea, Diego Costa ambaye tangu dakika za mwanzo za mchezo, alikuwa akionesha maudhi kwa beki huyo na pia kwa Laurent Koscielny.

Ukweli ni kwamba kama ni kutoa kadi nyekundu, Costa naye alitakiwa atolewe nje, kwa sababu mara kadhaa alionekana akivuka mstari, na hata Paulista kujibu hadi kupewa kadi nyekundu ni baada ya rafu za siri na maneno ya kuudhi, ambapo Costa alionekana akimsemesha Paulista sikioni kabla ya Mbrazili huyo kujibu, na Dean akaiendea kadi nyekundu.

Mtafaruku uliopelekea Arsenal kumaliza mechi ikiwa na wachezaji tisa tu...
Mtafaruku uliopelekea Arsenal kumaliza mechi ikiwa na wachezaji tisa tu…

Kana kwamba hiyo haitoshi, Costa alishamrushia mikono Koscielny usoni mara tatu, lakini yeye aliachwa uwanjani hadi kipindi cha pili kocha Jose Mourinho alipoamua kumpumzisha na kumwingiza Loic Remy, wakati huo Chelsea wakiongoza kwa bao moja.

Nimetazama kwa makini marudio ya kipande cha video kuelekea kutolewa kadi hiyo, na kujiridhisha kwamba ama wachezaji wote wangebaki uwanjani au wote wangetolewa, na katika uchambuzi zaidi, si ajabu Costa mwenyewe angetolewa.

Dean amekuwa mtu anayependa akishapangwa kwenye mechi kubwa, afanye kitu kisicho cha kawaida ili kubeba nafasi kwenye vichwa vya habari, na bila shaka picha yake kuoneshwa akiitoa kadi husika au kadi kadhaa.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Arsenal kuwa na wachezaji tisa, kwani dakika 11 hivi kabla ya kipenga cha mwisho, Dean aliikimbilia tena kadi nyekundu na kumpa Santiago Cazorla aliyeonekana kumchezea vibaya Cesc Fabregas. Alimpa Cazorla kadi ya njano ya mapema kabisa ya mchezo huo.

 

advertisement
Advertisement

Ukiwa ni mwamuzi unatakiwa kufuata sheria za soka tu; usitafute umaarufu, usitake kuwa nyota au mtu wa kusifiwa na upande mmoja au kuonekana mbabe ili uogopewe kadiri muda unavyokwenda au kwenye mechi nyingine. Daima ushindi wa timu zikiwa sawa kwa idadi ya wachezaji ndio mtamu.

Ukitazama kwa makini utaona kwamba ni Dean, labda na wenzake tu, walioonesha nia ya kutaka mchezaji Paulista apewe kadi nyekundu. Washabiki wa Chelsea wala hawakuwa na maslahi wala hawakuona haja hiyo, na pia wachezaji wengine wa Chelsea. Paulista alikuwa vizuri tu.

Nina hakika, iwapo hakuna mchezaji ambaye angetolewa nje katika hali ile, hakuna mtu angelalamika na si kazi ya mwamuzi kutafuta kisingizio cha kutoa wachezaji uwanjani, kwani hiyo si kazi yao, na Dean ameangukia mkenge katika hili. Bila shaka atajutia.

Wala hii si mara ya kwanza kufanya jambo kama hili; amekuwa akiharibu mechi kubwa, mechi ambazo wadau wanaingia gharama ya muda na rasilimali nyingine kwa ajili ya kuangalia, kisha wakaishia kupotezewa uhondo na mtu mmoja katika Mike Dean, na wengine sampuli yake.

Watu wanalipa fedha kubwa kuona soka, soka safi na soka ya wote na si kumwangalia Dean akitoa uamuzi kama mwalimu wa shule anayependa kujishaua mbele ya wanafunzi. Hatufiki kwa namna hii.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man City wacharazwa

Tanzania Sports

Van Gaal aota ubingwa