in , , ,

Guardiola awakwaza Man City

*Liver hoi, Newcastle, Sunderland doro

Manchester City wana kila kitu, lakini tangu walipoamua kutangaza
kwamba msimu ujao kocha mahiri kimataifa, Pep Guardiola ataingia
Etihad, wameanza kukwazika uwanjani.

Ni kana kwamba wingu la kocha huyo wa Bayern Munich atakayechukua
nafasi ya Manuel Pellegrini linawafunga macho nyakati fulani kiasi cha
kukosa uendelevu katika uchezaji wao.

Jumapili hii walijikuta katika uvuli huo huo na wakaambulia kufungwa,
tena wakiwa nyumbani, mbaya zaidi walikuwa jirani zao, Manchester
United ambao hawajakaa vizuri kihivyo. Alikuwa kinda Marcus Rashford
aliyefunga mapema kipindi cha kwanza na City wakashindwa kuchomoa.

Kinachoonekana sasa ni kwamba kuna athari kisaikolojia kutangaza kocha
mpya mapema kiasi hicho, hivyo kwamba wachezaji wanakuwa wanamsubiri
afike aanze vitu vyake ili wapae, baadhi wakisitikishwa na taarifa za
kuondoka aliyepo na kocha aliyepo pia kukosa ari kubwa.

Kwa hali inavyokwenda, si ajabu msimu ujao City wakacheza Ligi ya
Europa kwa sababu wamebaki na pointi zao 51, juu yao wakiwamo Arsenal
wenye 55, Tottenham Hotspur wenye 61 na Leicester 66.

3500
West Ham na Manchester United wanawapumulia, wote wakiwa na pointi
50, hivyo mechi chache zilizobaki ndizo zitaamua nani awe bingwa,
akina nani watacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), Europa na wa kubaki
hapa hapa kusubiri tena ligi ya msimu ujao.

Spurs wameendelea kuing’ang’ania nafasi ya pili baada ya kuwatandika
Bournemouth 3-0 na wanaifukuzia ndoto yao ya kutwaa ubingwa,
ikishindikana basi wacheze UCL, nafasi ambayo wamekuwa wakiitafuta
miaka mingi bila mafanikio, wakishindwa kwa alama chache kufuzu.

Matumaini ya Liverpool kumaliza katika nne bora msimu huu nayo
yameendelea kufifia, baada ya Southampton kuibuka na ushindi wa 3-2
kwenye mechi ngumu iliyofanyika katika uwanja wa St Mary’s.

Wafuatiliaji walidhani kwamba Liver wangeibuka na ushindi, hasa baada
ya Phelipe Coutinho na Daniel Surridge kufunga mabao katika muda wa
dakika tano tu za kipindi cha kwanza, kisha Saido Mane wa Saints
akakosa penati mapema kipindi cha pili. Penati ilitolewa kutokana na
Martin Skirtel kumchezea vibaya Graziano Pelle.

Hata hivyo, Mane alirekebisha makosa yake kwa kufunga bao baadaye
kidogo, kisha Pelle akasawazisha dakika ya 83 kabla ya Mane tena
kucheka na nyavu dakika tatu tu baadaye. Liverpool walijaribu
kushinikiza wasawazishe lakini hawakumudu, wakaishia kulilia penati na
kunyimwa, baada ya kuona kwamba mshambuliaji wao, Christian Benteke
amechezewa vibaya ndani ya eneo la penati.

*Spurs waendelea kuukaza mwendo EPL

Newcastle, Sunderland doro
Newcastle, Sunderland doro

kwa ushindi huo, wamepanda hadi nafasi ya saba wakiwa na
pointi 47 wakati Liverpool wamebaki nafasi ya tisa, huku mbinu za
kocha Mjerumani,Jurgen Klopp zikionekana kushindwa kufanya kazi kwa
uendelevu.

Kwingineko, sare ya 1-1 baina ya mahasimu wa Tyne-Wear, Newcastle na
Sunderland imemaanisha kwamba wote wanabaki kwenye uvuli wa kushuka
daraja kama hawatajifunga mkanda na kufanya kwenye kwenye mechi
zijazo.

Sunderland walidhani wangeondoka na ushindi kutokana na bao la Jermain
Defoe lililokuja dakika moja tu kabla ya mapumziko, lakini tegemeo la
Newcastle, Aleksandear Mitrovic dakika saba kabla ya mechi kumalizika
lilibadili mwelekeo.

Wakati Newcastle wana pointi 25 wakishika nafasi ya pili kutoka
mkiani, Sunderland wanazo 26, wakiwakalia Aston Villa wanaoonekana
‘kuridhishwa’ na pointi zao 16 na pengine wanatakiwa sasa kufikiria
habari ya Ligi Daraja la Kwanza (Championships), maana kuiepuka
itakuwa ngumu kwa mwenendo wao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Mourinho ndani Man U?

Tanzania Sports

SABABU ZINAZOLINDA KIBARUA CHA VAN GAAL