in , , ,

MESSI ALIFANYA KILA KITU SAWA KASORO KUFUNGA GOLI

Baada ya Cristiano Ronaldo kufunga goli tatu yani “hat trick” mzigo mkubwa alibebeshwa Lionel Messi, mzigo ambao alitakiwa kuutua kwa yeye kufunga goli tatu ili kuzima kelele za mashabiki wa Cristiano Ronaldo, lakini hakuweza kufanya hivo.

Ni kweli Lionel Messi alikuwa na mchezo usioridhisha katika mechi ya Jana ?

Pasi mia na kumi na tano (115), mashuti kumi na moja (11) , mashuti matatu (3) yaliyolenga goli huku akitengeneza nafasi tatu (3) za kufunga goli. Hii inatosha kuonesha kuwa Lionel Messi alifanya kila kitu cha kuisaidia timu yake ya taifa kasoro kufunga goli tu. Hivo alionesha kiwango ambacho kilitoa taswira kuwa alikuwa anataka kufanya kitu chenye msaada ndani ya timu yake ya taifa.

Ni kweli Argentina inahitaji mtu mwingine zaidi ya Lionel Messi?

Huu ni ukweli uliowazi, Lionel Messi ni kila kitu katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina, ndiye mfungaji, ndiye mtengeneza magoli, ndiye mpiga pasi. Kwa kifupi timu imetengenezwa kumzunguka yeye.

Anatakiwa atengenezewe mazingira mazuri ambayo yataiwezesha timu ya taifa ya Argentina icheze kitimu kuliko kumwangalia mtu mmoja hasa hasa wanapoenda kushambulia.

Pavon alitakiwa aanze kwenye kikosi cha kwanza?

Bila shaka baada ya yeye kuingia kuna mabadiliko makubwa ambayo yalionekana katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina ambapo aliweza kupiga pasi ambazo zilikuwa na ubunifu ndani ya timu.

Javier Mascherano bado anahitajika katika kikosi cha Argentina?

Ameshinda kila kitu katika ngazi ya klabu, Jana akaweka rekodi ya mchezaji aliyecheza mechi nyingi katika timu ya taifa ya Argentina ambapo amefikisha mechi mia moja arobaini na nne (144).Na Jana alionesha kiwango kikubwa ikiwa ndiye mchezaji aliyepiga pasi nyingi.

Pengo la Segio Romeo lilionekana Jana? 

Hapana shaka hakuna ubishi kwenye hili, Jana alikosekana Sergio Romeo na Argentina walimwihitaji sana katika mechi hii, Willy Cabarello Jana alionesha kiwango cha kawaida ambacho kiliigharimu timu yake.

Safu ya ulinzi ya Argentina inaweza kuifikisha timu ya taifa mbali kwenye michuano hii ya kombe la dunia?

Hapana, Argentina safu ya ulinzi ambayo inafanya makosa mengi binafsi na makosa ya kutofanya “Marking” vizuri. Pia hata mabeki wao wa pembeni hawana msaada mkubwa wanapokuwa wanashambulia. Mpira wa sasa unahitaji pia mabeki wa pembeni kuwa sehemu ya kutengeneza nafasi za magoli ( au sehemu ya mashambulizi).

Di Maria hakustahili kuwepo katika kikosi cha kwanza kilichoanza Jana??

Jana Angel Di Maria alionesha kiwango ambacho cha kawaida sana, kiwango ambacho hakikuwa na msaada mkubwa ndani ya timu yake ya taifa.

Hivo Paolo Dyabala angekuwa mtu sahihi katika mechi hii kwa kucheza katika eneo huru na kumwacha Lionel Messi acheze nyuma ya Aguero. Au Lionel Messi kucheza eneo huru na Paolo Dyabala kucheza nyuma ya Aguero.

Iceland ubora wao ulikuwa wapi?

Tangu walipofanikiwa kufika robo fainali ya Euro 2016 ilionekana ni timu ambayo inacheza kwa pamoja. 

Vivo hivo katika mechi ya Jana. Walikuwa wanashambulia kwa pamoja na kukaba kwa pamoja. Na walikuwa wanakaba njia za mpira pamoja na man to man marking hali ambayo iliwapa wakati mgumu sana Argentina katika mechi hii.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HISPANIA WAMSAHAU JULEN LOPETEQUI NA KUIKUMBUKA BENDERA YAO

Tanzania Sports

JOHN OBI MIKEL- ANAIKABA NIGERIA