in , ,

Mourinho kwaheri Real Madrid

*Chelsea wamsubiri ‘mtu wao’ kwa hamu

Sasa ni rasmi kwamba Jose Mourinho ‘The Only One’ anaachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu, baada ya miaka mitatu ya kufundisha miamba hao wa Hispania.
Klabu hiyo imetangaza rasmi kupitia Rais Florentino Perez kwamba uamuzi umeshafikiwa, ambapo Mourinho amekuwa akihusishwa sana na kurejea kwenye klabu ya Chelsea.
“Tumefikia uamuzi kwamba mahusiano yetu kama kocha na klabu sasa yafikie tamati…hakuna mtu aliyefukuzwa bali na maafikiano ya pamoja,” alisema Rais Perez.
Mourinho mwenyewe amekuwa akitajwa kuchukua nafasi iliyo wazi Chelsea, kwa sababu Rafa Benitez alipewa kazi ya muda tu hadi mwishoni mwa ligi iliyomalizika Jumapili hii. Kadhalika, Mourinho alisikika akisema anapenda England, atakwenda anakopendwa na akasema ana mahaba yasiyo ya kawaida na Chelsea.
Mourinho anaondoka wakati ambapo Real wamekuwa nyuma ya mabingwa, Barcelona, kwa pointi 13, lakini aliwashikisha adabu katika mechi mbili za mwisho kwa kuwafunga kwa idadi kubwa ya mabao, kwenye Kombe la Mfalme, ambalo hata hivyo limeishia mikononi mwa mahasimu wao wa Madrid, Atletico. Alisema majuzi kwamba huu ni mwaka wake mbaya zaidi kikazi.
Mourinho anajivunia mafanikio makubwa katika ukocha, ambapo ametwaa Kombe la Mabingwa Ulaya na Porto 2004 na Inter Milan 2010; Kombe la Uefa na Porto 2003; Ubingwa wa England na Chelsea 2005 na 2006; Kombe la FA na Chelsea 2007 na Kombe la Ligi na Chelsea pia 2005 na 2007.
Mourinho ametwaa Ubingwa wa Hispania na Real 2012 na Kombe la Mfalme 2011. Alitwaa Ubingwa wa Italia akiwa na Inter Milan 2009 na 2010, Coppa Italia 2010 na Inter na Ubingwa wa Ureno 2003 na 2004.
Real, hata hivyo, wamepoteza mechi zao zote za nusu fainali kwenye Ligi ya Mabingwa kwa misimu mitatu chini ya Mourinho, na wikiendi hii watakuwa chini ya Mreno huyo watakapoumana na Real Sociedad, kabla ya kuumana na Osasuna dimbani kwao Bernabeu kwa mara ya mwisho.
Rais wa Real alimshukuru Mourinho kwa kazi ngumu na kubwa aliyofanya, na akamtakia kila la heri. Miaka miwili kabla Mourinho kujiunga na Real, timu hiyo haikutwaa kombe lolote lile.
“Timu imeboreshwa na kuwa nzuri katika kipindi hiki cha miaka mitatu, nasi tunamtakia kila la heri,” akasema Rais Perez akimuaga Mourinho ambaye mkataba wake ulikuwa umalizike 2016.
Yapo madai kwamba kocha aliyepata kuwafundisha Chelsea, Carlo Ancelotti atachukua nafasi yake Bernabeu, baada ya yeye mwenyewe kueleza kwamba angependa kwenda huko badala ya kubaki Paris Saint-Germain alikotwaa ubingwa mwaka huu.
Baada ya kutangazwa kuondoka kwake, wadau wa Chelsea wanasubiri upande wa pili kutangaza kumchukua, ambapo tetesi zimeanza kwamba atawasili na Cristiano Ronaldo, anayetajwa pia kuweza kwenda Manchester United.
Chelsea wamekuwa na kawaida ya kubadilisha makocha mara kwa mara, ambapo katika miaka ya karibuni wamekuwa nao Andre Villas-Boas, Roberto Di Matteo na Rafa Benitez anayeondoka.
Kabla ya hapo, kuanzia 1993 wameongozwa na David Webb, Glen Hoddle, Gianluca Vialli, Graham Rix, Claudio Ranieri, Mourinho, Avram Grant, Luiz Felipe Scolari, Ray Wilkins, Guus Hiddink na Ancelotti aliyempisha Villas-Boas 2011.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal sherehe tupu

Fergie kocha bora wa mwaka