kupanda na kushuka kwa kiwango, uzinzi, ulevi na kupigana na hata uendeshaji magari kwa mchezaji husika.

HIKI ni kipindi cha uhamisho, ambapo ni kawaida kuwapo tetesi nyingi – baadhi hutokea kuwa ukweli na wachezaji wakahama na kusajili kulikotajwa, lakini nyingine hubaki kuwa tetesi tu pasi na ukweli wowote.

Mmiliki

Mfumo mzima hulainishwa na mawakala: jinsi wanavyofanya kazi na jinsi wanavyofanya mambo kufanya kazi. Katika klabu yangu, tumefunga mlango wa hilo sasa. Tulikuwa tukisema tulikuwa tayari kwa yale ambayo mawakala walitutumia lakini katika uzoefu wetu ni karibu pendekezo moja tu kati ya 100 ambalo lilikuwa muhimu, sembuse kufaulu.

Tunaposajili, nitashiriki katika kuchagua walengwa wakuu na nitatuma orodha kwa mkurugenzi wa michezo. Ataangalia uwiano wa kikosi; mambo kama umri, uongozi na utaifa, na kuona nini kinaleta maana kwake. Kisha nitaweka bajeti ikijumuisha ada, mshahara, masharti yanayotarajiwa kutoka kwa wakala na klabu ya kuuza, na tutaichukua kutoka hapo.

Wakati mwingine uko maili nje na mmiliki mwingine hatauza. Kwa hivyo unaendelea. Tunapouza mchezaji ambaye hatutaki kumpoteza, tunajadiliana kulingana na klabu inayotaka. Hakuna maana kuweka ada maalum na kisha kuona moja ya klabu tajiri zaidi ikiingia. Unajaribu kutafuta dili ikiwa mchezaji anataka kuondoka, kwa sababu hutaki kusababisha kutokuwa na furaha kwenye kikosi.

Kwangu , kipindi kibaya zaidi cha mpango wa uhamisho ni juu ya mtititiko unavyokwenda hadi kukubaliana. Klabu yetu haitabadilisha masharti mara makubaliano yakishafikiwa, lakini upande mwingine unaweza kufanya hivyo.

Mimi hujaribu kila wakati kuhakikisha unatumiwa muda mfupi iwezekanavyo kati ya makubaliano na vipimo vya afya, ili hakuna mtu mwingine anayeweza kuingia. Ufanano na ununuzi wa nyumba bado haujatoweka.

Maskauti

Siku hizi, maskauti kwa kawaida ni kituo cha pili kuhusiana na uhamisho. zaidi ya hapo, hatua ya utafutaji mchezaji na utambulishi hufanywa na timu ya wanadata kwenye klabu nyingi, kitu ambacho ni maendeleo makubwa katika miaka ya karibuni.

Skauti hufanya uchunguzi wake na kisha kuiambia klabu husika kwamba fulani anawafaa katika eneo hili au lile. Lazima mcheazji aangaliwe historia yake na kukadiria hali yake inaweza kuwaje siku za usoni au siku nyingi zijazo.

Lazima pia kuchunguza na kujua hali na tabia ya mchezaji husika ndani na nje ya uwanja, hasa masuala ya nidhamu, kuumia mara kwa mara, kupanda na kushuka kwa kiwango, uzinzi, ulevi na kupigana na hata uendeshaji magari kwa mchezaji husika.

Wakala

Maskauti wakishatoa ushauri kuna hatua ya mawakala kushawishi pande mbili husika. Lazima skauti ahakikishe kwamba kitu anachoambiwa ni cha kweli, lakini wakala kazi yake ni kuvutia mambo mazuri kwa yule anayemwakilisha.

Wakala anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye meza ya majadiliano baina ya timu moja na nyingine na mchezaji husika kadhalika. Huyu anaweza kuwa mtu anayetengeneza na kukuza PR, kusimamia mtindo wa maisha, uhusiano, fedha na uwekezaji. Kadhalika kudhibiti mambo yanayozua hisia. Huyu ana kazi nyingi mtambuka. Mchezaji akitokea kuuzwa, basi wakala ana fungu lake hapo.

