in , , ,

MBIO ZA UBINGWA ZIMEFIKIA UKINGONI ?

MANCHESTER DERBY.

Jana kulikuwa na mechi ya Manchester Derby, mechi ambayo ilikuwa inawakutanisha mahasimu wawili ambao msimu huu wanaonekana kama timu ambazo zinauwezo wa kuwa bingwa.

Manchester City walifanikiwa kuvunja rekodi ya Manchester United ya kucheza michezo 41 bila kufungwa katika uwanja wao wa nyumbani, na kufanya washinde mechi 8 zote walizocheza ugenini msimu huu, na kuwa timu ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya England kushinda mechi 14 mfululizo.

Wamefanikiwa kuongeza nafasi ya alama 11 mbele ya Manchester United ambaye anamfuata katika nafasi ya pili. Ongezeko la alama kumi na moja ( 11) inaonesha mbio za ubingwa ndiyo zimefikia tamati ?

Ni mapema sana kusema mbio za ubingwa kuwa zimefikia tamati, ila kwa hali halisi sasa hivi mbio za ƴubingwa zimekuwa ngumu tofauti na awali. Kuongoza kwa tofauti ya alama 11 ukiwa na timu bora na iliyoimarika kama Manchester City ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kuna ugumu zaidi kwenye mbio za ubingwa.

Manchester United walifanikiwa kwa kiasi gani na mbinu za Mourinho ?

Mourinho aliingia na mbinu ya kukaa nyuma ya mpira, wachezaji wote 11 walitakiwa kujilinda kwa pamoja na kushambulia kwa pamoja.

Walifanikiwa sana kujilinda kwa sababu hawakuwapa mwanya Manchester City kupata nafasi za wazi kwa sababu ya kukaba nafasi na njia za mpira.

Kuwaanzisha Martial na Rashford kwa pamoja kulikuwa na maana ya kufanya mashambulizi kwa kushtukiza, jambo hili lilifanikiwa hasa hasa kipindi cha kwanza.

Lingard alikuwa msaada mkubwa kwa kushuka katikati na kuongeza idadi ya viungo wa eneo la katikati.

Valencia na Young waliingia uwanjani kwa ajili ya kutimiza jukumu la kukaba kwa asilimia kubwa.

Mourinho alijua Sane pamoja na Raheem wanakasi na wana madhara makubwa kama wakiachwa huru, hivo Valencia na Young muda mwingi waliutumia nyuma kukaa na Sane pamoja na Raheem, hali ambayo ilipunguza madhara.

Kutoka kwa Kompany kulikuwa na faida au hasara kwa Manchester City?

Falsafa ya Pep mara nyingi ni timu yake kuanza kushambulia nyuma. Wakati Kompany alipokuwepo, safu ya ulinzi ya Manchester City ilikuwa inakaa nyuma sana bila kusogea mbele, hali ambayo ilikuwa inafanya kina Fernandiho, Kevin De Bryune kuwa wanafuata mipira nyuma.

Lakini alipotoka, nafasi yake ikachukuliwa na Gundogan, na kumlazimu Fernandinho kuwa beki, kuliisaidia Manchester City kwa kiasi kikubwa kuanza kumiliki mpira kwa kuanzia nyuma.

Ujenzi wa mashambulizi ulianzia nyuma kwa Fernandinho na timu ikawa imesogea mbele kidogo tofauti na awali ilikuwa karibu na eneo la 18.

Kina Gundogan wakawa na uwezo wa kupata mipira katika eneo la katikati na kupelekea mashambulizi ambayo yaliwafanya Manchester United kufanya makosa.

Baada ya Manchester City kupata walichokitaka ilikuwa rahisi kwao wao kumwingiza Mangala, beki ambaye ana asili kubwa ya kujilinda kuliko Fernandinho.

Kufungwa kwa Chelsea kuna maana ipi ??

LONDON DERBY ( WESTHAM VS CHELSEA).

Kufungwa kwa Chelsea kuna leta picha gani?

Msimu jana Antonio Conte alifanikisha kupoteza alama 21 tu katika harakati zake za kuwa bingwa.

Kufungwa na Westham kunafanya awe na idadi ya michezo 4 aliyopoteza msimu huu, na kumfanya apoteze alama 16 mpaka sasa katika hatua hii ambayo hata raundi ya kwanza haijaisha.

Matokeo haya ni tofauti na matokeo ya msimu jana, hivo kiuhalisia Chelsea wamejiwekea mazingira magumu ya wao kutetea ubingwa wao.

Big Sam na David Moyes wanaweza kuzinusuru Everton na Westham?

Kupata ushindi dhidi ya timu kubwa kama Chelsea kuna manufaa chanya kwenye kikosi cha David Moyes, kwa sababu kitu ambacho walikuwa wanakosa ni morali ya kupata matokeo mazuri.

Unapopata matokeo mazuri mbele ya timu kubwa unaongeza hali ya kupigana zaidi katika kikosi chako. Matokeo haya yatakuwa na faida kubwa sana katika kikosi cha David Moyes.

Big Sam amefanikiwa kuunganisha timu, kuwaunganisha wachezaji wapya na wa zamani kwa pamoja.

Na ndiyo maana timu kwa sasa hivi inapata matokeo mazuri tofauti na mwanzoni. Hata hali ya kupigana imekuwa katika hali ya juu.

SOUTHMPTON vs ARSENAL.

Olivier Giroud

Kitu kimoja kuhusu Arsenal, mabeki wao wa kati wamekuwa na makosa mengi ya binafs.

Jana Per , alishindwa kufanya Clearance nzuri kitu ambacho kilipelekea Arsenal kufungwa goli. Makosa haya binafsi hata katika mechi ya Manchester United yalionekana kwa kiasi kikubwa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Mourinho katika mtihani mgumu zaidi

Tanzania Sports

Ambacho tunakikosa kipo Zanzibar