in , , ,

Mourinho ndani Man U?

Katika soka hakuna siku kutakosekana tetesi, na sasa inaelezwa kwamba
kocha mahiri Jose Mourinho amesaini mkataba wa makubaliano tangulizi
kwa ajili ya kuwafundisha Manchester United.

Kocha huyo aliyefukuzwa kazi Chelsea baada ya kuuanza msimu kwa
kuvurunda kuliko alivyopata kufanya popote au timu hiyo kufanya,
anadaiwa kukutana na wakuu wa Old Trafford na kukubaliana hivyo.

Kana kwamba hiyo haitoshi, iwapo Man U watavunja kwa namna yoyote
makubaliano hayo ya awali, basi watatakiwa kumlipa Mreno huyo pauni
milioni 15 kama fidia, ili ajiuguze na maumivu ya kutoteuliwa, jarida
la Hispania la El Pais limeeleza.

Mourinho hana kibarua tangu afutwe kazi Chelsea Desemba mwaka jana na
baada ya kushindwa kuingia Man U wakati Sir Alex Ferguson alipostaafu,
anaona kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kuchukua nafasi ‘yake’, aweke
rekodi ya kufanya kazi kwenye klabu nyingi kubwa duniani.

Inavyowekwa ni kwamba Mourinho ama atateuliwa kushika nafasi hiyo Juni
mosi mwaka huu, vinginevyo wakuu wa Old Trafford waingie benki kumlipa
chake. Kocha wa sasa wa Man U, Louis van Gaal anaonekana
kutowafurahisha wengi klabuni hapo, japokuwa inadaiwa kwamba Makamu
Mwenyekiti Mtendaji, Ed Woodward amekuwa akimtetea.

Wiki iliyopita, Mourinho alisema kwamba anataka kujiunga na klabu mpya
majira yajayo ya joto baada ya “kusoma na kusikiliza uongo kidogo” juu
ya hatima yake. Chanzo cha habari kutoka kwa kampuni ya Gestifute
inayomilikiwa na wakala wa Mourinho, Jorge Mendes ‘Super Agent’
kilithibitisha kwamba Mourinho (53) tayari amemwaga wino tangu mwezi
uliopita lakini Man U wana haki ya kubadili mawazo, ila watagharimika.

“Ikiwa United hawatasaini mkataba wa mwisho kabla ya Mei Mosi, lazima
wamlipe Mouriunho pauni milioni tano ifikapo Juni Mosi; ikiwa hadi
Juni Mosi hawatakuwa wamesaini basi watamlipa tena Mourinho pauni
milioni 10,” taarifa hiyo inasema.

Kifungu hicho kimetumbukizwa humo kwa sababu watu wazito wa Old
Trafford, ikiwa ni pamoja na Sir Ferguson na Sir Bobby Charlton
wanaamini kabisa kwamba Mourinho ndiye mtu sahihi wa kuchukua nafasi
ya Van Gaal.

Zipo taarifa kwamba hata Real Madrid wamekuwa wakifikiria kumchukua
tena ‘The Only One’ kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Zinedine Zidane
aliyepandishwa cheo majuzi baada ya kufukuzwa kazi kwa Carlo
Ancelotti. Hata hivyo, Mourinhop angependelea zaidi kuingia Old
Trafford.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Leicester kama wanamsukuma mlevi

Tanzania Sports

Guardiola awakwaza Man City