in , , ,

‘Messi ana msongo wa mawazo’

Imeelezwa kwamba mchezaji nyota wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi yupo kwenye msongo mkubwa wa mawazo.

Rafiki yake wa karibu aliyekuwa akicheza naye kwenye timu ya taifa, Pablo Zabaleta anasema hali aliyo nayo Messi si ya kawaida, kwani sonona imemzidi wakati huu wa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.

Argentina walishindwa kuwashinda Iceland, wakaenda sare lakini wakaja kukung’utwa na Croatia kwenye mechi ya pili na kuwaacha wakining’inia, wasijue iwapo watavuka hatua hii, na kigingi wanachotakiwa kuvuka ni kuwafunga Nigeria kwenye mechi ya mwisho ya kundi lao.

Zabaleta anasema kwamba Messi aliyekuwa amejawa raha alimwona mara ya mwisho walipocheza naye 2012 ambapo alifunga mabao matatu (hat-trick) kwenye mechi dhidi ya Brazil jijini New York, akicheza mechi yote kwa uhuru na tabasamu likiwa kubwa usoni mwake.

Lugha yake ya mwili ilikuwa tofauti kabisa kabla ya kuanza kwa mechi dhidi ya Croatia wiki jana, na kwa hakika watu walijawa wasiwasi kumwona Messi akiwa na usononi na kukosa raha kabisa jinsi hiyo.

“Ni rafiki yangu na mchezaji mwenzake wa zamani, kwa hiyo nilimwonea huruma. Ni nadra sana kumwona katika hali hiyo, lakini ilikuwa ishara ya kilichokuwa kikiendelea kichwani mwake – msongo wa mawazo. Nyakati kama hizi, huwa kuna shinikizo kubwa kwake kwa sababu watu wanatarajia makubwa mno kutoka kwake na kwamba afanye kila kitu kwa ajili ya timu ya taifa,” anasema Zabaleta ambaye kwa sasa anakipiga West Ham.

Zabaleta anasema hakushangaa kumwona akihangaika na kushindwa kufanya mambo makubwa uwanjani, kwani mwenyewe akiwa ni mchezaji anajua kwamba ukienda mchezoni ukiwa huna raha ni vigumu sana kufanya vyema. Anasema hilo lilikuwa pigo kubwa sana kwao kama nchi.

“Haikuwa kwa Leo (Messi) tu, bali kwa ujumla timu yote ilifanya vibaya. Tuna bahati sana kwamba bado tuna fursa ya kutumia kusonga mbele kwenye 16 bora kwa kuwafunga Nigeria leo, lakini sijui kama tutafanikisha. Tutatakiwa kufanya vyema kuliko ilivyokuwa kwenye mechi zetu mbili za awali,” anasema Zabaleta aliyechezea Manchester City mechi 230 na mechi 58 kwa timu yake ya taifa kwa wakubwa.

Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli

Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli alionekana kuchanganyikiwa ndani na nje ya uwanja, ambapo aliwatupia lawama wachezaji wengine kwa kutomlisha vyema Messi ili afunge mabao. Hata hivyo, ilielezwa kwamba wachezaji wamemkasirikia na walikuwa wakitaka aondoke kwenye timu, wabaki hata bila kocha.

“(Javier) Mascherano ni kiongozi, Messi analeta utulivu unaotakiwa kwenye timu na (Sergio) Aguero anatia muziki. Huyu anahakikisha muziki sahihi upo kwa kila mtu, kwa kawaida tumekuwa tukisikiliza muziki wa cumbia, muziki wa jadi wa Ufaransa kabla ya mechi. Nimeshakuwa na timu hii ya Argentina wakati mambo yakienda vyema na wakati yalipoenda kombo – hivyo najua jinsi mambo yalivyo,” anasema Zabaleta.

Anaongeza kwamba Messi ni mtulivu sana na huwa hazungumzi mara kwa mara, bali hufanya vitu vyake uwanjani. Kwamba kila mchezaji akimwona akiwa na tabasamu usoni kabla ya mechi, basi kujiamini kwao kunaongezeka kwa sababu wanaona wapo na mmoja wa wachezaji bora kabisa duniani.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA

Tanzania Sports

TETESI ZA USAJILI: