in

Molinga,Yikpe, Zahera na Yanga

Dar Young Aricans

Ukilala usingizi mnene yaani fo!fo!fo!! Ukiamshwa na kuoneshwa umbo la  Yikpe unaweza ukadhani Emanuel Adebayor yupo mitaa ya Twiga na Jangwani, kumbe daaa! pasua kichwa.

Mara usingizi haujaisha unaona kipande cha mtu papaa David Molinga mutu ya Kongo hapo utakuwa unasema timu si ndio hii sasa una watu wa maana kule mbele.

Inawezekana maoni yangu yakawa machungu hasa kwa wahusika ila siku zote sisi waandishi ndio huwa tunafuga ugonjwa na kukuza mambo yasiyo na msingi.

Sijui kama hawa wote wawili wamesajiliwa kipindi cha asilimia kumi, ila mbona kama GSM walihusika kwa Yikpe, bado viwango vyao havijakidhi kucheza Yanga huo ndio ukweli . Haya ni maoni ambayo yanahitajika yaheshimiwe kama  wengine wanavyotoa  ya kwao.

Tuanzie hapa, kila navyoangalia uwezo wao uwanjani inanifanya nikubali kuwa kuna uwezekano mkubwa nyota hawa kukatwa katika usajili ujao kwakuwa bado ni maumivu kwa wapenzi wa timu hiyo.

Tangu atue katika timu ya Yanga Yikpe hajawahi kuwa karibu na mashabiki wa timu hiyo, tatizo sio kuwashawishi kwa mdomo bali anatakiwa afanye kazi uwanjani.

Namna anavyopokea mpira , kugeuka na kutoaa pasi kwa  mwenzake imekuwa taabu kidogo, kiwango alichokuwa nacho hata mchezaji wa Ndondo Cup huenda akipewa nafasi akafanya vizuri zaidi yake.

Maskini lile umbo  lake  lilivyokubwa wakati mwingine anaweza kupigwa kikumbo akapepesuka kama mie hapa sasa napata kuhoji hii ndio ‘Level’ yamchezaji wa kimataifa ? au wameingia chaka viongozi wa Yanga.

Nyota huyo ana goli moja tangu atue na hajawahi kufanya kitu cha toufauti yaani kifupi hana maajabu, inawezekana ikawa siku ngumu kwake akiona makala hii ila ukweli siku zote anapata afya mtu anayesema ukweli  kamamie baada ya hapa nitakuwa salama.

Nakuja kuamka kumbe hayo yote nimeyaona usingizini basi kumbe ndoto , ndoto ambayo huenda ina ukweli ndani yake ukapatikana.

Basi nimelala tena namuona Davidi Molinga papa ya mutu ya Kongo, ahadi ya Mwinyi Zahera bado iko kichwani mwangu  alisema kama hajafikisha magoli 15 tumkate mkono wake tena wa kulia ashindwe kuandika.

Aliwaaminisha wana Yanga kuwa Molinga  anaweza  kufunga  magoli 15 nakuendelea je kweli  atafikisha huku akiongezeka uzito ambao nilimuona nao katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ? 

Molinga amefunga magoli 8 ndani ya Yanga  katika msimamo wa wafungaji ligi kuu Bara, sio wastani mbaya sana ila unaweza ukaangalia namna anavyocheza nakusaidiaa  timu uwezo huo upo, ukubwa wa Yanga kweli inafanana nae.

Papa Molinga anaonekana kuridhika sana hasa ikifika kipindi cha mapunziko huwa anajiachia sana, tukumbuke alivyokuja hapa bongo kwa mara ya kwanza alikuwa mnene na maelezo ya Zahera alikaa muda mrefu bila ya mazoezi, hapa sasa miezi mwili tu ameongezeka uzito na anaonekana bado hajawa vizuri.

Ila katika kundi la yeye na Yikpe ukinipa nichague bora ni baki na Molinga, maana huyu mwingine hapana sijawahi kuona.

Tanzania Sports
Yikpe, akiwa kazini

Ndio maana nathubutu kusema kuwa siwaoni katika daftari lampiga kura wa kudumu laYanga msimu wa 2020/21.

Viwango vyao vya kawaida sana hawatishi kama walivyo wengine, tunaona upande wa pili kuna mnyama mmoja anaitwa Mk14 huyu mtu hata akisema ana miaka 50 ila jukumu lake analitimiza  vizuri haina shida.

Pia ninayo sababu yakuona hayo niliyoyasema hasa navyosikia Yanga mpya itakayoundwa kwa wachezaji nyota tena wenyewe wanasema kama mchezaji wa kimataifa awe ana uhakika wakuitwa timu ya taifa lake, kama ni hivyo kwanini nisiwe muwazi kuwa hawa watu lazima watafute pakutokea jiji la Dar es Salaam zito sana.

Je Zahera unaikumbukaa ahadi hii na ikifikaa mwisho wa ligi  nije na panga nikate mkono au utabadili maamuzi kabla haijaisha mwezi mmoja unaokuja.

Hebu tukumbuke kidogo nyota ambao waliwahi kupita Yanga  kama kituko kidogo, namba moja kabisa ni Jama Mba huyu jamaa sijui walimtoa wapi yaani alivyokuja alimulikwa sana na vyombo vya habari ila sasa ndani ya uwanjai ikawa mshikemshike uwanjani,Sadney Urikhob na Issa Bigirimana.

Hii pia inanikumbusha upande wa pili Simba SC nao waliwahi kumsajili mshambuliaji mmoja , waliyemuita Pape N’daw ‘Power Bank’ naye kituko  sana, kwanza alikuwa mrefu kisha vitu hana mguuni kwanini walimuita ‘Power Bank’ nitakujuza siku nyingine.

Yanga na  timu zote ligi kuu Bara mnatakiwa muwe na msimamo wa kuingiza wachezaji wasio na viwango.

Niliwahi kumsikia rafiki yangu mmoja akisema kuwa hata zama za Wenger aliwahi kukosea aliwasajili wachezaji wawili vilaza  Maroune Chamakh pamoja na Yaya Sanogo.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

74 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
mechi ya kirafiki

Simba,Yanga ‘LOCKDOWN’ imewatafuna

Vita ya kubaki EPL

Vita kubaki EPL ngumu