Mchezaji

Tanzania Sports
2025 transfer window 

Kwa kawaida utasikia juu ya uwezekano wa uhamisho wa mchezaji muda mrefu kabla ya jambo lenyewe kutengenezwa. Kabla ya klabu kuweka ofa mezani, inamaanisha tayari imeshaongea na wakala lakini pia kwa siri na mchezaji mwenyewe ili kumchota. Mchezaji aweza kumwambia wakala: “Sawa, ningependa (nina maslahi) na uhamisho huu.”

Kwa mchezaji, kwa kawaida ni vizuri kujua ikiwa kocha wa klabu husika anampenda, anatamani huduma zake, anamwona kuwa mchezaji anayeweza kuongeza thamani na kubadili kitu kwenye kikosi. Ikiwa hivyo, basi hapo ni vizuri kwa mchezaji. Baada ya hapo sasa mchezaji aweza kuiambia klabu yake: “Nina taarifa juu ya klabu ‘A’ kunitaka. Wanalifanya hilo rasmi sasa.” We una Mawazo gani? Wangependa kufanya biashara? Ndiyo maswali yanakuwa hivyo.

Mara nyingi hutegemea iwapo mchezaji yuko kwenye mwaka wake wa mwisho wa mkataba na klabu yake, basi huanza kuzungumza na klabu yake akisema: “Una mipango gani ya muda mrefu namie? Au msimu ukimalizika mtasajili mtu wa kunibadili? Au tunaanza mazungumzo kwa ajili ya kuongeza mkataba nibaki hapa klabuni?”

Kwa hiyo wachezaji hawana udhibiti wa hatima yao mara nyingi. Mchezaji anatakiwa wakati wote tayari kubadilika kwa kuhama klabu, nchi, ligi, miji na majiji. Soka inakuwa ndicho kipaumbele cha kwanza. Kutokana na kwamba maisha ya soka ya ushindani kwa mchezaji ni mafupi, mchezaji hutakiwa kutafakari kwa makini mbadala wa timu aliyopo na kufanya uamuzi sahihi. Kinaweza kuwa kitendo cha haraka.

Maangalizi ya familia/Watoto

Kutokana na wingi wa safari za mara kwa mara kutoka mji mmoja hadi mwingine au hata nchi moja hadi nyngine, mchezaji anatakiwa kuhakikisha ana mtu au watu wa kuitazama familia yake, hasa Watoto, kuwahakikishia usalama na matunzo/makuzi yanayofaa.

Uratibu

Kitu kingine muhimu ni kuratibu hatua zote hizo na pia kupanga kwa uhakika na kufanikisha siku ya kutiliana Saini. Hayo ni Pamoja na kukata tiketi ya ndege, iwe kukodi kabisa au kutumia ndege za kawaida, kumfikisha mchezaji husika hotelini na kuhakikisha kwamba watu wa pembeni hawamwoni wala kujua mitikasi iliyowekwa na kwamba kuna usalama wa kutosha.

Wengine hupenda kutumia magari ya ‘decoy’ kutoka uwanja wa ndege hadi hotelini kuhakikisha kwamba waandishi wa Habari hawaambulii chochote. Watalitumia pia katika kumpeleka  mchezaji kwa ajili ya vipimo vya afya, huduma za ukalimani na manunuzi.

Timu ya kumhudumia mchezaji itakutana naye mara tano kwa siku kwa wiki kadhaa za kwanza, kwa ajili ya kuhakikisha anapata nyumba na anaifurahia, apate gari, akaunti ya benki, visa, simu na shule ikiwa vyote vinahitajika. Baada ya hapo majukumu hubadilika kwa wahusika, na kuwa kumsaidia kwa mbali au ushauri tu na si kukaa naye muda mwingi kama zile wiki za mwanzo.

Report

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Magoli ya video kwa wenyeji wa CHAN

Tanzania Sports

Shekhan Khamis karafuu ya Kizanzibari